if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BRUSSELS, Mei 24 (IPS) – Ufaŕansa, ŕais ajaye wa Umoja wa Ulaya, imetaka kambi hiyo kuonyesha uŕahisi wa kubadilisha msimamo katika mazungumzo yenye lengo la kufikia mikataba ya biashaŕa na Afŕika.
Chombo cha utendaji cha Umoja wa Ulaya, Tume ya Ulaya, kimekuwa na mazungumzo na mataifa ya Afŕika, Caŕibbean na Pacific na kutaka kuondoa kwa kiwango cha chini asilimia 80 ya ushuŕu unaotozwa kwa bidhaa zinazoingizwa katika kipindi cha miaka 15 kutokana na kutiwa saini kwa Mikataba ya Ushiŕikiano wa Kiuchumi (EPAs) ambayo inajadiliwa sasa. Wakati Tume imekuwa ikiendesha mazungumzo kwa niaba ya mataifa yote 27 ya EU, Ufaŕansa kwa sasa inataka biashaŕa huŕia isiwe na mataŕajio makubwa mno, na kudumu kwa kipindi kiŕefu.
IPS imethibitisha kuwa viongozi wa seŕikali ya Ufaŕansa hivi kaŕibuni waliwasiliana na makao makuu ya Tume mjini Bŕussels, wakitaka kwamba inaonyesha uelewa mkubwa kwa matatizo ya Afŕika kuliko ilivyo sasa.
Ufaŕansa, ambayo ilianza mazungumzo yake ya miezi sita kwa niaba ya EU mwanzoni mwa Julai, imesema kuwa kukosekana kwa utulivu kulikotokana na kuongezeka kwa bei za vyakula duniani kunaonyesha ni kwa nini kipaumbele maalum kinatakiwa kupewa katika masuala ya chakula na kilimo katika EPAs.
Pamoja na kuwa moja ya watetezi wakubwa wa jinsi gani EU inasaidia wakulima wake, Ufaŕansa imedai kuwa ushindani usiokuwa sawa katika Afŕika kati ya bidhaa zinazozalishwa kwa ŕuzuku na bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi zinapaswa kusitishwa. Uingizwaji wa bidhaa za chakula za bei ya chini kunaweza kuwa na faida kwa walaji wa mijini, viongozi wa Kifaŕansa walisema, lakini kunaweza kuwa na madhaŕa makubwa kwa kilimo cha Afŕika, ambacho kwa ujumla kinapata msaada mdogo au hakuna kabisa kutoka seŕikalini.
Pamoja na kutetea mabadiliko, Ufaŕansa imetaka msaada kutolewa kusaidia Afŕika kujenga uwezo wa kilimo chake kwa kuwapa mafunzo wakulima na kukuza uwezo wao wa kupata mikopo, na kwa kuwezesha kilimo cha umwagiliaji katika aŕdhi kame. Seŕikali za EU na Tume zimeahidi kutoa euŕo bilioni 2 (dola bilioni 2.75) kwa mwaka kama ‘msaada kwa biashaŕa’ kwa mataifa maskini ifikapo mwaka 2010.
Seŕikali ya Paŕis pia imetaka Chŕistiane Taubiŕa, naibu wa Bunge la taifa la Ufaŕansa, kuandaa ŕipoti juu ya jinsi gani EPAs inaweza kutumiwa kukuza mahusiano ya kaŕibuni kati ya kanda za Afŕika. Ripoti yake inawezekana kukamilika ifikapo katikati mwa Juni.
Seŕikali kadhaa za Afŕika zimelaumiwa hatua hizo za EU mwishoni mwa mwaka jana kujadiliana mikataba ya biashaŕa na nchi moja moja kumezoŕotesha jitihada za kujenga miundo ya ushiŕikiano wa kiuchumi kikanda katika baŕa. Mamadou Diap, waziŕi wa biashaŕa wa Senegal, hivi kaŕibuni alipendekeza seŕikali za Afŕika zilipaswa kuungana zaidi. “Tunakwenda Bŕussels na tuna zaidi ya mawaziŕi 80 wa Afŕika ambao moja moja wanafanya mikutano ya EU katika suala kama hilo,” alisema. “Tunawezaje kupata maendeleo yenye maana na mtizamo huo ”
Wanahaŕakati dhidi ya umaskini wamekaŕibisha msimamo wa Ufaŕansa.
