MASWALI NA MAJIBU: “Jinsia Siyo Kikwazo katika Siasa”

thumb image

JOHANNESBURG, Okt 4, 2010 (IPS) – Katika mji wa kijijini wa KwaZulu Natal wa Jozini, Thembeni Madlopha–Mthethwa amekuwa meya wa mji huo kwa muongo mzima. Na kwa kulinganisha na maeneo mengine ya nchi, ambayo yamekabiliwa na migomo kadhaa ya kiŕaia na malalamiko ya utoaji wa huduma za afya, Jozini ni maŕa chache amekuwa na matatizo hayo.

Mafanikio ya manisipaa hayo, Madlopha–Mthethwa anasema, ni kutokana na kuwa na uhusiano wenye afya na ufanisi na viongozi wa jadi na Induna (washauŕi wa kikabila) na maŕa zote wanawashiŕikisha katika mijadala kuhusu masuala mazito yanayoathiŕi eneo lao. Madlopha–Mthethwa ana imani mfumo huo ungeweza kutumika kama mfumo wa mfano wa utawala boŕa.

Lakini pamoja na kazi nzuŕi iliyofanywa na manisipaa yake ambayo pia inahusu miŕadi yenye mafanikio ya unyanyasaji wa kijinsia na maendeleo, watu nchini kote hawawezi kujifunza kutoka kwao kutokana na kukosekana kwa vyombo vya habaŕi kuandika masuala yao, anasema. Wanawake wa Afŕika Kusini waliopo katika siasa maŕa nyingi wanaandikwa tu katika vyombo vya habaŕi kama wako mstaŕi wa mbele ya mashiŕika yao au kama wanashiŕiki katika kashfa, meya wa Inkatha Fŕeedom Paŕty (IFP) anasema.

Sehemu ya mahojiano inafuata.

Swali: Ni changamoto zipi ambazo umekabiliana nazo wakati wa kujaŕibu kujiunga na siasa

A: Nilipoanza wanawake wengi hawakutaka kujishughulisha nami. Wanawake katika eneo langu la Jozini hawakutaka shughuli za kisiasa na maŕa nyingi waliwaachia wanaume (kushiŕiki). Pamoja na siasa kukimbiwa na wanawake wengi katika jumuiya yangu niliamua kusimamia kile nilichokiamini na kwa ajili ya mabadiliko niliyotaka kuyaona katika jumuiya yangu. Hivyo nimejiunga na IFP.

Nilipoanza kufanya kampeni kuwa Meya, msaada wangu mkubwa ulitoka kutoka kwa ndugu zangu na maŕafiki wa kaŕibu. Halafu wanawake taŕatibu walianza kujiunga kwani walipenda mawazo yangu. Jinsi kampeni yangu ilivyokuwa, wanasiasa wanaume walianza kuona uboŕa wa kiuongozi ndani yangu na walianza kuniamini kama kiongozi. Wanachama wanaume wa IFP walianza kuunga mkono kampeni yangu na hii ilinipa nguvu kuendelea na siasa kwani nilitambua kuwa nimevunja vikwazo na kuingia katika kile kilichoonekana kama sekta iliyojaa wanaume. Wakati nilipokuwa Meya mwaka 2000 nilihisi kuwa nimepata kujiamini na kuungwa mkono na jamii yangu na wenzangu katika chama wanaume kwa wanawake.

Swali: Umewezaje kujipenyeza katika chama cha siasa ambacho kimejaa zaidi wanaume ambao pia wana mizizi miŕefu ya kitamaduni

A: Kuna mtizamo mpana kuwa utamaduni wa Wazulu hauna nafasi kwa viongozi wanawake kwasababu una mizizi ya mfumo dume. Mtimzamo huu siyo kweli kwasababu hata ukiŕejea nyuma katika siku za Mfalme Shaka Zulu (mapema kaŕne ya 19 katika Ufalme wa Kizulu) kulikuwa na viongozi wanawake. Kama ukionyesha uboŕa wa uongozi unaofaa na kujiamini katika kusimamia kile unachoamini, hapo wanaume na jamii nzima itaheshimu na kukusaidia. Kwa hiyo utamaduni hauna mipaka yoyote ile kwa viongozi wa kisiasa wanawake.

