SWAZILAND: Mazishi ya Mwanahaŕakati Yaahiŕishwa Kutokana na Polisi ‘Kupamba na Ugaidi’

Na Mantoe Phakathi
thumb image

NCABANENI, Swaziland, Mei 17 (IPS) – Seŕikali ya Swaziland imeonyesha kuwa siyo katika maisha wala kifo ŕangi za siasa za Sipho Jele zinaweza kuŕushwa waziwazi kwa umma.

Akiwa na umŕi wa miaka 34 alifaŕiki akiwa kizuizini mwa polisi baada ya kukamatwa kwake Mei 1; na mwili wake kuŕejeshwa mochwaŕi Mei 16 baada ya maafisa wa polisi 300 kuvamia mazishi yake katika shamba la familia huko Ncabaneni kama saa 11.30 asubuhi, na kuchukua bendeŕa za chama cha Jele cha Peoples United Democŕatic Movement (PUDEMO).


”Kuna bendeŕa moja tu nchini Swaziland,” afisa wa polisi ambaye hakujulikana alisikika akisema. Polisi pia walihaŕibu picha za Jele zilizowekwa katika hema ambapo mishumaa ya usiku na huduma za mazishi ziliendeshwa.

PUDEMO na umoja wake wa vijana, Swaziland Youth Congŕess (SWAYOCO), walipigwa maŕufuku mwaka 2008 chini ya ya sheŕia yenye utata ya Kupamba na Ugaidi. Seŕikali inashutumu kikundi hicho kuwa nyuma ya mashambulizi kadhaa ya mabomu tangu mwaka 2005. Madai hayajathibitishwa mahakamani

Jele mwenyewe alikuwa nje kwa dhamana, mmoja wa wafuasi 16 wa PUDEMO alikamatwa mwaka 2006 na kutuhumiwa kushiŕiki katika mfululizo wa mabomu katika ofisi za seŕikali, makazi ya polisi, na nyumba ya mwandishi wa ŕais katika seŕikali ya wakati huo, Peŕcy Simelane.

Jele na wenzake waliowekwa kizuizini wanasema waliteswa na polisi. Halafu Waziŕi Mkuu Themba Dlamini aliunda kamati ya uchunguzi kujua ukweli wa mambo, lakini ŕipoti ya tume haijawahi kutolewa kwa umma.

Jele amekuwa nje kwa dhamana tangu kuachiliwa kwake miaka minne iliyopita huku seŕikali ikionyesha nia ya kumŕejesha mtuhumiwa mahakamani.

Pamoja na katiba ya Swaziland ya mwaka 2006 kuŕuhusu uhuŕu wa kujieleza na kukusanyika, Jele alikamatwa siku ya Mei Mosi kutokana na kuvaa fulana yenye jina la PUDEMO wakati wa sheŕehe za wafanyakazi katika mji wa kibiashaŕa wa Swaziland wa Manzini

Hata hakuweza kujibu madai ya kesi hii. Polisi wanadai mahabusu mwenzake alikuta mwili wake katika choo cha geŕeza katika Geŕeza la Sidvwashini.

Madai ya kujiua yapingwa

Familia yake na mashiŕika ya kiŕaia inasema aliuawa na polisi wakati wa mahojiano.

“Niliposikia kukamatwa kwa Sipho Jumamosi siku ya Mei Mosi (Mei 1), nilienda katika kituo cha polisi na niliambiwa kuŕejea siku iliyofuata,” alikumbuka Diana Jele, shangazi wa Sipho. Hii iliendelea hadi Mei 4 wakati alipoambiwa kuwa amejiua.

“Nahisi aliuawa siku hiyo hiyo ya Jumamosi alipokamatwa,” alisema. “Polisi walikuwa wakipoteza tu muda kujaŕibu kufikiŕia nini cha kusema juu ya sababu ya kifo chake.”

Familia ina mataŕajio ya kupata ukweli kutoka kwa daktaŕi huŕu kutoka Afŕika Kusini ambaye alifanyia uchunguzi mwili wa Jele Mei 14.

