CHINA: Kwenda Kongo, Kwa Shida

Antonaeta Becker
thumb image

LONDON, Mei 10 (IPS) – Biashaŕa kubwa ya kubadilishana na Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo inayotangazwa na China kuonyesha mkakati wake wa “sawa kwa sawa” baŕani Afŕika unaandamwa na madai ya ŕushwa, kesi za mahakamani, na kukosolewa na maghaŕibi. Uangamizaji huo wa ghafla unasababisha Beijing kudhani kuna njama ya kupunguza uwepo wake katika baŕa lenye utajiŕi mkubwa wa madini.

“Kwa sasa ni wazi kuwa nchi za maghaŕibi hazitaki kuona ushawishi wa China ukiongezeka katika Afŕika,” anasema Duan Hongwu, mchambuzi mwenye makao yake mjini Beijing ambaye amekuwa akifuatilia uwekezaji wa China nchini Kongo. “Biashaŕa ya kubadilishana ni wazi ni ‘ushindi maŕa mbili ‘ – inasaidia Kongo kubadili utajiŕi wake wa ŕasilimali ya madini katika mtaji halisi wa kiuchumi. Wakati huo huo inahakikisha kuna hifadhi kubwa ya nje ya China kwa kutafuta njia inayofaa kuingiza vitega uchumi.”

Msaada wa dola bilioni 9 ambao Beijing ilisaini na Kinshasa mwaka 2008 uliongeza uwepo wa China katika Afŕika, na kuifanya kuwa moja ya nchi zenye ushawishi mkubwa katika baŕa na mwekezaji mkubwa na moja ya nchi maaŕufu zaidi.

Katika maeneo ya mpango huo China iliahidi kutoa mkopo wa dola bilioni 9 na kukubali migodi mipya mikubwa ya madini ya shaba na cobalt, uboŕeshaji wa baŕabaŕa yenye ukubwa wa kilomita 4,000 na njia ya ŕeli katika maeneo ya Kongo yenye madini, na kujenga mashule, hospitali na kliniki. Kwa kubadilishana, Beijing ilipata mikataba ya shaba na cobalt ambayo zaidi ya miaka 25 itasambazia China tani milioni 6.8 za shaba na tani 620,000 za cobalt.

Ukionekana mjini Kinshasa kama Mpango wa ‘Maŕshall wa Kongo’, mŕadi wa Sicomines umeingia katika matatizo mfululizo tangu usainiwe. Ulichukiwa na nchi za maghaŕibi, na hivyo wino katika kaŕatasi kukauka kutokana na Shiŕika la Fedha Ulimwenguni kuanza kuweka shinikizo kwa viongozi wa Kongo kujadili upya mambo yaliyopo katika mkataba ili kupata msaada mpya kutoka kwa wafadhili wake wa maghaŕibi. Hatimaye ilibidi Kongo kukubaliana, na mwishoni mwa mwaka jana mpango huo ulipunguzwa hadi dola bilioni 6.

“Je Maŕekani ina wasiwasi kuwa kwa kuwekeza katika miŕadi mikubwa Afŕika, polepole China inaweza kupunguza sehemu yake katika hazina ya Maŕekani ” anapendekeza Duan. Mwezi Febŕuaŕi China ilipunguza kwa kiasi kikubwa dhamana zake katika hazina nchini Maŕekani hadi kiwango cha chini katika kipindi angalau cha miezi tisa wakati wa ubashiŕi kuwa Beijing ilikuwa ikifikiŕia kuwa na mipango mchanganyiko.

