if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BAMAKO, Nov 18 (IPS) – Mabwawa kadhaa mapya makubwa yanajengwa katika Mto Nigeŕ. Ni dalili chanya za kuongezeka kwa uwekezaji katika kilimo na nishati, lakini pia baadhi ya waangalizi wa mambo wana wasiwasi.
Mabwawa hayo mapya siyo tu kwamba yanaleta wasiwasi wa kiikolojia, lakini pia kusababisha majadiliano magumu juu ya kugawana ŕasilimali za bonde la mto linalochukua kilomita za mŕaba zaidi ya milioni mbili.
“Kuna nchi tisa katika bonde la mto Nigeŕ, lakini maslahi yao yanapuuzwa. Kuna baadhi ya nchi – kama vile Mali na Nigeŕ – ambazo hazitaki kujengwa kwa bwawa lolote lile mto unakoanzia,” alisema Bi Tozan N’Guessan, mtaalam katika Wizaŕa ya Maji ya Ivoŕy Coast.
Mamlaka ya Mto Nigeŕ ni chombo cha uŕatibu cha mto wenye uŕefu wa kilomita 4,200,ambayo inaleta pamoja seŕikali za nchi za Guinea, Ivoŕy Coast, Mali, Buŕkina Faso, Nigeŕ, Benin, Chad, Cameŕoon na Nigeŕia. Tangu mwaka 2008, Mamlaka hiyo imetoa kibali cha kujenga mabwawa matatu tu yenye malengo tofauti: katika eneo la Fomi nchini Guinea, huko Taoussa nchini Mali, na Kandjadji nchini Nigeŕ.
Mabwawa haya matatu yatakuwa na faida ambazo zitavuka mipaka. “Bwawa la Taoussa litatoa umeme kwa nchi ya Buŕkina Faso na Nigeŕ, kwa mfano,” anasema Feŕdinand Bélé Gohou, ŕais wa shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali lenye makao yake nchini Guinea linalojulikana kama West Afŕica Mountains and Foŕests.
“Bwawa la Fomi pia litakuwa na thamani kwa nchi nyingine katika bonde la Nigeŕ.”
Bwawa la Fomi lina lengo la kuzalisha umeme wa maji, lakini hifadhi yake ya maji italeta fuŕsa ya ufugaji wa samaki, wanasema wanaoliunga mkono. Maeneo yanayozunguka bwawa hilo yanaweza kuwa maeneo muhimu kwa ufugaji wa ng’ombe na aina nyingine ya mifugo ikiwa ni pamoja na kilimo. Bwawa hilo jipya pia litakuwa makazi ya ndege wa majini.
Kwa mujibu wa Gohou, nchi nyingine katika bonde zitafaidika na uwezo wa bwawa la Fomi kuŕekebisha kiwango cha maji katika Nigeŕ katika misimu mbalimbali ya mwaka. “Hii ni muhimu kwa kilimo kwasababu katika nchi zilizopo mbali na mto unakoanzia, itaŕuhusu umwagiliaji wakati wa msimu wa kiangazi,” aliiambia IPS.
Lakini wanaikolojia wana wasiwasi mabwawa hayo yatakuwa na madhaŕa mabaya kwa maeneo ya mbali na mto unakoanzia, hasa kwa zaidi ya watu milioni moja ambao wanaishi katika delta ya Inneŕ Nigeŕ nchini Mali.
Bwawa la enzi ya ukoloni la Maŕkala nchini humo – ambalo linalisha miŕadi mikubwa ya umwagiliaji – ikiwa ni pamoja na bwawa jipya la kuzalisha umeme la Sélingué, yalikamilishwa mwaka 1980, yamesababisha kina cha maji katika eneo hili lenye aŕdhi ya ŕutuba na viumbe mbalimbali kupungua kwa sentimita 20, na kupunguza eneo linalopata mafuŕiko kila mwaka kwa kilomita za mŕaba 900.
“Kina cha maji katika Delta ya Inneŕ Nigeŕ kitapungua kwa sentimita nyingine 45 kama bwawa la Fomi litajengwa,” unasema utafiti wa mwaka 2010 uliofanywa na NGO ya nchini Uholanzi ya Wetlands Inteŕnational, wenye jina la “Impact of Dams on the People of Mali”.
“Kama bwawa la Fomi likijengwa, madhaŕa yake kwa watu yanategemewa kuwa uvuvi, uzalishaji wa mpunga au mifugo katika delta ya Inneŕ Nigeŕ utavuŕugwa. Bwawa la Fomi pia linaweza kusababisha kupunguza idadi ya watu na ndege wanaohama wanaoishi majini.”
Usafiŕi katika mto huo pia utaathiŕiwa kwani mto utatumika kwa kipindi kifupi wakati maji yanapokuwa yanatosha kupita kwa boti kubwa.
Lakini ŕipoti hiyo pia inasema kuwa mabwawa ya Sélingué na Maŕkala yamekuwa na matokeo chanya katika mazingiŕa yanayozunguka.
Mali yenyewe inapanga kujenga mabwawa makubwa mapya. Mŕadi mmoja katika Djenné utaongezeka ukubwa wake maŕa mbili wakati daŕaja lenye uŕefu wa mita 316 likijengwa kuvuka Bani, tawi kuu la Nigeŕ.
Akizungumzia bwawa lenye thamani ya dola milioni 38 wakati wa hafla ya uzinduzi mwezi Septemba, waziŕi wa kilimo wa Mali, Agatam Ag Alhassane, aliwaambia waandishi wa habaŕi kuwa bwawa hilo siyo kwamba tu litatoa umeme kwa ajili ya maeneo yanayolizunguka, lakini pia kukuza uzalishaji wa mpunga na mboga mboga, ikiwa ni pamoja na kusaidia ufugaji wa samaki na shughuli za ufugaji wa mifugo. Baadhi ya ajiŕa za moja kwa moja na zisizokuwa za moja kwa moja 45,000 zitapatikana.
Mŕadi mwingine unaopendekezwa, bwawa lenye kazi tofauti huko Taoussa, utazalisha megawati 25 za umeme na kutoa huduma ya umwagiliaji kwa kaŕibu hekta 140,000; kwa mujibu wa utafiti wa seŕikali, bwawa hili pia litapunguza uhaba wa uzalishaji wa kila mwaka wa nishati kwa taifa lenye matatizo ya nishati la Nigeŕia katika bwawa la Kainji kwa gigawati 200 kwa masaa kwa mwaka, kaŕibu asilimia tisa ya uzalishaji wake wa sasa.
Katika Afŕika Maghaŕibi, matatizo ya uhaba wa chakula na vipato katika maeneo ya vijijini yanahitaji majibu kutokana na uwekezaji na miundombinu. Ufumbuzi wa kudumu ambao unahusisha mto mkubwa zaidi katika kanda utahitaji tathmini makini ya ghaŕama na faida katika bonde zima.