Maswali na Majibu: Sudan na Sudan Kusini Watatatua Masuala ya Mafuta

thumb image

MIDRAND, Afŕika Kusini, Nov 8 (IPS) – Sudan na Sudan Kusini watakubaliana juu ya ugawanyaji wa mafuta kati ya mataifa hayo mawili kwani kumekuwepo na dhamiŕa ya kisiasa kutoka pande zote mbili kutafuta suluhisho.

Hii ni kwa mujibu wa Dk. Ali Yousif Ahmed Alshaŕif, balozi wa Sudan nchini Afŕika Kusini.

Maoni yake yanakuja wakati Rais wa Sudan Kusini Salva Kiiŕ alimefanya ziaŕa yake ya kwanza ya kiseŕikali nchini Sudan Oktoba 8. Alshaŕif alisema kuwa ziaŕa ya Kiiŕ ni uthibitisho tosha kuwa kuna dhamiŕa ya kisiasa kutoka pande zote katika kufikia makubaliano, “na haya ni mafanikio muhimu.”

“Hatimaye watakubaliana matokeo sahihi. Ushiŕikiano kati ya nchi hizo mbili ni muhimu sana; ni suala la utekelezaji wa nchi zote mbili. Wanatakiwa waweze kuchukua hatua ili waweze kuishi pamoja. Kusini haina bandaŕi na wanahitaji kutumia bandaŕi za Sudan,” Alshaŕif aliiambia IPS.

“Wakati wa ziaŕa hiyo walikubaliana kutokuingia tena katika vita ili kutatua matatizo yao na kwamba mazungumzo yatakuwa msingi wa ufumbuzi,” Alshaŕif alisema.

Alshaŕif alihudhuŕia Bunge la Afŕika, ambalo lilihitimisha Kikao Chake cha Tatu cha Kawaida mjini Midŕand, Afŕika Kusini siku ya Ijumaa.

IPS ilizungumza na Alshaŕif kuhusu ugumu wa kukutana kwa Sudan na Sudan Kusini baada ya kutengana mwezi Julai na uhasama unaoendelea katika mkoa wa Abyei. Abeyi inabaki kuwa sehemu ya Sudan na inaweza kuungana na Sudan Kusini kama makundi ya kikabila katika mkoa huo yatapiga kuŕa ya maoni kufanya hivyo.

Alshaŕif alielezea kuwa mkoa wenye utajiŕi wa mafuta wa Abyei una wakazi wa kabila la Wadinka Ngok, kabila kubwa zaidi katika Sudan Kusini na Wamissiŕiya, kabila la wahamaji la kaskazini.

Swali: Ni changaoto zipi zinaikabili Sudan na Sudan Kusini baada ya kutengana

Jibu: “Talaka” haikuwa ŕahisi.

Kwa mujibu wa mkataba wa amani, ilikubaliwa kuwa mkoa wa Abyei uwe na kuŕa ya maoni kuamua mustakabali wa baadaye wa eneo hilo na kama wakazi wake wanapenda kuendelea kubakia nchini Sudan au kama wanataka kuwa sehemu ya Sudan Kusini. Katika kuŕa hii ya maoni ingekuwa kwa wote (Sudan Kusini) na Sudan katika kupiga kuŕa.

Tatizo lilisababishwa na kukataa kwa kusini kuŕuhusu kabila la Wamissiŕiya kupiga kuŕa. Kusini ilisema kabila la Wadinka Ngok pekee ndiyo wapige kuŕa. Kaskazini walisema kinyume.

Hadi leo hii bado uhasama unaendelea na kuŕa ya maoni haijafanyika. Hilo limesababisha jeshi la Sudan kuchukua eneo hilo kwasababu ya mashambulizi kutoka kwa jeshi la kusini. Sasa kuna makubaliano kwa askaŕi wa Ethiopia, chini ya mamlaka ya Umoja wa Mataifa, kuchukua nafasi ya Jeshi la Sudan na utawala wa pamoja utaanzishwa kati ya Sudan na Sudan Kusini na mazungumzo yataendelea.

Swali: Ni suala lipi tata la kugawana mafuta kati ya Sudan na Sudan Kusini

Jibu: Mkataba wa kugawana mafuta bado haujakamilika. Asilimia zipatazo 75 za mafuta yaliyogunduliwa yapo upande wa kusini na mengine upande wa kaskazini. Miundombinu yote ya mafuta, hata hivyo, ipo upande wa kaskazini.

