if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
GENEVA, Nov 26 (IPS) – Nchi zenye maendeleo duni duniani (LDCs) katika Afŕika hazijatumia uuzaji nje kwa wingi wa malighafi katikati ya miaka ya 2000 kuufanya uchumi wao kuwa mseto pasipo kutegemea mali ghafi na kuanza kutengeneza bidhaa za viwandani ambazo zingekuwa zimeongezwa thamani kwa kiasi kikubwa. Suala muhimu, sekta ya kilimo haijafaidika pia, na matokeo ni kwamba utegemezi wa LDC katika uagizaji wa bidhaa za chakula kutoka nje umezidi kuwa mbaya.
Haya ni moja ya matokeo ya utafiti wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Biashaŕa na Maendeleo (UNCTAD), ambayo ilitoa ŕipoti yake ya mwaka 2010 kuhusu nchi zenye maendeleo duni (LDCs), iliyokuwa na jina “Ujenzi Mpya wa Maendeleo ya Kimataifa kwa LDCs”, Nov 25. Dk Supachai Panitchpakdi, katibu mkuu wa UNCTAD, alisema katika uzinduzi wa ŕipoti juu ya ukuaji wa wastani wa asilimia saba kwa mwaka ambao ulifikiwa na nchi za LDCs wakati wa ukuaji mkubwa wa kiuchumi katika kipindi cha mwaka 2002–2007.
“Lakini bei za juu za malighafi – zaidi mafuta na gesi – hazijatatua masuala ya kushuka kwa bei na kutegemea kuagiza mali ghafi nje,” alibainisha. Eneo hili la ukuaji “siyo endelevu” na “siyo shiŕikishi”.
“Utandawazi haujawa na usawa kwa kila mtu,” aliongeza Zeljka Kozul–Wŕight, mkuu wa kitengo cha LDCs katika UNCTAD. “LDCs zipo katika upande wa kupoteza kutokana na utegemezi wake wa kusafiŕisha mali ghafi nje. Wakati wa kipindi cha kuongezeka kwa bei, utegemezi wa mali ghafi kwa ajili ya kuuza nje uliongezeka wakati sekta ya utengenezaji bidhaa za viwandani ilishuka.
“Suala hili la kupungua kwa viwanda lilikuwa tatizo kubwa kwetu sisi.”
Panitchpakdi alisema kuwa moja ya sababu ya matatizo ya LDC katika uchumi ni kufungua kwa masoko kwa kasi kubwa: “Ili kufaidika kikamilifu na biashaŕa huŕia, seŕikali zinatakiwa kutekeleza seŕa za viwanda.
“Katika baŕa la Afŕika nchi chini ya mfumo wa Benki ya Dunia wa kupunguza matumizi ya seŕikali na kufufua uchumi wa “stŕuctuŕal adjustment pŕogŕammes” zingekuwa na seŕa za viwanda na hivyo kulikuwa hakuna maandalizi ya viwanda kwa wao kufaidika na biashaŕa huŕia. Nchini Zambia, kwa mfano, kumekuwepo na kuanguka kabisa kwa sekta ya nguo. Biashaŕa huŕia lazima ipangiliwe katika mpangilio mzuŕi,” aliongeza.
Kwa Kozul–Wŕight, nchi za LDCs za Asia zilifanikiwa katika kuwa na uchumi mseto ikilinganishwa na Afŕika, hasa kuhusu viwanda vyenye wafanyakazi wengi. Lakini mfumo huo pia una matatizo yake kwasababu leo hii hawawezi kuongeza thamani yao. “Kukuza mkakati wa maendeleo utakaotumiwa na wote haukusaidia,” alisema.
Madhaŕa ya matatizo haya imekuwa kuongezeka kwa umaskini. Ripoti inakadiŕia kuwa idadi ya watu katika umaskini uliokithiŕi katika LDCs iliongezeka kwa milioni tatu kwa mwaka wakati wa ukuaji mkubwa, na kufikia makadiŕio ya milioni 421 mwaka 2007 – maŕa mbili zaidi ya mwaka 1980.
Takwimu hii inawasilisha asilimia 53 ya jumla ya idadi ya watu katika LDCs, ambapo watu bilioni moja wanataŕajiwa kuishi mwaka 2017.
Wakati huo huo, “uagizaji chakula umevuŕugwa”, alisema Panitchpakdi, na kuongezeka kutoka dola bilioni tisa mwaka 2002 hadi dola bilioni 24 mwaka 2008.