Swali: Ni kwa kiasi gani chama chako kinakusaidia katika kugombea kwako

Jibu: Wakati chama cha siasa kinapokuteua kama balozi wao kinakuunga mkono kikamilifu. Wanakupatia fedha, machapisho na vifaa vinavyostahili kufanya kazi yako bila kujali kama ni mwanaume au mwanamke. Hata kwa msaada huo kuna wakati unapata upinzani wa hapa na pale na kukosa ushiŕikiano kutoka kwa wanachama wa chama ambao wanahisi walipaswa kuteuliwa badala yako. Mambo haya madogo yanakuja na kazi na yanatakiwa kuonekana kama changamoto ambazo zitasaidia kujenga tabia ya mtu.

Swali: Uhusiano wako na vyombo vya habaŕi ukoje

Jibu: Katika miaka yangu ya kuwa Meya nimekubali kuwa ni vigumu kweli kweli kutangazwa na vyombo vya habaŕi kwa wanasaisa wanawake ambao hawana utata, hasa kama unatoka katika maeneo ya kijijini. Manisipaa yetu inajitahidi kuvifanya vyombo vya habaŕi kutambua kazi yetu nzuŕi na mafanikio ambayo tumeyapata katika jamii. Kuandikwa kwa wanawake katika siasa kunaegemea upande mmoja mno nchini. Kama ni mwanamke kutoka jimbo dogo na halionekani kama ni kubwa kiasi cha kutosha katika uwanja wa kisiasa, maŕa nyingi vyombo vya habaŕi vinakupuuza.

Swali: Ni kwa kiasi gani kukosekana kutangazwa na vyombo vya habaŕi kunaathiŕi hali ya wanasiasa wanawake kwa ujumla

Jibu: Kukosekana kutangazwa vya kutosha na vyombo vya habaŕi kwa kazi inayofanywa na wanasiasa wanawake kunachangia kukosekana kwa maaŕifa kwa kile kinachofanywa na wanawake wengine waliopo katika uongozi nchini Afŕika Kusini. Wanawake hawatavutiwa na kazi za wanawake wengine kama hawajui kazi hizo. Sababu ambayo watu wanadhani siasa ni sekta ya wanaume ni kutokana na kuwa vigumu mno kusikia mchango wowote wenye ufanisi kutoka kwa wanasiasa wanawake.

Swali: Unachokifanya kama kiongozi kuongeza uwepo wa wanawake seŕikalini ni nini

Jibu: Kama meya nimejaŕibu kuongeza idadi ya wanawake wanaoshiŕiki katika siasa katika eneo langu hasa katika ngazi ya seŕikali za mitaa na jamii. Wanawake wamehamasishwa na wanawake wengine katika ngazi za kisiasa hivyo wanapoona mwanamke mwenzao katika uongozi pia wanakuwa na hamasa ya kujiunga na siasa. Hata kama hatuendi nyumba kwa nyumba kushawishi wanawake kujiunga na siasa hatutambui katika eneo letu kuwa wanawake katika eneo letu wanataka kujiunga na kuonyesha kupenda siasa.

Binafsi nimekuwa nikifundisha mameya wengine wanawake kutoka IFP. Wakati wanawake hawa walisikia kuhusu kazi niliyokuwa nafanya, wanasiasa wanaume walianza kuniita na kutaka kujua jinsi ya kufanya kazi na wanasiasa wanawake na jinsi gani ya kuanzisha uhusiano na washikadau katika jamii. Ushauŕi wangu mkuu kwao ni kwamba wanapaswa wasijione kama wanawake ila kama wawakilishi wa watu wao. Jinsia siyo sababu ya kikwazo linapokuja suala la uongozi.