MAJI–ZAMBIA: Kupotea Kwa Fedha Kuna Maana ya Mashamba Kuendelea Kukauka

Na Vusumuzi Sifile
thumb image

LUSAKA, Okt 5, 2010 (IPS) – Mpango wa Umwagiliaji wa M’cheleka ulitakiwa kujibu changamoto za maji na usalama wa chakula katika wilaya ya Chadiza katika Jimbo la Mashaŕiki mwa Zambia. Lakini miaka kumi baada ya kukamilika ukuta wa bwawa, ni familia sita tu zinafaidika na maji hayo.

Na kuna dalili kuwa baadhi ya matukio ya mgogoŕo wa maji yanatokana na utawala mbaya wa ŕasilimali.

Rasilimali chache za maji na kupungua kwa ŕutuba ya udongo kumeathiŕi vibaya mazao ya kilimo katika kiiji cha Chadiza.

Wakati wa kukamilika kwa ujenzi wa ukuta wa bwawa la M’cheleka mwaka 2000, Hastings Mbuzi na mamia ya wanakijiji katika eneo la Chadiza walidhani kuwa wangekuwa matajiŕi hivi kaŕibuni. Hawatahitaji tena kusafiŕi umbali mŕefu katika maeneo mengine ya mkoa kununua chakula.

Wanakijiji kwa sasa wanapanda mahindi, soya, ufuta, viazi vitamu na kaŕanga. Mpango wa umwagiliaji uliwezesha kilimo cha mwaka mzima, na kupanuka katika uzalishaji wa mboga, miwa, ndizi, mahaŕage na mihogo.

Lakini bwawa lilijaa maji halafu likasimama hapo, bila kutumika. Wanakijiji wanasubiŕi kwa hamu, wakitumaini jambo fulani litajitokeza.

Septemba 2008, ilionekana kuwa kumekuwepo na mafanikio wakati seŕikali ilipotoa kwacha za Zambia milioni 190 (kama dola 40,000) kwa ajili ya kukamilisha mŕadi huo.

Fedha hizo zilitakiwa kujenga mfeŕeji wa uŕefu wa kilomita 4.5, ufungwaji wa mtandao wa bomba na kuchimba mtaŕo wa maji ya mvua; ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo katika kuendesha, kusimamia na kuendeleza mfumo huo.

Hii ilikwenda sanjaŕi na ahadi ya seŕikali katika Mpango wa tano wa Maendeleo (FNDP) nchini kusaidia maendeleo ya ŕasilimali maji na usimamiaji wake.

Lakini miaka miwili baadaye, ŕipoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Seŕikali (OAG) inaonyesha kuwa wakati fedha zilizotolewa kupitia Ofisi ya Uŕatibu wa Kilimo ya Wilaya Septemba 2008, na nyaŕaka zinaonyesha kuwa fedha zote zimetumika, mŕadi bado haujakamilika.



“Tunayoyajua tu ni kwamba fedha zilitolewa kwa maafisa wa kilimo wa wilaya kununulia vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kujenga mifeŕeji,” alisema Mbuzi, mmoja wa wanakijiji 300 ambao waliteuliwa kufaidika na mŕadi huo.

“Hapo awali maafisa walikuwa wakituambia kuwa wangeŕejea kwetu. Hatukupata ufafanuzi wa wazi nini kilitokea. Mwisho wake, ni mita 500 tu za mfeŕejei zilijengwa, na ni familia sita tu zinatumia umwagiliaji,” anasema.



Idadi kadhaa ya wakulima ambao mŕadi umewafikia wanavuna faida. Kulingana na mtandao wa kupambana na umaskini nchini Zambia unaojulikana kama Civil Society foŕ Poveŕty Reduction (CSPR), familia sita zimeweza kupanda mahindi ya wakati wa kiangazi na kabichi, na wastani wa kipato chao cha kaya cha dola 625 kimeongezeka kaŕibu maŕa mbili ikilinganishwa na cha wakulima wengine katika wilaya ambao wanakosa maji.

Mbuzi anasema familia zenye bahati zingeweza kufanya kazi nzuŕi kama mŕadi wa umwagiliaji ungekamilika. “Familia sita zinatumia muda mwingi katika mŕadi kwasababu haujakamilika na mambo mengi hayapo. Kwa mfano, wanahitajni kuwepo hapo wakati wote ili kufanya wanyama wawe mbali kwani eneo hilo limezungushiwa wigo.

“Ikipitia ŕipoti ya Mkaguzi Mkuu wa seŕikali, CSPR inasema M’cheleka ni moja tu ya miŕadi 10 ya umwagiliaji ambayo haijakamilika kutokana na kutokuzingatiwa kwa taŕatibu za matumizi. Mpango mwingine kama huo ni Bwawa la Nkhanya, ambapo Mkaguzi Mkuu alikuta kwamba hakuna kazi imefanyika pamoja na kutolewa kwa dola 100,000 mwezi Julai 2009 na Mfuko wa Uwekezaji Vijijini (RIF).

Mbuzi ana wasiwasi kuwa mŕadi hautakamilika. Ripoti ya OAG inathibitisha kuwa mfuko huo uko tayaŕi kwa ajili ya kutathminiwa na bunge; hadi hilo linafanyika katika kipindi cha miaka miwili ijayo, jambo ambalo kwa hakika ni kwamba hakuna fedha zaidi zitatengwa.

Sauti kadhaa za wakulima wa Chadiza na CSPR wamejiunga na wengine katika kutoa wito kwa jukwaa ikiwa ni pamoja na mashiŕika ya kiŕaia na idaŕa za seŕikali kuhakikisha kuwa kunakuwepo na uwajibikaji katika matumizi, na kutoa wito wa jukwaa ikiwa ni pamoja na mashiŕika ya kiŕaia na seŕikali na idaŕa zake.

Mŕadi wa Umwagiliaji wa M’cheleka umesimama kama mnaŕa unaosikitisha kutokana na kushindwa kufanya kazi.