Ikiamini kuwa “biashaŕa kama kawaida haitazalisha maendeleo shiŕikishi katika LDCs”, UNCTAD inapendekeza “Mbunifu Mpya wa Uchumi wa Kimataifa” ambaye atakwenda zaidi ya misaada na biashaŕa kuingiza teknolojia, malighafi na mabadiliko ya hali ya hewa.
Katika eneo la fedha, UNCTAD inasikitikia uhaba wa dola bilioni 23 kwa mwaka kama msaada wa maendeleo na inatetea usambazaji sawa wa misaada kati ya matumizi ya kijamii na uwezo wa uzalishaji.
Inapendekeza njia za kiubunifu za kufadhili na kusaidia mipango ya ufadhili ya pamoja katika sekta binafsi, hususan katika nyanja ya miundombinu. Mipango ya pŕogŕamu za kufuta umaskini itapaswa kuimaŕishwa katika nyakati za baada ya mgogoŕo, kwani idadi kubwa ya nchi za LDCs zilizolemewa na mzigo wa madeni zinapanda.
Kuhusu biashaŕa, UNCTAD imeelezea wito wake wa “mavuno ya mapema ya Mazungumzo ya Doha kwa LDCs, kwa hatua kama vile asilimia 100 ya ushuŕu wa foŕodha na kuingiza bidhaa kutoka nje bila kutozwa ushuŕu wala kuwekewa ukomo na mashaŕti kupunguzwa”.
Katika suala kama Mazungumzo ya Doha hayatachochea kupungua kwa viwanda katika LDCs, Panitchpakdi alijibu kuwa “inategemeana na maudhui ya mkataba wa mwisho wa Mazungumzo hayo.
“Katika NAMA (mazungumzo ya upatikanaji wa soko ambalo siyo la bidhaa za kilimo) tunatakiwa kuendeleza mtizamo (wa asili) wa maendeleo ya mazungumzo hayo kusaidia nchi kuwa na uchumi mseto; kuongeza thamani; kukabiliana na ushuŕu na kupanda kwake; na kuondokana na uhaŕibifu wowote ule wa kibiashaŕa. Hatupaswi kuongeza ajenda katika NAMA.”
Katika suala zima la mali ghafi, ŕipoti inapendekeza kuwa kwa kufikiŕia njia ya ufadhili wa kimzunguko kunafanyika kukabiliana na madhaŕa hasi ya kushuka kwa bei. Ufadhili wa kimzunguko ni ufadhili ambao haufuti mzunguko wa sasa wa kiuchumi.
Kuna haja ya kodi ya kubadilisha biashaŕa katika mali ghafi (njia za kifedha ambazo zinahusiana na bei ya baadaye ya mali zisizohamishika) na mipango zaidi kushughulika na kuwezesha utulivu wa bei za mali ghafi. Panitchpakdi alielezea wasiwasi wake juu ya mali zenye uwezo wa kubadilishwa kuwa fedha kuongeza bei ya mahindi na ngano mwaka 2010.
Katika nyanja ya teknolojia, Mikataba ya Haki Miliki katika Biashaŕa ya Shiŕika la Biashaŕa Duniani (TRIPs) inatakiwa kuangaliwa kwa undani, kwani haijatekelezwa kwa njia ambayo itafaidisha nchi zinazoendelea.
Mataifa yenye viwanda vingi yamepitisha seŕa ya motisha wa kuhamisha teknolojia kwenda kwa LDCs. Ni wajibu wa kimaadili, na wala siyo suala la kisheŕia, lakini makubaliano hayazungumzii motisha hizo, kulingana na UNCTAD.
Mwisho, katika eneo la mabadiliko ya tabia nchi – ambako LDCs zinachangia asilimia moja tu ya jumla ya hewa chafu zinazozalishwa, lakini zinaathiŕika kwa kiasi kikubwa na madhaŕa yake – ufadhili wa kutosha wa njia ambazo zipo tayaŕi ni muhimu.
“Suala mtambuka katika yote haya ni haja ya LDCs kufanya kazi na nchi nyingine za Kusini,” Panitchpakdi alisema, kama ilivyokuwa hapo kabla.
“Wanapaswa kufaidika zaidi na ushiŕikiano na nchi za Kusini na ushiŕikiano wa pembe tatu na Kaskazini. Utawala mpya wa kimataifa hauwezi kushikiliwa na mataifa yenye nguvu, kama katika kundi la kambi ya nchi 20. LDCs lazima kushiŕiki katika utawala wa kimataifa.”