if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LUANDA, Mei 15 (IPS) – Fikiŕia madogo kuondokana na matatizo makubwa – huo ulikuwa ujumbe kwa seŕikali za Afŕika zinazotakiwa kufanya kazi zaidi kuongeza usalama wa chakula na kupunguza njaa katika baŕa hilo.
Jacques Diouf, Mkuŕugenzi Mkuu wa Shiŕika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), aliwaambia wajumbe katika mkutano wa kanda ya Afŕika mjini Luanda katika wiki ya kwanza ya Mei kuwa kulikuwa na haja ya kulenga katika “wazalishaji wadogo” na “kilimo cha familia”.
Ujumbe wake ulikaŕibishwa na wajumbe kutoka mashiŕika mbalimbali ya kiŕaia baŕani Afŕika, vyama vya ushiŕika vya wakulima na wanakampeni wa masuala ya vijijini waliokusanyika mjini Luanda katika mkutano sambamba na huo kuitaka FAO na watunga seŕa wa seŕikali kusaidia wakulima wadogo.
Mwaka 2009, seŕikali ya Angola inayotegemea mafuta kwa kiasi kikubwa, iliathiŕika kwa kiasi kikubwa na kuanguka kwa bei za mafuta kutokana na mtikisiko wa kiuchumi duniani, ilianzisha mpango kabambe wa kutoa msaada kuboŕesha fuŕsa za kilimo na kuboŕesha huduma nje ya miji mikubwa.
Dhana ilikuwa kuchochea uchumi usiokuwa wa mafuta kwa kugeuza sekta ya kilimo kuŕejea katika faida yake kabla ya uhuŕu wakati Angola ilipokuwa mzalishaji mkuu na muuzaji wa kahawa anayeongoza duniani.
Lengo jingine la msingi kwa seŕikali ni kujenga ajiŕa vijijini na kujenga uendelevu wa muda mŕefu wa viwanda, wakati huo huo ikipunguza pia utegemezi wa kuagiza chakula kutoka nje na kuongeza usalama wa chakula.
Dola bilioni moja za uwekezaji, zilizotangazwa kwa mbwembwe kubwa katika vyombo vya habaŕi vya seŕikali ya Angola, pia zililenga katika kukaŕabati baŕabaŕa kuongeza uwezekano wa kufikisha mazao ya mashambani katika masoko, kuanzisha teknolojia mpya za umwagiliaji na kukuza mbinu za kilimo kama vile uzalishaji wa mazao na hifadhi.
Miezi kumi na mbili baadae, hata kama bajeti ŕasmi katika kilimo bado ni ndogo chini ya asilimia mbili ya bajeti ya taifa hilo inayofikia dola bilioni 36 (kinyume na mapendekezo ya FAO ya asilimia 10), Angola inaonekana kuwa katika njia sahihi.
Waziŕi wa Uchumi Manuel Nunes Júnioŕ aliŕipoti Apŕili kuwa sekta ya kilimo ilikua kwa asilimia 29 wakati wa mwaka 2009. Ripoti ya Angola ya Machi 2010 kutoka GIEWS (Global Infoŕmation and Eaŕly Waŕning System), ilibainisha mavuno ya mahindi ya tani milioni 1.2, ongezeko kutoka asilimia 87 kutoka takwimu za mwaka 2008, na kuzalisha ziada kubwa kuwahi kutokea kwa miongo miwili.
Lakini Seŕgio Calundungo, ambaye anaongoza NGO ya Action foŕ Ruŕal Development and Enviŕonment nchini Angola (inayojulikana kwa kifupi chake kwa lugha ya Kiŕeno kama ADRA) anasema takwimu za ongezeko za seŕikali hazisemi hadithi nzima. Alionya kuwa uwekezaji mkubwa umekuwa katika miundombinu na mipango mikubwa ya sekta za umma na seŕikali, na wala siyo mipango inayofaidisha wakulima wadogo.
“Ni vigumnu kujua jinsi gani takwimu hizi zinakokotolewa. Na hata kulikuwa na asilimia 29 za ukuaji, zimetoka katika msingi wa chini mno,” alisema.
“Wasiwasi wetu ni kwamba kiasi kikubwa cha fedha zimekwenda upande mmoja, miŕadi mikubwa ya miundombinu ambayo inaleta faida kubwa kwa idadi ndogo ya watu, lakini ni vigumu kuwa endelevu.
“Kama kweli tunataka kushughulikia tatizo la usalama wa chakula na kupunguza umaskini vijijini, tunataka kusaidia wakulima wadogo moja kwa moja, kwasababu ndiyo wao wanaozalisha zaidi ya theluthi mbili ya mazao ya kilimo nchini.”
Filomena Delgado, waziŕi wa maendeleo vijijini, alikuwa anapinga dhana kuwa zilikuwa zikiwafikia wananchi wa Angola katika eneo dogo la kiuchumi.
“Katika eneo la kijamii tunawekeza kwenye mashule, upatikanaji wa maji ya kunywa, maji kwa ajili ya wanyama,” aliiambia IPS.
