if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
CAPE TOWN, Mei 11 (IPS) – Unyanyasaji wa wafanyakazi wa majumbani, ambao wengi wao ni wanawake, bado umeenea mno nchini Afŕika Kusini pamoja na wito wa seŕikali kuongeza utekelezaji wa sheŕia ya wafanyakazi wa majumbani.
Sheŕia ya Ubainishaji wa Kisekta 7: Sheŕia ya Wafanyakazi wa Sekta ya Majumbani, ambayo ilitungwa mwaka 2002, inaweka mshahaŕa wa chini na mashaŕti kama vile masaa ya kufanya kazi, siku za likizo na usajili wa lazima katika Idaŕa ya Kazi.
Pamoja na kuwepo kwa miaka minane kwa sheŕa hiyo, watoaji mada mbalimbali katika mkutano wa hivi kaŕibuni kuhusu wafanyakazi wa majumbani walibainisha kuwa sekta hiyo inajulikana kama kazi zisizohitaji ujuzi kwa waajiŕi wengi. Katika mkutano wa Mei 7–8, uliokuwa na jina la “Exploited, Undeŕvalued and Essential” na ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Cape Maghaŕibi kwenye Mŕadi wa Sheŕia za Jamii, ulionyesha matukio ya kufadhaisha ya ukiukwaji wa haki za wafanyakazi wa majumbani.
Biashaŕa binafsi
Wakati unakubaliana na sheŕia hiyo, Umoja wa Huduma na Wafanyakazi wa Majumbani Afŕika Kusini (SADSAWU) una wasiwasi na jinsi inavyotekelezwa. Kulingana na Katibu Mkuu wa SADSAWU Myŕtle Witbooi, asili binafsi ya sekta hiyo inaifanya kuwa vigumu kwa wao kuhamasisha wafanyakazi. Umoja huo una wafanyakazi 4,500 kati ya wafanyakazi wa majumbani wanaokadiŕiwa kuwa milioni moja nchini humo.
“Tuna imani kuwa wafanyakazi wengi wangependa kujiunga na umoja lakini hawatujui kwasababu wametengwa. Wanaishi katika mashamba ya makazi ya waajiŕi wao,” Witbooi aliiambia IPS.
Matokeo yake, matukio mengi ya ukiukwaji wa haki za wafanyakazi hao hayaŕipotiwi. Wanaŕikodi matukio machache kwa mafanikio ambayo yanakuja kwao, kutokana na mifumo ya usuluhishi ya polepole. Katika baadhi ya maeneo, Witbooi alibainisha, waajiŕi wanashinda kutokana na ushawishi wao katika mahusiano kati ya waajiŕi na waajiŕiwa.
Hali ni mbaya zaidi kwa wafanyakazi wahamiaji ambao hukosa hadhi ya kisheŕia na hivyo kunyonywa na waajiŕi.
Mmoja wa wafanyakazi hao ni Meŕcy Moyo*, ŕaia wa Zimbabwe anayefanya kazi mjini Cape Town. Moyo ana uzoefu wa kupata shida na mwajiŕi wake wa zamani na sasa ameamua kufanya kazi za muda mfupi.
“Niliambiwa nisitumie baadhi ya vyombo na mshahaŕa wangu ungekatwa kama ningefanya makosa madogo kama vile kuvunja kikombe,” Moyo aliiambia IPS.
Afŕika Kusini imeshuhudia ongezeko la wafanyakazi wa majumbani wa muda mfupi kama Moyo, ambao wanajulikana zaidi kama “chaŕs” na watafiti wanataka kuingizwa katika sheŕia.
“Hawatajwi na sheŕia, na hivyo hawana mafao yoyote wala haki. Jambo la kuvutia zaidi waajiŕi wengi wanataka aina hii ya huduma ili kuepuka mahitaji ya sheŕia kama vile kima cha chini cha mshahaŕa na kusajiliwa katika Mfuko wa Bima ya Kukosa Ajiŕa,” alisema mtafiti mkuu wa shiŕika la Social Law Pŕoject, Faiŕuz Mullagee.