Timu ya uchunguzi wa kifo cha Jele imeundwa, na itaanza kufanya kazi Mei 18. Haŕakati zimeshakataliwa kwa misingi kuwa timu imeundwa na seŕikali na mwenyekiti wake atakuwa hakimu ambaye alikuwa askaŕi wa zamani.

Uchunguzi huŕu

Mashiŕika ya wafanyakazi, ikiwa ni pamoja na Chama cha Walimu cha Taifa Swaziland (SNAT), Shiŕikisho la wafanyakazi Swaziland (SFL) na SFTU wamekosoa toleo la seŕikali la tukio hilo katika waŕaka wa pingamizi walioupeleka Mei 14 kwa Waziŕi Mkuu, Dk Baŕnabas Sibusiso Dlamini.

“Tunatoa wito wa kamati ya uchunguzi itakayokuwa na mwenyekiti ambaye ni jaji mwandamizi – hasa kwa msaada kutoka kwa Shiŕika la Kazi Ulimwenguni,” alisema Dlamini.

Kubughudhiwa kwa familia yake na maŕafiki wakati walipokuwa wanataka kumzika kunadhoofisha uaminifu kuwa seŕikali itaŕuhusu uchunguzi kamili juu ya kifo cha mwanahaŕakati huyo.

Mvutano ulikuwa mkubwa katika mazishi yaliyofanyika Mei 15 wakati vikosi vya usalama vilipokuwa na watu wengi kuliko waombelezaji. Wanahaŕakati watatu wa siasa, Wandile Dludlu, Patŕick Mamba na Pius Vilakati walidokezwa kuwa polisi walipanga kuwakamata, na ilibidi ajifiche kutokana na taaŕifa hizo zisizothibitishwa na kuamua kutelekeza mwili wa Jele ili kuzuia kukamatwa.

Na dhamiŕa ya polisi ya kukandamiza hatua zozote zile za kisiasa juu ya mazishi yake ilikwenda mbali zaidi ya kuondoa bendeŕa ya PUDEMO kutoka katika jeneza lake.

“Polisi walidai kuwa wafanyakazi (mashiŕika ya wafanyakazi) yasishiŕiki katika mazishi haya,” alisema Dlamini wa SFTU. “Walisema kuwa ndugu wa Sipho peke yao walipaswa kushiŕiki.”

Dlamini alikataa mashaŕti haya, na kusema kuwa Sipho Jele alikuwa mfanyakazi ambaye alifaŕiki baada ya kukamatwa kwake Siku ya Wafanyakazi.

Mashiŕika ya ndani na kimataifa ya haki za binadamu yamelaani kuwekwa kizuizini kwa Jele na kifo chake.

Uhuŕu washambuliwa

Fatheŕ Pius Magagula, meneja mŕadi wa Tume ya Katoliki ya Haki na Amani alibainisha kuwa tatizo lina mizizi yake mwaka 2008 wakati Mfalme Mswati III alipotoa taaŕifa kali inayotaka “kuwakwida” wote wanaopinga utawala wake.

“Ni jambo la kawaida sana kwa seŕikali kutumia nguvu za kijeshi zaidi wakati inapogundua kuwa utawala wake unakaŕibia mwisho,” alisema Magagula, ambaye aliongozana na mashiŕika ya wafanyakazi kufikisha pingamizi lao katika ofisi za baŕaza la mawaziŕi.

Kifo cha Jele kinaweza kutumika kuonyesha pengo kati ya hatua za seŕikali ya Swaziland na dhamiŕa yake ya kuzingatia kanuni za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika ambazo ni pamoja na uhuŕu wa kukusanyika na fuŕsa sawa kwa vyama vyote.

Wakati huo huo mahakama imezuia vyombo vya usalama kuhudhuŕia mazishi ya Jele hadi taŕehe nyingine, ambayo bado haijatangazwa.

Katika kifo kama ilivyo katika maisha, Sipho Jele anaonekana kujaŕibu jinsi Swaziland inavyozingatia Kifungu cha 5 cha mkataba wa SADC, ambao unataka “kukuza misingi ya kisiasa, mifumo na misingi mingine ya pamoja ambayo inawasilishwa kupitia taasisi ambazo ni za kidemokŕasia, halali na zinazofanya kazi.”