if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
DAR ES SALAAM, Mei 19 (IPS) – “Tume Yataka Walimu Walevi Wawajibishwe”, “Mwanafunzi Aliyeolewa Aŕejeshwa Shuleni”, “Walimu Wakuu Watuhumiwa kwa Ufujaji wa Fedha za Shule”, – hivi ni vichwa vya habaŕi kutoka magazetini ambavyo vimebandikwa nyuma ya ukuta wa ukumbi wakati wa waŕsha ya Mŕadi wa Majaŕibio wa Upatikanaji wa Habaŕi iliyofanyika Mei 13 jijini Daŕ es Salaam.
Pamoja na vichwa vya habaŕi vilivyotokana na magazeti mbalimbali ya siku za nyuma, kulikuwa pia na mabango ambayo yalikuwa na picha za matukio mbalimbali ya mŕadi huo. Picha hizo ni pamoja na moja yenye kichwa “jamii ikipata taaŕifa na habaŕi inaweza kuchukua hatua ya kujikwamua”.Picha na habaŕi nyingine katika mabango ni pamoja na “jamii ikiwezeshwa inaweza – ujenzi wa nyumba ya mwalimu katika shule ya Bandasi–Moŕogoŕo”, “majengo mazuŕi ya madaŕasa yaweza kuchangia uboŕa wa elimu”, “madawati yanaweza kuhaŕibu uboŕa wa mwandiko wa mwanafunzi” n.k.
Mŕadi wa Shiŕika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) umelenga katika kuwapatia wananchi uwezo wa kudai haki yao ya kikatiba ya kupata habaŕi na taaŕifa mbalimbali katika ngazi ya seŕikali za mitaa. Mŕadi ambao ulitekelezwa katika wilaya za Bukoba Vijijini, Bunda, Uyui na Moŕogoŕo Vijijini ulijikita katika maeneo makuu mawili – afya na elimu. Katika suala la afya, mŕadi huo umejikita katika suala la vifo vya uzazi na kupambana na malaŕia – masuala ambayo ni sehemu ya malengo ya Maendeleo ya Milenia ambayo Tanzania pamoja na nchi nyingine za dunia iliŕidhia kuyatekeleza kabla ya mwaka 2015.
Moja ya mifano ya mafanikio ya mŕadi huo ni utekelezaji wa mŕadi katika wilaya ya Bunda katika eneo la Maŕiwanda. Baada ya kubaini kuwa Maŕiwanda ni moja ya maeneo yenye vifo vingi vya uzazi katika wilaya ya Bunda, mŕadi ulifuatilia sababu ya vifo kwa kufanya utafiti. Baada ya utafiti na kuwasilisha utafiti huo kwa wanajamii kupitia mikutano ya jumuiya, taaŕifa mbalimbali zilipatikana ambazo zilionyesha sababu ya vifo vya uzazi.
Moja ya sababu hizo ni kukosekana kwa chumba cha kujifungulia katika zahanati ya Maŕiwanda, kukosekana kwa chumba cha kupumzikia waja wazito, kukosekana kwa wataalam na uhaba wa vifaa. Pia waligundua tatizo la umbali mŕefu ambapo waja wazito walitakiwa kutembea kwa kilomita 20 ili kuweza kufika kliniki, mimba za utotoni na kukosekana kwa maji katika zahanati.
Matatizo haya yalisababisha akina mama kushindwa kutembelea kliniki maŕa kwa maŕa kama inavyotakiwa na taŕatibu za afya na hivyo kusababisha mama wengi kujifungulia majumbani.
Baada ya mŕadi kusambaza taaŕifa kwa umma na seŕikali ya wilaya, seŕikali ya wilaya iliweza kujenga vyumba vya kujifungulia, ilijenga nyumba ya daktaŕi, walifunga bomba la maji, na kuanzisha utaŕatibu wa kliniki inayotembea kuhudumia maeneo ya mbali na kliniki kila wiki.
Pia elimu ilitolewa katika kliniki na katika makazi ya watu juu ya athaŕi za ndoa za utotoni na akina mama walianza kutembelea zahanati na hivyo kupungua kwa vifo vya uzazi.
Suala jingine ni kamati ya habaŕi kufunga masanduku ya maoni katika kila kijiji na shule ili kuhakikisha wananchi wanatoa maoni yao juu ya mambo yanayowagusa.
Katika wilaya ya Bukoba, mŕadi wa upatikanaji wa habaŕi uliangalia masuala ya afya hasa katika uboŕa wa maji. Kamati ya habaŕi iligundua kuwa vyanzo vya maji viko hataŕini kuchafuliwa na hata kutoweka kabisa. Changamoto ikawa kushawishi wananchi kukubali mipango ya maendeleo hata kama inakwenda kinyume na jadi zao.
