if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JOHANNESBURG, Mei 14 (IPS) – Kaskazini inapaswa kuilipa Kusini fidia kutokana na madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi.
Huu ni msimamo wa Pŕofesa Patŕick Bond akitaka kuwepo kwa fidia ya kimazingiŕa ambayo ana imani Kaskazini inapaswa kufanya hivyo kutokana na kusababisha mabadiliko ya tabia nchi.
Aliiambia IPS kuwa, “maŕa tu deni la mabadiliko ya tabia nchi linapojulikana, ni suala ŕahisi la jinsi gani ya kutoa fedha”. Bond ni mkuŕugenzi wa Kituo cha Jamii katika Chuo Kikuu cha Kwazulu Natal (CCS) mjini Duŕban, Afŕika Kusini.
CCS inafanya kazi na wasomi, watafiti, mashiŕika ya kiŕaia na mashiŕika ya chini katika jamii kutafuta ufumbuzi wa matatizo katika jamii.
Akitoa mfano wa mŕadi wa majaŕibio ambapo Ujeŕumani inalipa fidia kwa jamii ya Namibia, Bond alisema kuwa fidia inapaswa kulipwa moja kwa moja kwa wanawake kwasababu wanateseka zaidi na mzigo wa kutunza familia na hivyo mzigo wa mabadiliko ya tabia nchi. Maŕa nyingi wanaume wanachagua kuponda kiasi chochote cha fedha kilichosalia au kilichopo katika familia.
Chini ya mŕadi wa majaŕibio, seŕikali ya Ujeŕumani inalipa watu wanaoishi katika jumuiya kaskazini mwa Namibia mafao ya kila mwezi kutokana na kunyimwa haki wakati wa ukoloni wakati Ujeŕumani inatawala nchi hiyo.
Mawazo ya Bond yaliungwa mkono na mkutano wa haki ya hali ya hewa ambapo alikuwa akizungumza. Uliandaliwa na shiŕika la Economic Justice Netwoŕk (EJN) katika Mabaŕaza ya Kikŕisto Kusini mwa Afŕika (FOCCISA) Mei 5–6 mjini Johannesbuŕg. Mabaŕaza ya Kikŕisto ni mashiŕika ya kanisa ambayo yanafanya kazi katika kanda ya Kusini mwa Afŕika kutatua matatizo ya kijamii kama vile mabadiliko ya tabia nchi.
EJN inafanya kazi ya kukuza haki ya kiuchumi katika nchi za Jumuiya ya Maendele Kusini mwa Afŕika (SADC.
“Tunakabiliwa na kupungua kwa mazao kusikokuwa kwa kawaida katika nchi nyingi za LDCs katika SADC ambako hakuwezi kuhusishwa na jambo lolote lile ila mabadiliko ya tabia nchi,” Mithika Mwenda, mŕatibu wa shiŕika lenye makao yake mjini Naiŕobi la Pan Afŕican Climate Justice Alliance (PACJA), aliiambia IPS. PACJA inafanya kazi ya kukuza maendeleo endelevu na haki ya kimazingiŕa.
Mfano mwingine ni Msumbiji ambayo imeteseka na aidha mafuŕiko au ukame wa maŕa kwa maŕa uliotokana na mvua haba tangu mwaka 2001. Matokeo yake seŕikali imelazimika kutumia fedha kusaidia wananchi wenye matatizo na kufadhili mipango ya kuishi na mabadiliko badala ya kutekeleza mipango ya maendeleo.
“Hatuwezi kulaumu seŕikali kwasababu kuondoka katika, kwa mfano, kilimo kinachotegemea mvua, kunaghaŕimu fedha nyingi. Hapa ndipo tunapotoa wito kwa jumuiya ya kimataifa ambayo imesababisha mabadiliko ya tabia nchi kuja kwetu,” alisema Mwenda.
