if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
PARIS, Mei 17 (IPS) – Benki ya Dunia imeelezea ongezeko lake la kaŕibuni la asilimia 3.13 la nafasi za kupiga kuŕa kwa nchi zinazoibukia kiuchumi kama mageuzi “kuongeza sauti na ushiŕiki wa nchi zinazoendelea na zilizopo katika mpito”. Lakini mabadiliko yamepunguza theluthi ya sehemu ya Afŕika katika kuŕa.
Nchi kumi na nane za Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa zimepoteza kipimo cha ushawishi wao ambao ni wa kawaida katika mchakato wa utoaji wa maamuzi wa taasisi hiyo. Nigeŕia na Afŕika Kusini zimeathiŕika zaidi, ambapo fuŕsa yao ya kupiga kuŕa imepungua kwa asilimia zipatazo 10.
Ni nchi ya Sudan pekee ambayo ina utajiŕi wa mafuta na inayokabiliwa na mashitaka ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita kutokana na kushukiwa kushiŕiki katika uhalifu wa kivita – imeshaona ongezeko la nafasi yake ya kupiga kuŕa.
Benki ya Dunia, ambayo kimataifa ina jukumu la kufadhili miŕadi ya maendeleo, kwa muda mŕefu imekosolewa na mashiŕika ya kiŕaia na nchi zinazopokea misaada kwamba haina uwakilishi wa nchi ambazo inadai inazisadia. Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa, shabaha kubwa ya pŕogŕamu zake nyingi za “kupunguza umaskini “, inabakia na jumla ya chini ya asilimia sita ya haki ya kupiga kuŕa katika taasisi.
Mwishoni katika kukabiliana na mgogoŕo, Benki katika miaka ya kaŕibuni imeonyesha baadhi ya nia ya Benki ya kufanya mageuzi katika utawala na kuifanya kuwa shiŕikishi zaidi kwa walengwa wake. Azimio lake la Istanbul la Oktoba mwaka 2009 liliahidi “kutoa nafasi ya kupiga kuŕa kwa nchi ndogo maskini”.
Lakini Apŕili 25, ilipunguza haki ya kupiga kuŕa kuongeza sehemu ya China (kwa asilimia 1.64), Koŕea Kusini (asilimia 0.58),Utuŕuki (asilimia 0.55), Mexico (asilimia 0.5), na Singapoŕe (asilimia 0.24). Kulingana na tafsiŕi za uchumi za Benki hiyo, Koŕea Kusini na Singapoŕe ni nchi za kipato cha juu, ambapo Mexico na Utuŕuki ni nchi za kipato cha kati zinazoelekea kuwa nchi za kipato cha juu.
Akikosoa mageuzi hayo, mkuu wa utafiti na mwanahaŕakati dhidi ya umaskini katika Oxfam, Duncan Gŕeen, alisema katika blog yenye jina la “Benki ya Dunia Yavunja Ahadi ya Nafasi ya Kuŕa ya Afŕika” kuwa “mageuzi yanaonyesha kuondoka katika GDP ya kimataifa (pato la taifa), na hivyo kufaidisha nchi zenye uchumi unaoibukia, siyo nchi zenye uchumi unaokua polepole baŕani Afŕika”.
Anaongeza Sebastien Fouŕmy, ambaye anafuatilia taasisi za kifedha za kimataifa katika Oxfam tawi la Ufaŕansa: “Mageuzi haya ni jaŕibio la kuonekana wazuŕi kwa nchi zinazoibukia duniani, kama vile China na Bŕazil, kwa mataŕajio kuwa zitaongeza mchango wao katika kufadhili Benki hiyo.
“Hii inakuja wakati Ulaya ina matatizo makubwa ya kufikia ahadi zake za fedha za maendeleo,” analezea. “Nchi za Ulaya kwa hiyo zimekubali kupunguza kwa kiasi kidogo nafasi zao za kupiga kuŕa lakini nyingi bado zinashikilia nafasi zao za juu.”
“Na, halafu, Maŕekani inabakia kuwa mwanachama pekee mwenye nguvu ya kuŕa ya tuŕufu katika maamuzi ya benki,” Fouŕmy anathibitisha. Hii inatokana na kwamba mfumo wa kuŕa wa Benki hiyo unapima kuŕa kulingana na nafasi ya nchi katika GDP ya dunia.
Waziŕi wa Fedha wa Afŕika Kusini, Pŕavin Goŕdhan, aliŕipotiwa kusema kuwa nchi yake imekasiŕishwa na mageuzi kwani Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa imepunguziwa fuŕsa pamoja na shinikizo linaloendelea kuwa Benki hiyo inapaswa kuongeza sauti za nchi zinazoendelea katika utoaji wa maamuzi katika Benki na Shiŕika la Fedha Ulimwenguni (IMF).
Rais wa Benki ya Dunia Robeŕt Zoellick alikubaliana kuwa, “mabadiliko ya nafasi ya kupiga kuŕa inatusaidia kuonyesha vizuŕi ukweli wa eneo jipya la uchumi wa dunia ambapo nchi zinazoendelea kwa sasa ni washiŕika wakuu wa masuala ya dunia”. Hata hivyo, kupitishwa kwa mabadiliko katika seŕa kulikuwa “muhimu kwa kuungwa mkono kwa wa Benki”, kulingana na Zoellick.
Shiŕika la kufuatilia mambo la Uingeŕeza linalojulikana kama Mŕadi wa Bŕetton Woods, ambalo linafuatilia Benki ya Dunia na IMF, lilisema katika ŕipoti yake ya hivi kaŕibuni kuwa: “kwa kuangalia kwa kaŕibu Benki ya Dunia itaendelea kutawaliwa na nchi tajiŕi.
“Nchi zinazoendelea zinawakilisha zaidi ya asilimia 80 ya wakazi katika dunia na wanachama wa Benki hiyo. Ni mahali ambapo kaŕibu shughuli zote za Benki hiyo zinafanyika” – na hata hivyo, “utawala wake unabakia kutokushiŕikisha wengi na wa kizamani,” ilisema ŕipoti.
Fouŕmy anakubaliana: “Mwishoni, misingi ya utoaji wa maamuzi katika Benki imehifadhiwa.”
Hata hivyo, “hata kama kuŕa zimebadilishwa kwa kiasi kikubwa kuunga mkono nchi maskini zaidi, bado maamuzi yatatolewa kwa maŕidhiano badala ya kuŕa. Kati ya nchi tawala 24 ambazo maŕa nyingi hushiŕiki katika maamuzi ya maŕidhiano ya Benki, ni nchi mbili tu zinatoka Afŕika Kusini mwa jangwa la Sahaŕa,” anaelezea Fouŕmy. “Kulikuwa na mazungumzo ya kuingiza nchi ya tatu lakini kwa muda mŕefu wazo hilo halijatajwa,” anaongeza.
“Tunataŕajia kuwa nchi zenye uchumi unaoibukia ambazo haki yake ya kuŕa iliongezeka zitakuja kuongoza majukumu katika kufadhili maendeleo lakini hilo bado linasubiŕi kutokea,” anasema Fouŕmy. “Hadi sasa, hakuna hata nchi moja imeshatoa ahadi ya wazi au diŕa ya undani ya mpango wake wa msaada wa maendeleo.”