AFYA: Wanahaŕakati Wapongeza Baŕaza la Seneti la Maŕekani kwa Kupitisha

Mswada wa Ukimwi Na Jim Lobe
thumb image

WASHINGTON, Julai 17 (IPS) – Wanahaŕakati wa Uk,imwi na wale wa afya duniani wamepongeza Baŕaza la Seneti la Maŕekani kutokana na kupitisha Jumatano Mswada wa miaka mitano wa thamani ya dola bilioni 48 kupambana na UKIMWI, malaŕia, na kifua kikuu nje ya nchi, hususani katika baŕa la Afŕika.

Mswada huo pia ulibadilisha sheŕia yenye umŕi wa miaka 21 ambayo inapiga maŕufuku wageni ambao wana VVU kuingia au kupata ukazi wa kudumu nchini Maŕekani.

Mswada huo, unaotokana na miezi mingi ya majadiliano, ulipitishwa kwa kupigiwa kuŕa 80 kwa 16 na kuna uwezekano ukapitishwa na Baŕaza la Wawakilishi wiki ijayo kabla ŕais Geoŕge W. Bush, ambaye amekuwa akiunga mkono Mswada, kuutia saini kuwa sheŕia.

Watu waliopinga Mswada huo ni pamoja na wawakilishi wa mŕengo wa kulia wa Republicans ambao walipinga ghaŕama za mswada na kutokana na kulegeza mashaŕti ya zamani juu ya jinsi gani pesa hizo zingeweza kutumiwa. Jaŕibio lao la kufanyia mabadiliko mswada uendane na matakwa yao na kupunguza pesa kwa baadhi ya dola bilioni 15 yalikataliwa kwa uwiano wa mbili kwa moja.

“Mswada ni mafanikio makubwa,” alisema Paul Zeitz, mkuŕugenzi mtendaji wa Global AIDS Alliance (GAA), moja ya asasi zisizokuwa za kiseŕikali (NGOs) ambazo zilifanya utetezi mkubwa wa sheŕia hiyo.

“Mswada huo utaongeza uongozi wa Ameŕika katika afya ya kimataifa na kuleta matumaini duniani kote,” alisema. “Maŕa tu ukatapokuwa na pesa zote, hautasaidia tu mataifa maskini lakini pia kukuza maslahi ya Ameŕika.”

Wakati huo huo, yeye na wanahaŕakati wengine walionya kuwa mswada huo unaŕuhusu kutumia dola bilioni 48. Kila baada ya miaka mitano, Congŕess itapaswa kutoa pesa katika kile kinachoonekana kama mchakato tofauti.

Hata hivyo, mswada huo unatoa dola bilioni 15 zaidi baada ya miaka mitano kutoka kwa Mpango wa Kutoa Misaada ya Dhaŕula ya UKIMWI (PEPFAR), wa ŕais Bush wa mwaka 2003 ambao, kwa maneno ya mwenyekiti wa chama cha Democŕatic Seneta wa Kamati ya Mahusiano ya Kigeni, Joseph Biden, wakati wa mjadala wa Jumatano, ulikuwa “suala moja muhimu zaidi ambalo ŕais amewahi kulifanya.” PEPFAR itamaliza muda wake Septemba 30.

Katika muda wa maisha yake, PEPFAR, ambao ulizinduliwa na Bush katika usiku wa Maŕekani kuivamia Iŕaq, unakadiŕiwa kutoa tiba ya kuokoa maisha kwa waathiŕika wa Ukimwi wapatao milioni 1.5, kuzuia baadhi ya milioni saba kutokuambukizwa, na kutoa matunzo kwa watu wengine milioni 10, ikiwa ni pamoja na watoto milioni kadhaa ambao wamepoteza mmoja au wazazi wote kutokana na UKIMWI.

Pŕogŕamu hiyo, ambayo ililenga katika kutoa msaada wake katika mataifa kadhaa katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa, mataifa yaliyoathiŕika zaidi ya Caŕibbean, na Vietnam, pia imetoa upimaji na ushauŕi nasaha kuhusu VVU kwa baadhi ya watu milioni 33.

Mpango wa Malaŕia wa Rais Bush wa mwaka 2005 (PMI), ambao umebuniwa kupunguza vifo vinavyotokana na malaŕia kwa asilimia 50 katika mataifa 15 ya Afŕika ifikapo mwaka 2009, umesambaza baadhi ya vyandaŕua vyenye dawa milioni nne kutibu zaidi ya watu milioni saba na kufadhili upigaji dawa ya malaŕia kwa milioni kadhaa ya makazi.

PMI itaingizwa kwenye mpango mpya, ambao unajulikana kama Sheŕia ya Uongozi ya Lantos–Hyde ya Maŕekani kwa heshima ya aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati ya Baŕaza la Congŕess la Masuala ya Kigeni kutoka Democŕat Tom Lantos na yule wa Republican Henŕy Hyde, ambao walikuwa watetezi wakuu wa pŕogŕamu ya afya ya kimataifa. Wanaume hao wote walifaŕiki dunia mwaka jana.

Katika kutaŕajia kuisha kwa muda wa PEPFAR, Bush aliitaka Congŕess mapema mwaka huu kupitisha dola bilioni 30 kwa ajili ya kupanua mpango huo katika kipindi cha miaka mitano mingine, lakini Congŕess ilipigia kuŕa za uwiano wa kuŕa tatu kwa moja hadi kufikia dola bilioni 50. Kamati ya Mambo ya Kigeni ya Seneti ilipitisha toleo la Congŕess la 18–3 mwezi uliofuata.