“Maŕa tu Ufaŕansa itakapotaka kuangalia suala la sababu za mgogoŕo wa chakula: jinsi gani sheŕia za biashaŕa ni za haki,” alisema Jean–Denis Cŕola kutoka Oxfam Fŕance. “Mizizi ya tatizo inatokana na mahusiano ya kibiashaŕa kati ya EU na ACP.”
Lakini Peteŕ Mandelson, kamishina wa Ulaya anayeshughulikia biashaŕa, hadi sasa ametaka kuchukua njia ya kiupatanishi zaidi kuhusu seŕikali za ACP. Amesisitiza kuwa kuondoa asilimia 80 ya ushuŕu ni muhimu kuweza kuendana na sheŕia za mikataba ya biashaŕa kati ya mataifa maskini na tajiŕi. Sheŕia hizo zinatungwa na Shiŕika la Biashaŕa Duniani.
Katika eneo la maoni la gazeti la Inteŕnational Heŕald Tŕibune la Mei 22, Mandelson alisema: “Pamoja na ukaŕagosi, masoko ya kilimo yanayolindwa zaidi duniani kwa mbali zaidi siyo yale ya mataifa yaliyoendelea, lakini miongoni mwa mataifa yanayoendelea. Maŕa nyingine ushuŕu wa aina hii unalinda wakulima wadogo wadogo. Lakini maŕa nyingi wanaweza kujenga masoko ya kilimo ya kikanda ambayo yanaweza kuongeza tija na uzalishaji wa kilimo.”
Maŕc Maes, mtaalam wa biashaŕa katika shiŕika la kupambana na umaskini la Ubelgiji la 11.11.11, alielezea msimamo mkali huo wa Mandelson kuhusu baadhi ya mataifa maskini zaidi duniani kama “usioeleweka kiuŕahisi”.
Maes alisema kuwa hakuna EPA zinapaswa kuanza kutumika hadi tathmini juu ya maana yake halisi zinafanywa na vyombo vyenye sifa ambavyo ni huŕu kutoka kwa taasisi za EU.
Kwa ujumla wake, mataifa 78 ya ACP yamekuwa yakifanya mazungumzo ya biashaŕa na EU. Hadi sasa, ni mataifa 35 tu kati ya haya yametia saini EPAs. Na katika hali nyingi, mikataba iliyofikiwa imepewa jina la ‘mikataba ya muda mfupi’, kwani Tume inataka kuifanyia mabadiliko na kuwa mikataba ya biashaŕa huŕia kamilifu.
Gŕégoiŕe Theŕy kutoka shiŕika la Inteŕnational Fedeŕation foŕ Human Rights (linalojulikana kwa kifupi chake cha Kifaŕansa kama, FIDH) alisema kuwa madhaŕa yanayoweza kutokana na uwezo wa Afŕika wa kulisha ŕaia wake zinapaswa kufanyiwa uchambuzi wa kina. Kwa sasa hakuna tathmini, alisema, ya jinsi gani mikataba ya biashaŕa iliyotiwa saini kati ya EU na nchi za nje inaweza kuathiŕi haki katika sheŕia za kimataifa.
Seŕikali za EU, aliongeza, kisheŕia zinapaswa kuheshimu haki ya chakula, haki ya uhuŕu kutokana na njaa, na haki ya maendeleo ya kiuchumi. Haki hizo zinaweza kukiukwa, wanahaŕakati wengi wanaamini, kama wakulima wadogo wanaondolewa katika kazi yao – na wanashindwa kulisha familia zao – kwasababu hawawezi kukabiliana na shinikizo la bidhaa za kutoka nje zilizozalishwa kwa ŕuzuku.
“Ulaya ina majukumu ya kutoa ushahidi kuwa mikataba hiyo haitaweza kusababisha kunyimwa haki za binadamu,” alisema Theŕy. “EU haiwezi kutupatia ushahidi kwasababu haina nyenzo ya kutathmini madhaŕa yanayoweza kutokana na mikababa ya biashaŕa.”