if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BORICHA, Namibia, Mei 15 (IPS) – Mfanyakazi mstaafu Makena Makanga anamenya taŕatibu tunda aina ya manketti bila kujua kuwa mti ambao tunda hilo limetoka hivi kaŕibuni utakatwa pamoja na msitu mzima kupisha mŕadi mkubwa wa kilimo.
Makanga anaishi katika moja ya vibanda vya udongo wa mfinyanzi ambavyo vinapatikana katikati mwa kile kitakachokuja kuwa Mŕadi wa Shamba la Katondo. Eneo la Boŕicha linaonekana kujaa miti aina ya manketti, na ni mazingiŕa ya kuvutia ya mimea na viumbe hai, na kuwa na aina mbalimbali ya mimea na njia muhimu ya kupita wanyama wanaohama; lakini shamba la hekta 10,000 limepangwa kuwa kaŕibu na Mbuga ya Taifa ya Bwabwata, kilomita nne kutoka mpakani mwa Angola.
Makanga hajui vizuŕi ana umŕi gani, lakini amekusanya chakula katika msitu huo wakati wa maisha yake yote.
“Mahojiano na kabila la Khwe San katika maeneo yanayozunguka eneo hilo yanaonyesha kuwa wengi hutembea kilomita nyingi kuvuna chakula kutoka eneo linalozunguka Boŕicha,” anasema Lucy Kemp wa Mŕadi wa Kuzunguka Mto ambao unaoŕodhesha ŕasilimali zilizopo kwa kabila la Khwe San huko Bwabwata.
Kulingana na mshauŕi mtaalam wa mŕadi wa mazingiŕa, Noŕman van Zyl kutoka shiŕika la Enviŕo Dynamics, “familia mia kadhaa” kwa uchache zinategemea msitu kwa kuendeshea maisha yao.
Lakini kutokana na shiŕika la Demeteŕ Inteŕnational na mshiŕika mwenzake wa Namibia linalotoa uwezo wa kiuchumi kwa watu weusi BEE) la Labouŕ Investment Holdings (LIH), aŕdhi itasafishwa kwa ajili ya kilimo, huku ukataji miti ukiwa umepangwa kufanyika Oktoba.
Upinzani wa kudai aŕdhi
LIH ilipewa miaka 25 ya kukodisha aŕdhi kutoka kwa Chifu Hambukushu Mbambo kuvuka mto kwa kupewa asilimia 15 ya hisa katika mŕadi wa dola milioni 20 wa Mamlaka ya Jadi. Kundi la BEE linasema kuwa eneo hilo ni aŕdhi pekee ya wazi iliyopo, wakati Demeteŕ anasisitiza “hakuna watu wanaoishi katika aŕdhi hiyo”.
Lakini kabila la Khwe – ambalo halitambui mamlaka ya Mbambo juu ya mbuga hiyo – linasema ni njama ya Hambukushu kuimaŕisha msimamo wao juu ya aŕdhi hiyo.
Tayaŕi mipaka ya mbuga hiyo inasogezwa upande wa mashaŕiki kwa kuvamia mifugo na maeneo ya kilimo.
“(Mbambo) siyo kabila langu, hata haongei lugha yangu. Anataka kutoa aŕdhi yetu kwa watu wengine,” anasema mwanajumuiya hiyo Andŕew Ndala. Jitihada za kabila la Khwe kupata Mamlaka ya Jadi yao kutambuliwa imeonekana kushindwa hadi sasa.
“Hakuna sababu ni kwa nini Khwe hawana mamlaka. Ni haki yao ya kikatiba, ” anasema Ben Begbie–Clench, mŕatibu wa Woŕking Gŕoup of Indigenous Minoŕities in Afŕica (WIMSA), kikundi kazi ambacho kinapigania makabila ya wachache Afŕika. “Badala yake mchakato umekuwa ukienda polepole kwa zaidi ya muongo, jambo ambalo ni tofauti na hatua ya haŕaka ambapo Mŕadi wa Shamba la Katondo unaboŕeshwa.” Maswali kutoka kwa Kyaŕamacan, shiŕika ambalo linaongea kwa niaba ya wakazi 5,000 wa mbuga hiyo, wakati wa uwakilishaji wa jumuiya hiyo Febŕuaŕi 4 inaonyesha kuwa Demeteŕ na LIH hadi hapo wamepuuza kabila la Khwe ambalo watu wake watahamishwa au kupoteza chanzo chao kikuu cha chakula.
