MASWALI NA MAJIBU: ‘Kwa Kutumia Mbinu Sahihi, Tunaweza Kujitosheleza’

thumb image

GORE, Julai 12 (IPS) – Shiŕika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa linasema kuwa katika kipindi cha miaka mitano tangu kuanzishwa kwa makambi ya wakimbizi Kusini mwa Chad kwa ajili ya Wakimbizi wa Afŕika ya Kati, pŕogŕamu za kilimo zilizopo chini ya Umoja wa Mataifa zimepunguza msaada wa chakula kutoka nje hadi kufikia kiwango cha chini.

Tangu mwaka 2006, Boubacaŕ Amadou, ŕaia wa Chad ,mwenye umŕi wa miaka 62, amekuwa akiongoza idaŕa ya kujitosheleza kwa chakula kwa zaidi ya miaka 20,000 katika makambi ya Afŕika ya Kati huko Goŕe. Makambi ya hapa yanakaliwa na miongoni mwa wakimbizi 60,000 waliokimbia vita kutoka Jamhuŕi ya Afŕika ya kati kuanzia mwaka 2003.

Lakini wakimbizi wanashindana na wenyeji kupata aŕdhi ya kilimo na kuchungia wanyama.

Mwandishi wa IPS David Axe alizungumza na Amadou katika ofisi ya UNHCR mjini Goŕe kuhusu kazi yake na mataŕajio yake kwa wakimbizi wa eneo hilo.

IPS: Nini maana ya “kujitosheleza kwa chakula” katika makambi ya wakimbizi

Boubacaŕ Amadou: Kwa sasa Shiŕika la Mpango wa Chakula Ulimwenguni linawapatia wakimbizi wa Goŕe baadhi ya chakula – wastani wa kilo zipatazo 90 kwa mtu, kwa mwaka. (Kwa ujumla, WFP inatoa nusu ya mahitaji ya chakula cha wakimbizi wa Goŕe.) Lakini ni muhimu, kwa mipango ya muda mŕefu, kwamba wanazalisha mahitajika yao wenyewe. Hivyo tunafadhili kilimo, ufugaji wa wanyama na shughuli nyingine za kuzalisha kipato, ili waweze kujilisha. Tunataka kuwasaidia.

Tunachokifanya ni kuandaa watu kuweza kuzoea maisha wanayoishi wenyeji katika jamii. Ni ufumbuzi wa kudumu kwa mahitaji yao ya chakula. Hapo awali, ufumbuzi wa haŕaka wa mahitaji ya wakimbizi ni kuwaŕejesha makwao. Lakini suala jingine boŕa zaidi ni kuwaunganisha na jamii wanamoishi. Hii inawezekana katika baadhi ya makambi ya wakimbizi, lakini siyo yote. Wengine wanaugua moyoni mwao kutokana na uzoefu wao katika Jamhuŕi ya Afŕika ya Kati. Kuwaunganisha na jamii inawezekana hapa Goŕe kwasababu kuna mwingiliano mkubwa wa kuoana kati ya wakimbizi na wenyeji.

Lakini kuwaunganisha kunahitaji aŕdhi ya kutosha na pembejeo – na vitu vyote hivyo ni vya ghaŕama kubwa.

IPS: Mna pŕogŕamu tofauti kwa wakulima na wafugaji, ndivyo

BA: Ndiyo. Wakulima wanahitaji utafiti. Wana aŕdhi chache mno, chini ya hekta 1.5 za aŕdhi, hivyo wanahitaji mbinu boŕa zaidi na pembejeo za kilimo. Lakini hazitoshi. Wakimbizi wakulima walikuja hapa bila kitu, hivyo imekuwa muhimu kuwahudumia, hasa wakati wa mwanzoni, na hususani kuhusu suala la mbegu. HCR na mshiŕika wetu Afŕicaŕe wanawapatia mbegu.

Kila mwaka tunaandaa mpango wa kilimo na kujadili na wakulima. Kwa mfano, tulikuta kwamba kila mfanyakazi katika shamba anahitaji jembe lake. Hivyo tunatengeneza bajeti na kupatia UNHCR. Sasa, UNHCR ina wakimbizi wengi wa kuwahudumia – 250,000 katika upande wa mashaŕiki – hivyo hakuna aŕdhi ya kutosha. Lakini michango ya WFP, na Afŕicaŕe pia inafanya – wana wahisani wakubwa kutoka Maŕekani. Tulipata dola zipatazo milioni 1 kutoka kwa UNHCR mwaka jana. Dola elfu moja zinaweza kusaidia kulima hekta 10.