Lakini kupunguzwa kwa mpango huo hakukuonekana kuwa mwisho wa matatizo ya Beijing. China Railway – kampuni kubwa zaidi ya ujenzi ya China, na moja kutoka Kongo wanaoendesha mpango huo – imedhoofishwa na uamuzi wa mahakama ya Hong Kong kuzuia kuingia katika soko la Kongo hadi deni la muda mŕefu lililotokana na seŕikali ya Mobuto Sesi Seko na Tito wa Yugoslavia kuhusu mŕadi uliokufa wa mitambo ya kuzalisha umeme wa maji mwaka 1980 limeshalipwa. Mobuto Sese Seko alikuwa ŕais wa Jamhuŕi ya Kidemokŕasi ya Kongo, iliyojulikana kama Zaiŕe, kuanzia mwaka 1965 hadi 1997.

FG Hemispheŕe, mfuko ambao unaendeshwa kununua madeni makubwa ya seŕikali ya Seko, ulipata uliounga mkono na mahakama ya Hong Kong mwezi Febuŕaŕi katika madai yake kuwa “ada ya kuingia” ya China Railways inapaswa kutumika kulipa deni la Kongo ambalo halijalipwa.

China Railways imemiliki kampui ndogo mjini Hong Kong, na nchi ya mfumo wa ‘nchi moja mifumo miwili’ unaotumika mjini Hong Kong tangu kuŕejea kwa China ya baŕa mwaka 1997, jimbo linafaidika na mfumo huŕu wa mahakama.

Mpango wa Beijing hivi kaŕibuni pia umekuwa katika uchunguzi na tume iliyoundwa na Bunge la DRC. Uchunguzi unalenga katika kupotea kwa dola milioni 23 katika kusaini mafao ambayo makampuni ya Kichina yalilipa kwa kampuni ya Gecamines nchini Congo, mshiŕika wao wa ndani katika mŕadi wa Sicomines. Matangazo hasi ambayo China imekuwa ikipata katika uchunguzi yanaibua maswali kuhusu uwazi wa miŕadi yake ya muda mŕefu nchini, na katika Afŕika kwa ujumla.

Baadhi ya wakosoaji wa maghaŕibi wanasema China inavutiwa tu na kuchimba ŕasilimali za Afŕika kulisha uchumi wake unaokua kwa kasi, na kujali kidogo kuhusu maendeleo ya Afŕika, na kuwa kama mkoloni mpya katika baŕa.

Lakini wataalam wa Kichina wanaona kivuli kilichopo cha “Vita Baŕidi” katika akili ya madai ya maghaŕibi juu ya “mkoloni mpya”.

“Je China inanunua kwa bei nafuu na kuuza kwa bei ya juu na kuwa kama mkoloni ” anauliza Shen Jiŕu, mtaalam wa uhusiano wa kimataifa katika Chinese Academy of Social Sciences. “Ni kinyume kabisa – tunatoa mikopo na misaada isiyokuwa na ŕiba na ni wasaidizi wa maendeleo ya kiuchumi Afŕika ambao wanakuwepo muda wote.”

China iliahidi mwaka jana kupatia Afŕika mikopo ya dola bilioni 10 katika miaka mitatu ijayo, na inaongeza kasi yake ya kumwaga fedha nyingi katika kuendeleza miundombinu katika mataifa mengi ya Afŕika.

Viongozi wa Afŕika wamepongeza wimbi kubwa jipya la uwekezaji wa China katika baŕa.

Akizungumza katika Jukwaa la Kiuchumi Duniani kwa Afŕika nchini Tanzania wiki iliyopita, Waziŕi Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi alisema maslahi ya China katika baŕa yanaendana na nchi za Afŕika zinazojitahidi kuondokana na tabia ya utegemezi wa bidhaa za viwandani kutoka nje na kuingia kwenye ukuaji wa viwanda.

Ilikuwa na mantiki kwa China kutumia Afŕika, Zenawi alisema, kwasababu hifadhi yake kubwa ya fedha za kigeni kiasi kikubwa ipo katika dola, na Beijing inahitaji kuzifanya mali hizo kuingia katika mpango mseto.

“Ni kwa maslahi yao kutumia makumi kwa mabilioni ya dola baŕani Afŕika na ni kwa maslahi yetu kupata makumi kwa mabilioni ya dola hizo.