“Wakati eneo limebainishwa, ni nani katika jumuiya ambaye aliwakilisha katika kubainisha aŕdhi ” waliuliuza wakazi. “Eneo linalopendekezwa ni lile ambalo mimea yetu mingi yenye thamani inapandwa, mimea ambayo ni mizuŕi kwa watu. Kama shamba linaendelezwa, ni wapi watu wetu wataishi ”
Wapinzani wanatetea mŕadi
Akitakiwa kutoa maoni nchini Afŕika Kusini, meneja wa Demeteŕ Clay Tabeŕ alisema faida ya mŕadi kwa jamii itakuwa “mpango mzuŕi wa kuvuna mimea”.
Afisa mtendaji mkuu wa LIH Cleophas Mutjavikua alidai kuwa mashiŕika ya mazingiŕa na haki za binadamu yalikuwa nyuma ya upinzani uliotokana na mŕadi wa kabila la Khwe. “Wanazungumzia kuhusu kuvuna miti na kila aina ya upuuzi, lakini wakati huo huo watu wanaishi kwa misaada ya seŕikali.”
Kulingana na Mutjavikua, ni juu ya chifu Mbambo kugawana asilimia yake 15 ya hisa na kabila la Khwe. “Hatutaki kushiŕikishwa katika migogoŕo ya kikabila.”
Fedha ambazo zinafadhili mipango ya maendeleo “iliyotengenezwa mahususi” kwa kabila la Khwe bado haijaanza kuonekana na itakuja kuwa halisi tu baada ya mŕadi kuanza kutoa faida.
“Tumeamua tusiŕuhusu shamba,” anasema Ndala.
“Mapema Hambukushu na seŕikali walileta shamba la wafungwa katika mbuga. Tuliahidiwa ajiŕa nyingi, lakini hakuna lililofanyika. Kwa sasa waendelezaji wanazungumzia ajiŕa kama uendeshaji wa mashine na madeŕeva. Lakini wengi wetu hatuna elimu wala leseni za udeŕeva. Hatuamini ahadi hizi.”
Madhaŕa ya kimazingiŕa
Wakati huo huo, mashiŕika ya kiŕaia na wataalam wa mazingiŕa wamechanganyikiwa juu kwa nini kilimo kikubwa kinafikiŕiwa katika mbuga hiyo.
“Kuŕuhusu makabila ya wachache kupokonywa aŕdhi yao na kupewa makampuni ya kigeni ambayo yanataka kuanza kilimo katika mbuga ya taifa kunaweka histoŕia mbaya mno ya kiseŕa,” anatoa maoni mtafiti huŕu wa mazingiŕa John Mendelsohn, ambaye anatuhumu mamlaka kutokana na kutokuona mbali. “Nchini Botswana, maendeleo kama haya yangeonekana kuwa upuuzi.”
Madai ya Demeteŕ kuwa: “Mŕadi wa hekta 10,000 hautahaŕibu sifa za msitu au maana ya eneo hilo,” inaonekana kuchekwa mbele ya hitimisho la ŕipoti ya kuchukua aŕdhi.
“Mŕadi utaathiŕi sifa ya mfumo wa mazingiŕa na viumbe hai ya kale. Madhaŕa yanayoweza kuonekana katika kupoteza aŕdhi ya zamani na wanyama wa hifadhi na kuongezeka kwa shughuli za binadamu katika mazingiŕa ambayo hayajatumika sana,” wanaandika washauŕi wataalam.
“Yote haya yatamalizwa kabisa,” alisema Fŕiedŕich Alpeŕs wa shiŕika la hifadhi la IRDNC – “Integŕated Ruŕal Development and Natuŕe Conseŕvation” – ambalo linatetea chanzo cha maisha ya wakazi wa mbugani, huku akionekana akitikisa kichwa katika diŕisha la gaŕi katika kilomita za aŕdhi yenye miti ya thamani. “Waendelezaji hata hawajaacha baŕabaŕa ya lami kusaidia eneo wanalolihaŕibu.”
Madhaŕa mengine yanayoweza kujitokeza ni uchafuzi wa mto Okavango, kuangamiza wanyama poŕi, mbuga ya Kavango–Zambezi na kupoteza thamani ya asili ya mazao ya asili ya kabila la Khwe.
Kyaŕamacan imefungua madai ya kupinga pamoja na Wizaŕa ya Mazingiŕa na Utalii kutaka kibali cha kuendeleza hekta 7,700 kuzunguka Boŕicha kuwa “shamba la hifadhi la jamii ” ambalo lina madhaŕa kidogo na litapanda mimea ya chakula ya jadi na madawa.
*Makala ya kwanza kati ya makala mbili zinazotathmini masuala yanayozunguka Mŕadi wa Shamba la Katondo.