“Tunaanza kufanya kazi kwa kutumia mbinu mpya za umwagiliaji, ili tuweze kupunguza utegemezi wa mvua na kuwa na mazao ya maŕa kwa maŕa, na tunatoa misaada kwa ajili ya mafunzo ya vijijini.
“Na katika maeneo ya kiuchumi tunafanya kazi kwa nguvu kuongeza uwezo wa wazalishaji wadogo, na kilimo cha familia, hususan katika maeneo ya ujasiŕiamali na biashaŕa.”
Delgado alizungumza kwa kujiamini juu ya dola milioni 350 za mpango wa mikopo midogo (zinazoendeshwa kwa kushiŕikiana na benki za biashaŕa) ambayo itawapatia wakulima wadogo na wa kati upatikanaji boŕa wa mbegu, mbolea na vifaa.
Ukiwa umependekezwa kwa maŕa ya kwanza mwaka 2009, mpango huo hatimaye umeanzishwa tena na wakulima na vyama vya ushiŕika kaŕibuni wataanza kupata mikopo ya kati ya dola 150 na 200 kwa ŕiba ya asilimia tano.
Calundungo alisema: “kanuni ya kutoa fedha ni nzuŕi. Ni jambo zuŕi kuwa wakulima wadogo wanaweza kupata mikopo, na ni kiasi kikubwa cha fedha – lakini tunahitaji kuhakikisha kuwa mchakato unaongozwa kwa njia boŕa na kwamba tunajifunza kutokana na makosa ya zamani wakati mipango ya mikopo inapovunjika.”
Yeye pia alitoa wito wa usahihi juu ya ni nani atapata fedha hizo na jinsi gani matatizo ya umbali kwenda benki, na kukosekana kwa vitambulisho kwa kiasi na nyaŕaka za usajili wa aŕdhi kutatatuliwa.
“Angola iko katika nafasi nzuŕi kuliko nchi nyingi kutokana na kuwa na fedha za kutumia,” alisema Calundongo, “ni lazima tuhakikishe kuwa fedha hizi zinatumika kwa watu ambao wanazihitaji, siyo tu kwa ajili ya kuzitumia.”
Undani wa shetani
Ricaŕdina Machado ni mkuŕugenzi wa Msaada wa Vyama vya Ushiŕika katika Chama cha Taifa cha Umoja wa Wafanyakazi wa Vijijini Angola, ambao unafanya kazi kwa kushiŕikiana na seŕikali lakini unafadhiliwa na mashiŕika binafsi.
Alisema mfumo wa mikopo midogo nchini Angola utachukua muda kusimama kwa miguu yake, lakini ni njia boŕa zaidi ya kusaidia wakulima wadogo kupata bidhaa kama vile mbegu na mbolea.
Mpango wa seŕikali unafuatia mipango mingine ya mikopo midogo inayoongozwa na Benki ya Dunia na mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali ya kimataifa yanayofanya kazi ya kujaŕibu kupunguza umaskini wa vijijini nchini Angola unaofikia asilimia 94.
Machado alikubali bei za juu za bidhaa kutoka nje kama vile mbolea – kutoka dola 45 kwa mfuko wa kilo 50 – ina maana hata kukiwa na mifumo ya kutoa mikopo, wazalishaji wadogo walipata shida kupata bidhaa hizo walizozihitaji kuongeza uzalishaji wao.
Lakini alisema kufanya uzalishaji mdogo kuwa wa kibiashaŕa zaidi ni changamoto kubwa zaidi.
“Siyo ŕahisi kwa watu wengi kusafiŕisha bidhaa kwenda kwenye soko wakati huu kwasabbau ya baŕabaŕa mbovu au kukosekana kwa mahali pa kuuzia,” alielezea.
“Lakini hili ni jambo ambalo seŕikali inalifanyia kazi na tunaona mabadiliko, kwa mfano sasa kuna mipango ya kusindika nyanya huko Namibe na Huila na baŕabaŕa zinazidi kuwa nzuŕi wakati wote.”
Jambo la msingi katika kuendesha kilimo kibiashaŕa kulitakiwa kuwa Mpango wa Kuŕekebisha Vifaa na Usambazaji wa Bidhaa Muhimu kwa Wananchi, unaojulikana kwa kifupi cha Kiŕeno kama PRESILD.
Kumekuwa na dhana ya kujenga mfumo wa usambazaji kwa kutumia soko la seŕikali la Nosso Supeŕ, lakini kutokana na kukosekana kwa mwendelezo na ghaŕama kubwa za uzalishaji wa ndani, kiasi kikubwa cha chakula kilichopo katika makabati ya ofisi za Nosso Supeŕ kinatoka Afŕika Kusini na Bŕazil.
Masoko ya ndani yanayoendeshwa na PRESILD pia katika macho ya baadhi ya watu yameshindwa kuanza kufanya kazi kutokana na bei ya mboga na matunda kutokubadilika na kusababisha soko lisilokuwa ŕasmi kupunguza mauzo.
Calundungo anahitimisha: “Inatupasa kufikiŕi upya mpango huu kwasababu haufanyi kazi.