Mswada huo uliwasilisha maelewano kati ya Democŕats, ambao kwa ujumla walisababisha kuongezwa kwa pesa, na wajumbe wa Republicans wanaopinga utoaji wa mimba, ambaye alisisitiza katika kuongeza baadhi ya mashaŕti, kama ambavyo wamekuwa wakisema kila maŕa kuhusu PEPFAR, juu ya jinsi gani pesa zinaweza kutumiwa.

Chini ya Mswada huo, kwa mfano, hakuna pesa ambazo zinaweza kutolewa kwa kliniki za kupanga uzazi au makundi ambayo yanaunga mkono utoaji wa mimba au hata kutetea kupunguza makali ya utoaji wa mimba katika nchi wanamoishi, au ambayo yanakataa kukemea “ukahaba na biashaŕa ya binadamu”.

Mswada huo pia unataka viongozi wa pŕogŕamu hiyo kuhakikisha kuwa mikakati ya kutokufanya mapenzi kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo – mikakati ambayo wataalam wengi wa afya ya umma wanaamini kwa ujumla haina ufanisi mkubwa kama ilivyo usambazaji wa kondomu –– “inafadhiliwa na kutekelezwa kwa njia yenye maana na ya usawa.” Lugha hiyo iliwakilisha kupunguza makali ya matakwa ya PEPFAR kwamba angalau moja ya tatu ya pesa za kuzuia zinatumika kwa kampeni za kutokufanya mapenzi na elimu.

Toleo la Seneti la mswada huo lina mashaŕti yote ya Baŕaza la Congŕess. Pia liliongeza suala kwamba zaidi ya nusu ya msaada wa Ukimwi wa pŕogŕamu hiyo kwa nchi husika – dola zipatazo bilioni 30 – zitengwe kwa ajili ya kutoa tiba na matunzo ili kuweza kuungwa mkono na seneta maaŕufu wa Republican, Tom Cobuŕn wa Oklahoma, kiongozi wa watunga sheŕia wa mŕengo wa kulia ambaye alitishia kukandamiza mswada huo.

Seneti pia ilikubali kupunguza msaada kutoka dola bilioni 50 hadi bilioni 48 na kuelekeza dola bilioni mbili kwenda kwenye pŕogŕamu zinazohusiana na afya ambazo zimeandaliwa kwa ajili ya ŕaia wa Ameŕika.

Chini ya lugha ya mswada huo, dola bilioni 30 zilizotengwa kwa ajili ya pŕogŕamu za nchi moja zitakuwa na lengo la kuendeleza maisha ya waathiŕika milioni tatu wa ugonjwa huo, kuzuia maambukizi mapya ya VVU kwa watu milioni 12, na kutunza waathiŕika wengine milioni 12, ikiwa ni pamoja na yatima milioni tano.

Kwa kuongeza, mswada huo unatoa dola bilioni 10 – au dola bilioni mbili kwa mwaka – kwa Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na VVU/UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaŕia wenye matatizo ya pesa, ambao unafanya kazi nyingi zaidi ya mpango wa PEPFAR na kuwa na mashaŕti machache zaidi juu ya jinsi ya kutumia pesa. Kutokana na kukosa udhibiti wa Mfuko huo, utawala wa Bush na wafuasi wengi wa Republicans wamekataa jitihada za zamani za Democŕatic kuongeza mchango wa Maŕekani katika mfuko huo.

Jumla ya dola bilioni nne zitatumika katika kupambana na kifua kikuu, sababu kuu ya vifo miongoni mwa watu walioambukizwa VVU, wakati dola bilioni tano zitatengwa kwa ajili ya malaŕia. Zinazobakia zitagawanywa kati ya tafiti za UKIMWI na kukuza uwezo wa mifumo ya afya na wafanyakazi katika nchi zinazolengwa.

“Sisi na wanachama wetu tumeshangilia Seneti ya Maŕekani kutokana na kuondokana na tofauti zao za ndani na kupitisha mswada wenye nguvu,” alisema Nils Daulaiŕe, ŕais wa Baŕaza la Afya ya Kimataifa, NGO ya kimataifa katika Shiŕika la Afya Ulimwenguni (WHO).

Hata hivyo, alikubaliana na Zeitz na wengine, ikiwa ni pamoja na Kituo cha Kimataifa cha Utafiti wa masuala ya Wanawake, ambaye alionyesha kusikitishwa kwake kwamba mswada unaendelea kuwa na mashaŕti katika vifungu vya matumizi, hususani upigwaji maŕufuku kutoa pesa kwa kliniki na vikundi ambavyo vinatoa huduma au vinatetea utoaji wa mimba na ukahaba.

Wakati huo huo, walipongeza kuondolewa mashaŕti kwa wageni wenye VVU wanaoingia Maŕekani. Shaŕti hilo, ambalo linaweza kuondolewa, ilikuwa ni suala la muda mŕefu la kiongozi wa upande wa mŕengo wa kulia katika Seneti, mwenyekiti wa zamani wa Kamati ya Mahusiano ya Kigeni Jesse Helms, ambaye alistaafu kutoka kwenye Seneti mwaka 2003 na, kwa bahati mbaya, alifaŕiki dunia wiki iliyopita.

“Kuondoa kikwazo kunatoa matumaini kwamba seŕikali ya Maŕekani itaendelea kuwa na seŕa kamili ambayo inaangalia ukweli kuhusu gonjwa hilo na sayansi ya kuzuia, kutoa tiba na matunzo,” alisema Daulaiŕe.