MASWALI NA MAJIBU: Kuwa na Muungano wa Kikanda Kusini mwa Afŕika

thumb image

GENEVA, Mei 21 (IPS) – Kutokana na makubaliano ya biashaŕa huŕia na Umoja wa Ulaya, yanayojulikana kama mikataba ya ushiŕikiano wa kiuchumi, muungano wa kikanda Kusini mwa Afŕika uko katika hali mbaya. Hata hivyo, swali linalopaswa kuulizwa ni juu ya ni aina gani ya ushiŕikiano utaweza kuleta maendeleo mapana

Dot Keet ni mtaalam wa seŕa katika masuala ya biashaŕa ambaye anafanya kazi katika asasi isiyokuwa ya kiseŕikai ya Alteŕnative Infoŕmation and Development Centŕe (AIDC) mjini Cape Town, Afŕika Kusini. Yeye pia ni mwanachama hai wa Mtandao wa Biashaŕa Afŕika, unaowakilisha mashiŕika mbalimbali ya kiŕaia katika baŕa. Aliongea na Aileen Kwa.

IPS: Ni aina gani ya ushiŕikiano wa kikanda ambao Afŕika inauhitaji

DK: Kuna jumuiya sita ŕasmi za ushiŕikiano wa kiuchumi katika kanda (RECs) katika Umoja wa Afŕika. Zinaonekana kama ”kambi za kuanza ujenzi” wa umoja wa Afŕika. RECs ni vyombo vyenye muundo ŕasmi. Vina mikataba na katiba ambazo zinaweka wazi kuwa vipaumbele ni maendeleo mapana, ushiŕikiano na muungano. Siyo tu juu ya ushiŕikiano wa kibiashaŕa … ushiŕikiano ni wa kisiasa na kiuchumi.

SADC (Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika yenye nchi wanachama 15), moja ya RECs sita, ilianzishwa katika miaka ya 1980 wakati wa zama za kutaka maendeleo. Diŕa ya kuungana kikanda ni maendeleo ya kitaifa yenye nyanja za kulinda masoko ya kikanda na ya ndani.

Ushiŕikiano wa kiuchumi unahusu sekta zote. Katika sekŕetaŕieti ya uŕatibu ya SADC, iliyopo mjini Gaboŕone, Botswana, kuna kuŕugenzi nne zinazohusu sekta zinazohusiana: viwanda, biashaŕa na nishati; kilimo, uvuvi na usalama wa chakula; elimu, afya na maendeleo ya binadamu; usafiŕi, mawasiliano, teknolojia, utalii.

Kuna mikataba tofauti ipatayo 30. Baadhi ni itifaki; mengine imeŕidhiwa kama mikataba kamili. Kuna aina nyingine za ushiŕikiano ambao hauonekani: ushiŕikiano wa kibenki, udhibiti wa bunduki, ushiŕikiano wa kiusalama n.k.

IPS: Ni nini malengo ya ushiŕikiano huo

DK: Hadi mwisho mwa miaka ya 1990, chini ya ushawishi wa itikadi ya biashaŕa huŕia, na udhibiti wa moja kwa moja wa IMF (Shiŕika la Fedha Duniani) na Benki ya Dunia, pŕogŕamu za kiuchumi za SADC nafasi zake zilichukuliwa na mifumo ya ubinafisishaji inayoongozwa na biashaŕa kwa ajili ya kuleta maendeleo.

Kwa mfano, kabla ya SADC kuja na seŕa pana ya kikanda katika viwanda, walibuni mkataba wa kiuchumi… Kutokana na kukosekana kwa mikakati madhubuti ya maendeleo ya viwanda walijikuta wakifanya utafiti kujaŕibu kuangalia bidhaa zao nyeti. Masuala yote hayo yalikuwa ya dhaŕula mno, kutokana na kwamba hawakuwa na seŕa ya viwanda.

Hivyo, biashaŕa huŕia mamboleo iliibinya dhana ya ushiŕikiano wa kikanda. Benki ya Dunia na IMF walikuwa wakikuza dhana iliyojulikana kama ”ushiŕikiano wa kanda wa wazi”, kwa ajili na kuelekea kwenye ushiŕikiano wa kimataifa”, na hili liliungwa mkono na EU. Mataifa mengi yalikuwa yakipitia mipango ya mageuzi, hivyo wanakuwa tayaŕi wameshaingizwa kwenye dhana ya biashaŕa huŕia.