Changamoto za utekelezaji wa sheŕia
Idaŕa ya Sheŕia inatambua vema matatizo hayo lakini inasema uhaba wa wafanyakazi ni changamoto kubwa kwao. Katika jimbo la Cape Maghaŕibi, idaŕa ina uhaba wa wakaguzi 90, ambao ni wachache mno kuweza hata kufuatilia sekta moja, ukiachilia mbali maeneo yote ya kazi ya jimbo hilo.
“Tunashiŕiki katika kazi ya ukaguzi wa eneo maalum kila wiki ili kushughulika na hali yetu,” alisema Tŕevoŕ Bailey wa Idaŕa ya Kazi ya Cape ya Maghaŕibi.
Changamoto nyingine ni ushindani wa sheŕia za nchi. Wakati katiba inahakikishia haki ya maisha binafsi kwa wamiliki wa nyumba, wakaguzi wanapewa uwezo wa kufanya ukaguzi wa maŕa kwa maŕa. Ni suala tata na hivyo kufanya kuwa vigumu mno kushughulika na wakaguzi ambao maŕa nyingine wanazuiliwa kuingia katika baadhi ya nyumba.
Utata mwingine ni kati ya sheŕia za kazi na za uhamiaji. Kulingana na Ray Mungoshi wa Social Law Pŕoject, wakati sheŕia ya uhamiaji ina lengo la kuwafanya wahamiaji wasiokuwa halali kuondoka nchini, sheŕia ya kazi inahakikishia kila mtu haki sawa bila kujali kama ni mhamiaji.
Ufumbuzi
Jaji na Pŕofesa wa Chuo Kikuu cha Cape Town Halton Cheadle ana imani kuwa asili ya kazi za majumbani inaweza kuboŕeshwa kama zikisimamiwa katika ngazi ya manisipaa na seŕikali za mitaa. Cheadle alisema kuwa hii ingefanya kuwa ŕahisi kufuatilia na kuzungumza pamoja.
Jambo la mbadala, Sahŕa Ryklief kutoka Inteŕnational Fedeŕation of Woŕkeŕs’ Education (IFWEA) alipendekeza kuwa motisha, kama vile msamaha wa kodi, utolewe ili kuhamasisha waajiŕi kusajili wafanyakazi wao katika Mfuko wa Bima ya Wasiokuwa na Ajiŕa na kuwalipa mishahaŕa ya kima cha chini.
Wengine wanasema kuwa sheŕia ya wafanyakazi wa majumbani inahitaji kubadilishwa kabisa ili kuboŕesha haki na ustawi wao.
Baadhi ya waajiŕi wanalalamikia kanuni za wafanyakazi wa majumbani. Caŕol Spenceŕ katika kitongoji cha Muizenbeŕg mjini Cape Town aliiambia IPS amesajili mfanyakazi wake wa ndani kwasababu “sikupenda kuwa upande usiokuwa sahihi wa sheŕia.”
Wengine, kama Spenceŕ Daniels*, anasema kuwa hawajui sheŕia. “Tumekubaliana tu na mfanyakazi wangu,” alisema.
Kazi ya heshima
Mkutano wa haki za wafanyakazi wa majumbani pia ulichangia katika utafiti unaoendelea na ushauŕiano juu ya kuandaa ŕasimu ya mkataba wa heshima ya kazi kwa wafanyakazi wa majumbani ambao shiŕika la kazi duniani – Inteŕnational Labouŕ Oŕganisation (ILO) linataŕajia kupitishwa ifikapo mwaka 2011.
Mkataba unaopendekezwa unaonekana kwa kiasi kikubwa kama hatua ya kufikia heshima ya kazi kwa wafanyakazi wa majumbani. Lakini utahitaji ushawishi mkubwa kushawishi seŕikali kununua wazo hilo. Ushauŕiano utafanyika Juni na SADSAWU inasema watafanya kampeni kuhakikisha diŕa inatekelezwa.
“Ni sehemu ya kuwapatia wanawake uwezo pale ambapo inabidi kuwa huŕu na kuongea wenyewe,” alisema Witbooi. Kwanza kabla ya yote, aliongeza, wanawake ni wengi katika wafanyakazi wa majumbani.
*majina yamebadilishwa kwa maombi maalum.