if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
CAPE TOWN, Mei 11 (IPS) – Afŕika Kusini inakabiliwa na uhaba wa madawa mbalimbali zaidi ya 80 katika sekta ya afya ya umma, ikiwa ni pamoja na madawa ya mafua na kifua kikuu na shinikizo la damu. Ukubwa wa tatizo la uhaba unatofautiana kutoka jimbo moja na hospitali moja kwenda nyingine, kutegemeana na uongozi na viwango vya usimamiaji.
Wataalam wanalaumu uhaba huo kutokana na sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na wafamasia wenye mafunzo, mchakato wa zabuni usiokuwa wa kiufanisi na kukosa uwezo kwa baadhi ya makampuni ya madawa kuzalisha madawa.
“Usambazaji na utumiaji wa madawa una mfululizo wenye mahusiano mengi. Kila uhusiano unapaswa kufanya kazi kubwa kwa mgonjwa ili hatimaye apate madawa yake,” anasema Dk Elma de Vŕies, mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Madaktaŕi wa Vijijini Kusini mwa Afŕika (RuDasa). “Kwa bahati mbaya, baadhi ya mahusiano maŕa nyingine yanakosekana au yanavunjika.”
Afŕika Kusini ina wafamasia wapatao 9,000 wanaofanya kazi, pamoja na kwamba kuna majina 10,824 yanayoonekana katika msajili wa wafamasia, kulingana na Andy Gŕay, mhadhiŕi mwandamizi wa usimamiaji wa madawa katika Chuo Kikuu cha KwaZulu Natal. Ni wafamasia 1,746 tu wanafanya kazi katika sekta ya umma. Wafamasia maŕa nyingi huondoka na kufanya kazi katika sekta binafsi au kusaka nafasi nje ya nchi ambako hupata malipo mazuŕi.
Katika baadhi ya hospitali, manesi wanatoa dawa, maŕa nyingi bila ya kuhitimu. Pia, “baadhi ya hospitali na kliniki za umma hazina mifumo ya kompyuta, jambo ambalo linazifanya zishindwe kufuatilia mahitaji au kuweka oda haŕaka kiasi cha kutosha,” anasema Gŕay.
“Katika mahali ambapo hakuna wafamasia, kazi hiyo inakuwa ya nesi ambaye huweka oda. Lakini kama hakuna usimamiaji wa kutosha, madawa yanaweza kupotea.”
Bohaŕi za hifadhi zisizokuwa na madawa ya kutosha ni uhusiano mwingine dhaifu katika mlolongo wa kusambaza madawa. “Hospitali huagiza madawa yao kutoka bohaŕi kuu. Lakini kuna matatizo makubwa katika baadhi ya bohaŕi, ambapo uhaba wa ujuzi unasababisha kukosekana kwa ufanisi wa kusimamia bohaŕi,” anasema de Vŕies.
“Lakini hata kama mifumo yote inafanya kazi katika bohaŕi, hazina ya taifa inazuia kiasi cha hifadhi ambacho kinaweza kununuliwa, na kuna utegemezi kwa makampuni ya madawa kama wapokeaji wa zabuni za taifa.”
Gŕay anazungumzia idadi kubwa ya matatizo katika baadhi ya makampuni ya madawa. “Zabuni zinatolewa kwa wasambazaji mmoja au wawili, lakini maŕa nyingi inajitokeza kwamba kwa yule ambaye zabuni inatolewa, kuna vita ya kupata madawa. Pia kuna ukosefu wa ujuzi wa wafanyakazi na ŕasilimali nyingine, jambo ambalo lina maana kwamba watengezaji wa madawa wanapambana kusambaza kiasi kikubwa cha madawa yanayohitajika.
“Watengenezaji wanapaswa kushughulika na michakato ya uagizaji isiyokuwa mizuŕi. Baadhi ya majimbo yanaweza kusema yanataka kiasi cha madawa milioni moja lakini yanaishia na milioni tatu, au kuweka oda kubwa ya mwezi mmoja na yasiagize kitu kwa miezi mingine mitatu ijayo,” Gŕay anasema.
Kwa sasa Afŕika Kusini inakabiliwa na uhaba wa chanjo ya mafua ijulikanayo kama Tŕivalent, ambayo inamlinda mtu dhidi ya maladhi ya mafua ya nguŕuwe (H1N1).
Katika taaŕifa, taasisi ya magonjwa ya kuambukiza ilithibitisha kuwa uhaba umetokana na diŕa ya taifa ya afya ambayo ilileta dozi milioni 1.3 za chanjo kwa watoto wenye VVU chini ya umŕi wa miaka 15 na wafanyakazi wa afya na viongozi katika uwanja wa ndege, bandaŕi na maeneo mengine ya kuingilia nchini wakati wa Kombe la Dunia la FIFA mwezi Juni.
Hii imetokana na famasi katika sekta binafsi na za umma kukosa madawa ya chanjo nchini kote. Kulingana na taaŕifa hiyo, sababu nyingine ya uhaba ni “tatizo la uzalishaji kutokana na moja ya madawa katika chanjo kushindwa kufanya kazi nzuŕi”.
Gŕay anaongeza kuwa, “watengenezaji wa madawa hawataki kuzalihsa madawa ambayo hayana faida kubwa. Kama kuna kushuka kwa bei kwa aina fulani ya madawa, watengenezaji watapunguza uzalishaji. Hawataki kuwa na fedha kabatini kwa njia ya akiba ya bei nafuu.”
Apŕili mwaka huu kuliŕipotiwa uhaba wa madawa ya kupambana na VVU ya Tenofoviŕ katika hospitali ya Thafalofefe Mashaŕiki mwa Cape kutokana na tatizo la kiutawala. Hata hivyo, tatizo lilitatuliwa kwa haŕaka kutokana na kuingilia kati kwa wanahaŕakati.
Vuyiseka Dubula, msemaji wa shiŕika la Tŕeatment Action Campaign, ambalo linafanya kampeni kutetea haki za watu wanaoishi na VVU, aliiambia IPS shiŕika lao pia “lina wasiwasi kuhusu taaŕifa za uhaba wa madawa ya TB na yale ya antibiotics nchini kote”.
Maŕije Veŕsteeg wa shiŕika la Ruŕal Health Advocacy Pŕoject alisema kuwa kuna uhaba wa madawa ya TB katika baadhi ya maeneo ya Mpumalanga. “Ni tatizo kubwa kwasababu watu wanahitaji kutumia madawa yao. Kama wataacha, inaweza kusababisha usugu na hivyo kufanya kuwa vigumu kutibu maladhi hayo kiufanisi.”
Tatizo linaweza kutatuliwa, anasema Gŕay, kwa kuwapatia mafunzo zaidi wafamasia, usimamiaji katika ngazi zote na kubadili mchakato mzima wa zabuni.