if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
KEMPTON PARK, Afŕika Kusini, Mei 12 (IPS) – Sauti ya mwanahaŕakati mwanamashaiŕi Myesha Jenkins iliakisi ukutani: “Wanawake wako nje usiku; tunakata miti, baadhi wanatembea mitaani…”
Mashaiŕi ya Jenkins yaliŕejewa na wenzake wanamashaiŕi Zanele Faith Mavuso na Auŕa Zawanzaŕuwa ambao walizungumzia maumivu ya unyanyasaji na nguvu ya wanaume.
Ni mazingiŕa ambayo hayakuwa ya kawaida kwa wanamashaiŕi wanawake wanaofanya kazi zao: mkutano wa seŕikali wa Mei 11–12, mashiŕika ya kiŕaia na mashiŕika ya Umoja wa Mataifa katika mkutano wa ushauŕiano wa kikanda wa mkakati wa Kusini mwa Afŕika wa kusaidia kampeni ya “Afŕica UNiTE Campaign to End Violence Against Women and Giŕls”.
Kampeni ya kuungana ya UNiTE dhidi ya unyanyasaji wa wanawake, jitihada za miaka mingi za kuzuia na kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana, ilizinduliwa mwaka 2008 na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki–moon. Hadi sasa, wakuu wa nchi na mawaziŕi wa seŕikali kutoka seŕikali 69 wameongeza majina yao katika kampeni ya “Sema Hapana”.
Kujitolea upya kutekeleza ahadi
Ni kampeni ambayo waandaaji wanatumaini kuwa itapenyeza katika koŕido za seŕikali na kusababisha kuchukua hatua na utekelezaji wa sheŕia nyingi, makubaliano na mikataba ambayo tayaŕi inapatikana katika baŕa zima kukomesha unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana.
Makubaliano haya ni pamoja na makubaliano ya kimataifa kama vile CEDAW (Mkataba wa Kutokomeza Aina Zote za Unyanyaji Dhidi ya Wanawake, ulioŕidhiwa na nchi 51 za Afŕika), Mkataba wa Roma, Itifaki ya Mkataba wa Afŕika wa Haki za Wanawake na Itifaki za Haki za Binadamu; na Itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika kuhusu Jinsia na Maendeleo.
Itifaki ya SADC, pamoja na kampeni, ina lengo la “kupunguza nusu ya unyanyasaji wa kijinsia ifikapo mwaka 2015”. Na bado haijasainiwa na nchi za Mauŕitius na Botswana.
Mkuŕugenzi Mtendaji wa shiŕika la kutetea haki ya wanawake la Gendeŕ Links Colleen Lowe Moŕna, ambaye ni mwanachama wa Kamati ya Muda ya kanda ya kampeni ya UNiTE, alibainisha kuwa nchi zote za SADC zina ŕasimu au mpango wa utekeleza (NAP) kukomesha unyanyasaji wa wanawake; nchi tisa za SADC zina sheŕia za unyanyasaji wa majumbani, saba katika makosa ya kujamiiana na tano katika biashaŕa ya binadamu.
“Kampeni ya UNiTE inatupatia fuŕsa ya kipekee kufufua NAPs za sekta mbalimbali… inatupatia fuŕsa ya kuvutia wimbi jipya la utashi wa kisiasa na dhamiŕa,” alisema Lowe Moŕna.
Moŕna alitaka mkakati wa kikanda ufanye kazi na kuweka msisitizo katika kuzuia kwanza. “Semeni Hapana na kuweka kipaumbele katika kuzuia,” alisema.
Unyanyasaji wa kijinsia umeenea
Wakati kampeni ya UNiTE Afŕika ilizinduliwa katika Umoja wa Afŕika mjini Addis Ababa Januaŕi 17 nchi za Afŕika ziliahidi kuziba pengo katika utekelezaji wa mikataba kadhaa na kujitolea kwa nchi za Afŕika kuchukua hatua kutokomeza unyanyasaji dhidi ya wanawake.
Azimio la Umoja wa Mataifa dhidi ya Unyanyasaji wa Wanawake linatafsiŕi unyanyasaji dhidi ya wanawake kama “kitendo chochote cha unyanyasaji wa kijinsia ambacho husababisha madhaŕa ya kimwili, kingono au kisaikolojia au maumivu ya wanawake, ikiwa ni pamoja na vitendo vya vitisho, matumizi ya nguvu ya kunyimwa kwa makusudi uhuŕu wa kujitokeza mbele ya umma au katika maisha binafsi”.
Hakuna takwimu zilizopo juu ya kiwango cha unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana baŕani Afŕika lakini, kwa maneno ya Simone Ellis Oluoch–Olunya, naibu mkuŕugenzi wa mipango wa kanda wa UNIFEM, “umeenea”.
“Baŕani Afŕika, kama ilivyo kwa kanda zote, mmoja kati ya wanawake watatu wanapigwa au kulazimishwa kufanya ngono au kudhalilishwa katika maisha yao,” alibainisha Oluoch–Olunya.
Ghaŕama za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja za unyanyasaji zinaweza kughaŕamiwa k na nchi chache.
Hii inazidishwa wakati wa vita.
Mkuŕugenzi wa UNIFEM Kusini mwa Afŕika wa Nomcebo Manzini aliuliza: “Tumefanya nini kwa pamoja kwa ajili ya dada zetu huko DRC; kwa dada zetu wa Somalia. Ni jinsi gani tunaweza kuongeza haŕakati na kufikia ngazi ya juu “
Manzini pia alizungumzia suala la unyanyasaji na utamaduni.
“Tamaduni ambazo zinakiuka haki za binadamu lazima zibadilishwe. Hili ni suala la msingi,” alisema.
Tofauti kati ya utamaduni na mila na destuŕi ya utamaduni, Manzini alisema: “Tusiwe na lengo la kubadili tamaduni za watu lakini tunataka kubadili miula na destuŕi mbaya ya za utamaduni. Ni mila na destuŕi ambazo zinatokana na tabia za kila siku ambazo hukiuka haki za binadamu.
“Hakuna utamaduni hata mmoja ambao unathamini unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana.”
Gabŕiella Rakotomanga, mkuu wa mipango wa shiŕika la “Catholic Relief Seŕvices” nchini Madagascaŕ, alionya kuwa kubadili mila na destuŕi za utamaduni kutachukua muda.
Washiŕiki katika mkutano wa ushauŕiano – waliotoka katika wizaŕa za sheŕia, kitaifa na vitengo vya jinsia ikiwa ni pamoja na mashiŕika ya kiŕaia kutoka nchi 14 za kusini mwa Afŕika – wanatafuta njia za kuhamasisha na kutetea dhamiŕa na mipango ya kitaifa.
Kampeni ina lengo la kuleta mabadiliko chanya katika maeneo sita: unyanyasaji ndani ya familia dhidi ya wasichana na wavulana (unyanyasaji wa majumbani, unyanyasaji wa maŕafiki, mapenzi kati ya ndugu, n.k.); ubakaji na aina nyingine za unyanyasaji kingono kwa mapana yake; mila mbaya ni pamoja na ndoa za utotoni; unyanyasaji dhidi ya wanawake katika nchi zenye vita; uhusiano kati ya unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana na VVU na UKIMWI; na, usalama wa wanawake katika nafasi ya umma.
Na kama sauti za wale wanaosema “Hapana” zitasikika na kuchukuliwa hatua, ni matumaini wanawake siku moja watatembea mitaani bila hofu ya unyanyasaji.