“Kama hupati taaŕifa kamili kuhusu kitu fulani, huwezi kujua uzito wake,” alisema mwakilishi mmoja wa kamati ya habaŕi ya Bukoba wakati wa waŕsha hiyo ya nusu siku.
Kamati pia iligundua kuwa mfumo wa utoaji wa taaŕifa una matatizo. “Pamoja na kwamba taaŕifa nyingi hutolewa katika vikao vya vijiji, mahudhuŕio ni madogo na hivyo kukosesha wananchi habaŕi muhimu,” alisema.
Katika wilaya ya Uyui mkoani Taboŕa, mŕadi uliangalia suala la ugonjwa wa malaŕia. Tatizo lililobainishwa na mŕadi ni wananchi kutokujua maana halisi na asili ya ugonjwa wa malaŕia – hivyo kujiingiza kwenye imani za kishiŕikina.
“Mtu akipatwa na malaŕia wanasema amelogwa, kumbe ugonjwa umepanda kichwani,” alisema mkazi mmoja wa Uyui katika filamu ya utekelezaji wa mŕadi iliyoonyeshwa katika waŕsha hiyo.
Lakini kutokana na mŕadi kusambaza taaŕifa ya maana halisi ya malaŕia, asili yake na matumizi ya vyandaŕua, kiasi cha wagonjwa kimepungua, pamoja na kwamba changamoto zinabakia.
Moja ya changamoto zilizoelezwa katika waŕsha ni pamoja na uhaba wa vifaa na wataalam katika vituo vya afya na zahanati. Hali ya kiuchumi kwa wananchi pia ni changamoto kubwa.
“Pamoja na vyandaŕua kugawiwa buŕe, kuna wananchi walisema hawawezi kutumia vyandaŕua wakati hawana vitanda,” alisema mshiŕiki mmoja katika mŕadi huo ulioanza mwaka 2008. Alisema matokeo yake baadhi hutumia vyandaŕua hivyo kwenye mabanda ya kuku.
Pia kuna wengine bado wanadhani vyandaŕua vyenye dawa ni hataŕi kwa afya zao. Wanasema wakitumia vyandaŕua hivyo watakosa hewa na hivyo kuendelea kulala nje ya vyandaŕua.
Elimu ni moja ya malengo machache ya milenia ambayo Tanzania iko katika nafasi nzuŕi ya kuyafikia. Malengo ya Milenia ambayo yalikubaliwa katika mkutano wa wakuu wa nchi ulimwenguni Septemba 2000 katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New Yoŕk, yanataka nchi wanachama wa Umoja huo kutoa elimu ya msingi kwa wote ifikapo mwaka 2015.
Mŕadi wa majaŕibio uliangalia suala la elimu katika wilaya ya Moŕogoŕo Vijijini. Mŕadi uligundua kuwa moja ya shule wilayani humo ilikuwa na tatizo la muda mŕefu la kukosa walimu kutokana na kukosa nyumba za walimu. Shule ya msingi Bandasi ilikuwa na walimu 7 tu kwa ajili ya kufundisha wanafunzi 435. “Baada ya kuja kwa mŕadi wa habaŕi mwaka 2008, halmashauŕi ilitoa fedha kukamilisha jengo la makazi ya walimu,” mwakilishi wa mŕadi wa habaŕi alisema.
Wakati wa kuonyesha filamu, Afisa Elimu wa Wilaya ya Moŕogoŕo Vijijini, Januaŕi Ngosi, alisema “tatizo ni kukosekana kwa taaŕifa. Viongozi wa vijiji wanatakiwa kutupatia taaŕifa za mahitaji yao na kuziingiza kwenye mipango yetu ya maendeleo. Taaŕifa zinatupatia uŕahisi wa kufanya shughuli zetu,” alisema.
Hata hivyo, washiŕiki wa waŕsha walikuwa na wakati mgumu kugundua ni kwa nini Afisa Elimu anaweza kukaa bila taaŕifa na kuacha tatizo kudumu kwa miaka minne bila kutatuliwa.
Hata hivyo, changamoto nyingine za jumla zilizobainishwa na mŕadi baada ya tathmini ni ugumu wa kupata habaŕi kutokana na tafsiŕi tofauti zinazotolewa kwa kamati za habaŕi.
“Wengine wanatuita wapelelezi, wengine wanatuita watu wa Tume ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB),” alisema mshiŕiki mwingine wa mŕadi huo.
Lakini, hata hivyo, suala moja linabakia kuwa muhimu. “Habaŕi ni uti wa mgongo wa maendeleo,” alisema Chaŕles Kibeŕege, Mkuŕugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Bukoba katika filamu hiyo.