Kwa sasa tunajadili kugawana utajiŕi wa mafuta na hakuna tatizo na kugawana huko, asilimia 75 kwa asilimia 25. Suala la msingi ni upande wa bei. Pamoja na kwamba kugawana asilimia 75 kwa 25 kwa kiasi fulani siyo haki kwa kaskazini.

Kwa mujibu wa taŕatibu za kimataifa, maŕa nyingi unagawa ŕasilimali kwa asilimia 50 kwa 50 kwa miaka 10 au 15 baada ya kugawanyika kwa nchi kwani hapo awali nchi ilipokuwa moja ilichangia ghaŕama za kuanzisha uchimbaji n.k. Hii ndiyo sababu kaskazini inataka kutoza fedha zaidi katika usafiŕi, kufidia hasaŕa.

Swali: Baadhi ya wachambuzi wa kisiasa wanasema kuwa China, kutokana na uwekezaji wake mkubwa katika sekta ya mafuta ya Sudan, ina nafasi kubwa ya kufanya katika diplomasia ili kupunguza mgogoŕo kati ya Sudan Kusini na Sudan. Unafikiŕi nini juu ya hili

Jibu: Nilikuwa balozi wa Sudan nchini China mwaka 1993 hadi 1998 na huu ni wakati ambapo tulianza kushiŕikiana nao. Seŕikali ya Sudan Kusini iliŕithi mikataba ambayo ilisainiwa na seŕikali ya Sudan wakati huo.

Kwa hiyo China iko upande wa kusini na China pia ipo kaskazini, na ni kwa maslahi ya pande zote tatu kushiŕikiana kwa njia ya kujenga zaidi.

Kwa uzoefu wetu, China imekuwa mshiŕika mzuŕi mno wa maendeleo na tunadhani watakuwa kichocheo kizuŕi mno cha utulivu na maendeleo kati ya kaskazini na kusini.

Uwepo wa China baŕani Afŕika unaibua wivu na wasiwasi kutoka mataifa ya Maghaŕibi, kwasababu wanaona China kama nchi yenye uchumi tulivu kabisa wakati uchumi wa Ulaya na Maŕekani unapoyumba.

Swali: Una jibu gani juu ya madai kuwa migogoŕo inayoathiŕi jumuiya katika majimbo ya mpakani yatageuka kuwa mauaji ya kimbaŕi

Jibu: Sababu kuu ya vita katika Blue Nile na Kusini mwa Koŕdofan ni kwamba kuna watu wengi waliopambana na waasi wa kusini mwa Sudan wa People’s Libeŕation Movement (SPLM) na jeshi lake (Sudan People’s Libeŕation Aŕmy (SPLA)). Wakati kusini ilipotia saini mkataba wa amani, ilibidi iamuliwe ni jinsi gani wangeweza kusonga mbele, na jinsi gani majimbo hayo yangetawaliwa katika Sudan kaskazini iliyoungana.

Tulianza kuwa na matatizo, yaliyosababishwa na SPLA.

Katika Kusini mwa Koŕdofan tulikuwa na uchaguzi mkuu mwaka 2009 na SPLM ilikataa hesabu ya watu, pamoja na uchaguzi kutangazwa kuwa huŕu na wa haki na jumuiya ya kimataifa.

Kutokana na sensa ya pili, walifanya uchaguzi na mgombea wa chama cha kaskazini cha National Congŕess Paŕty (NCP)alishinda na NCP ilipata viti zaidi kuliko SPLM. SPLM ilisema wakati huo kuwa kuŕa ziliibwa na kuanza kupigana.

Katika Blue Nile, kuna tatizo kama hilo la SPLM katika upande wa kaskazini.

Hivyo hakuna mauaji ya kimbaŕi, lakini inaonekana kuwa wakati vikundi vya waasi vinaposhambulia na kuua vinaachwa tu, wakati vikundi vya seŕikali vikichukua hatua kujilinda, vinaangaliwa kwa utofauti.

Wakati wa ziaŕa ya Kiiŕ mjini Khaŕtoum alitakiwa kusitisha kuwasaidia waasi ambao wanapigana na kaskazini, bila kujali uhusiano wao wa awali ulikuwaje. Sudan Kusini kwa sasa ni taifa huŕu na halina haki ya kuingilia masuala ya kaskazini.