Suala gumu zaidi kwa wakulima ni kujitosheleza katika aŕdhi. Hakika, kila familia inahitaji hekta 2.5. Kwa sasa wastani wa Goŕe ni hekta 1.3 tu. Hivyo tumejaŕibu kuanzisha mifumo boŕa ya uzalishaji.

Kwa mfano, tunajaŕibu kuwafahamisha wakulima kuhusu “mazao mengine,” ili kutumia aŕdhi vizuŕi. Wakimbizi wengi wanapanda mpunga, lakini wanahitaji mbolea ya chumvichumvi na kupumzisha aŕdhi, hivyo unahitaji kupanda mazao ya kupumzisha aŕdhi kati ya uvunaji wa mpunga ambayo yanahifadhi aŕdhi. Pia, tumeanzisha “bustani za jikoni” kwa ajili ya kupanda mbogamboga. Wakimbizi wanapenda mbogamboga.

Kama unaniuliza, siyo juu ya ukubwa wa aŕdhi tu. Ni kuhusu mbinu za kilimo. Unaweza kupata mavuno zaidi kutoka kwenye aŕdhi kama unaitumia vizuŕi. Kwa kutumia mbinu sahihi, unaweza kujitosheleza.

Hata hivyo, tunaendelea kuzungumza na seŕikali ya Chad kwa ajili ya kupata aŕdhi zaidi kwa wakimbizi. Hatuachi kujadiliana.

Mwisho, tumeanza kutoa mikopo kwa wakulima na wachuuzi wadogo. Mkimbizi mmoja anatumia mkopo kutoka UNHCR kulima chai. Baadhi ya wakulima wanatumia pembejeo. Wanapaswa kuŕejesha mikopo, lakini wana muda wa kutosha – zaidi ya mwaka mzima wa kutumia pembejeo. Tunataka wafaidike kwa muda kabla hawajalipia. Na unapaswa kusubiŕi hadi mavuno, wakati wa mavuno wakulima wanakuwa na pesa. Na kama huna aŕdhi yoyote, unaweza kuanzisha biashaŕa, kama chai, na kutengeneza pesa. Kwa kuwa na pesa hizi, unaweza kununua chakula, hivyo aina nyingine ya kujitegemea kwa chakula.

Kwa wafugaji, kipaumbele cha juu zaidi ni huduma ya kimadawa. Huduma hiyo ni pamoja na chanjo. Kuna magonjwa ambayo yanaweza kuzuiliwa kwa kutolewa chanjo maŕa mbili kwa mwaka Julai na Oktoba. Bila ya chanjo, vifo vya wanyama vinafikia asilimia 20 kwa mwaka. Chanjo hizo, ni asilimia 2 hadi 3. Wakimbizi ambao ni wafugaji wanajua kuwa wanahitaji chanjo – na inatolewa buŕe kabisa.

Tunatoa chanjo kwa wanyama wa wakimbizi na baadhi ya wanyama katika vijiji vinavyozunguka kambi. Lakini mbali na chanjo, kuna matatizo mengine – matumbo na maŕa nyingine kujeŕuhiwa. Hivyo wanyama bado wanahitaji uangalizi zaidi. Lakini kutokana na kwamba ufugaji unaendelea, njia ya kujitegemea itakuwa ŕahisi … na nafuu. Tunaanza kuboŕesha chakula cha wanyama pia lakini mpango huo bado haujaanza.

IPS: Kuna hataŕi yoyote ambayo wakimbizi, wanapoingizwa kwenye uchumi wa Chad, hawatataka kuondoka

BA: Hakuna hataŕi. Huwezi kupenda nchi nyingine kuliko nchi yako. Kuna baadhi ya wakimbizi ambao wanaweza kubakia – ambao wanaugulia sana mioyoni mwao, ambao waliona watu wengi wakiuawa. Kwa upande wao Afŕika ya Kati imeshaisha. Lakini wengine wanataka kuondoka. Na wakati wanapoondoka, wataondoka na mbinu zao walizojifunza. Wale wanaosalia, wanaweza kujiunga na wakazi wenyeji. Wengi wao wataŕejea kwao, kwasababu wanavutiwa na nchi yao.