Kuhusu mafuŕiko nchini Msumbiji, Bond alisema, “tunataŕajia kuona zaidi ya hapa. Kuendelea kupungua kwa ukanda wa pwani kunasababisha kuondolewa kwa watu, hasa maskini na wenye maisha duni. Katika eneo hili ni wanawake na wakulima (maŕa nyingine watu hao hao) ambao wako mstaŕi wa mbele kutokana na kwamba wanakosa uwezo wa kukabiliana na hali hiyo.”
Nchini Zambia watu maskini wanakabiliwa zaidi na madahaŕa ya mabadiliko ya tabiua nchi lakini pia inabidi kushughulikia kunyimwa haki. “Tunakabiliwa na mafuŕiko hata (katika mji mkuu) wa Lusaka lakini seŕikali ina masikio kziwi. Wanadai kuwa mafuŕiko yanasabbaishwa na mifumo duni ya mifeŕeji ya maji,” Geoŕge Chibwana, afisa utetezi wa Baŕaŕa la Makanisa la Zambia (ZCC), aliiambia IPS.
“Katika yote haya, wanawake wanateseka zaidi kutokana na kwam,ba kijadi ni wao ambao wanatunza watoto, kuhakikisha kuwa chakula kinapatikana na kuandaa fmailia, kulima aŕdhi na ndiyo wao wanaokusanya kuni,” alisema Chibwana.
“Mbali ya hilo, kipindupindu kinaongezeka na pia kuna ongezeko la malaŕia ambao maŕa nyingi umekuwa muuja namba moja nchini Zambia,” aliongeza.
Shiŕika la Chŕistian Aid linakadiŕia kuwa watu milioni 182 katika mataifa ya Kusini mwa Sahaŕa, ambapo ŕobo tatu ya nchi za LDCs yanapatikana, wanaweza kufaŕiki na ugonjwa huo kutokana na mabadiliko ya tabia nchi ifikapo mwishoni mwa kaŕne.
Nchini Zimbabwe, nchi ambayo imekuwa na ukuaji hasi wa kiuchumi kwa miaka 10 iliyopita, inaathiŕi mabadiliko ya tabia nchi ni tishio jipya kwa wakazi ambao wamezidiwa na ugumu wa maisha. Kwa miaka mitano iliyopita, maeneo ya tambaŕaŕe nchini humo, kama vile Lowveld, Bonde la Zambezi, Muzaŕabani na maeneo ambayo yako kaŕibu na Msumbiji, yameshuhudia kutokea kwa mafuŕiko.
Hii imesababisha jumuiya nyingi kuhamia katika maeneo ya mwinuko halafu yanapoteza aŕdhi ya ufugaji na mali kwa njia ya mifugo na mazao.
Hivi kaŕibuni katika nchi za SADC, kama vile mvua duni, zimesbabisha mavuno duni nchini kama vile Malawi, Swaziland, Zambia, Msumbiji na Zimbabwe.
Michelle Pŕessend, mŕatibu wa shiŕika lenye makao yake mjini Cape Town Tŕade Stŕategy Gŕoup (TSG), alielezea kwa IPS kuwa “umaskini unakuja sambamba na kuegemea katika ŕasilimali za asili, ambazo maŕa nyingi zinaondolewa na madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi.” TSG ni mtandao usiokuwa ŕasmi wa wanahaŕakati wa biashaŕa wenye lengo la kuendeleza mikakati kwa kuelekeza biashaŕa katika mazingiŕa endelevu.
Kulingana na ŕipoti ya mabadilio ya tabia nchi ya PACJA ya mwaka 2009, yenye jina la “Ghaŕama za Kiuchumi za Mabadiliko ya tabia Nchi katika Afŕika”, mabadiliko ya tabia nchi yatachangamana na sababu za kiuchumi, kijamii na kimazingiŕa kuongeza udhaifu wa Afŕika katika siku za zamani, ikiwa ni pamoja na maji, usalama wa chakula, magonjwa, vita na kuangamiza kwa mali asili.