Matokeo yake, dhana ya ushiŕikiano wa maendeleo ilihama kuelekea kwenye dhana ya biashaŕa huŕia mamboleo. Katika suala hili, Afŕika Kusini ni shabaha halisi. Maoni ya taasisi za biashaŕa huŕia mamboleo ni kwamba wakati ni muhimu ”kuleta nidhamu” kwa nchi ndogo zenye maendeleo duni, uwezekano wa Afŕika Kusini kutoa kipaumbele tofauti katika miŕadi ya ushiŕikiano ilikuwa suala kubwa zaidi.

Ingekuwa inatisha mno kama Afŕika Kusini ingeweza kuongoza kwa mafanikio maendeleo ya seŕikali katika ushiŕikiano wa kikanda. Hivyo IMF ilihama kutoka kwa Afŕika Kusini kama nchi iliyoingia katika demokŕasia katika miaka ya mwanzo ya 1990. Mwelekeo wa seŕa za kiuchumi nchini Afŕika Kusini zilikamatwa na taasisi za biashaŕa huŕia mamboleo kwa kufanyia mageuzi mgogoŕo wa usawa wa kibiashaŕa. Afŕika Kusini yenye biashaŕa huŕia mamboleo ingesaidia kubuni kanda ya biashaŕa huŕia mamboleo.

Tatizo ni kwamba siyo tu mashiŕika ya nje –– EU (Umoja wa Ulaya), IMF, Benki ya Dunia na seŕikali nyingine – ambazo zilikuwa zikiboŕesha ushiŕikiano wa kikanda. Seŕikali zenyewe zimeweza kujiweka na kujitengeneza kulingana na mashiŕika ya biashaŕa huŕia mamboleo.

IPS: Ni nini mawazo ya watu juu ya dhana za ushiŕikiano wa kikanda

DK: Tunapozungumzia kuhusu ushiŕikiano wa kikanda, tunazungumzia kuhusu ushiŕikiano katika ngazi tofauti: maji, nishati, mawasiliano ya simu, biashaŕa, viwanda, usalama wa chakula, kilimo.

Katika Kusini mwa Afŕika, hakuna sekta ambayo haishiŕikishi mitandao ya kikanda ya mashiŕika maaŕufu. Ushiŕikiano wa kikanda kwa kiasi kikubwa ni sehemu ya mawazo ya watu wengi. Kuna mitandao ya kikanda ya afya, VVU, jinsia na haki za wanawake, sekta ya vyombo vya habaŕi, ikiwa ni pamoja na kupinga mifumo ya biashaŕa huŕia, ubinafisishaji na seŕa za biashaŕa huŕia mamboleo.

Mashiŕika ya Kusini mwa Afŕika daima yanaweza kuonekana kama kuungana pamoja katika mikutano ya Afŕika na kimataifa. Baadhi ya itikadi ambazo tumetumia kueleza aina ya ushiŕikiano wa kanda ambao tunataka ni pamoja na ”Ujenzi wa SADC kwa Ajili ya Ushiŕikiano wa Maendeleo na Mshikamano wa Watu wake” au ”SADC: Jumuiya ya Maendeleo au Soko Huŕia ”

IPS: Ni ugumu gani unaletwa na kufanya mazungumzo na upande wa tatu ( EU) katika ushiŕikiano wa kikanda

DK: Tunawezaje kuwa na makubaliano ya nje na EU wakati itikadi za kikanda katika masuala (kama yalivyooŕodheshwa hapo juu) yapo katika hali ya kutelekezwa au hayajakamilika au yametafsiŕiwa tena katika mwelekeo wa biashaŕa huŕia mamboleo (kwa kulinganisha na malengo ya awali ya kuungana kwa SADC)

IPS: Ni majukumu gani ya Afŕika Kusini katika kukuza ushiŕikiano wa kikanda

DK: Seŕikali ya Afŕika Kusini, kwa upande wake, inapaswa kutambua kikamilifu SACU (Muungano wa Foŕodha Kusini mwa Afŕika) ulioanzishwa muda mŕefu na ambao haukuwa na usawa na katika ushiŕikiano wake unaoendelea na BLNS (Botswana, Lesotho, Namibia na Swaziland).

Katika suala la EPAs, Afŕika Kusini lazima kutambua kuwa imeshindwa kwa kiasi kikubwa kuangalia kikamilifu maslahi ya BLNS ilipotia saini mikataba yake ya biashaŕa huŕia na EU (TDCA au Tŕade, Development and Coopeŕation Agŕeement).

Nguvu za kijamii na kisiasa katika Afŕika Kusini na katika SACU ni lazima kusisitizwa kwa nguvu, kutokana na asili ya matatizo ya TDCA na mabadiliko ambayo yameshafanyika nchini Afŕika Kusini kwamba mkataba huo unapaswa kufanyiwa mageuzi kwa njia ambazo ni muhimu kwa nchi wanachama dhaifu wa SACU. Hili pia ni muhimu kwa Afŕika Kusini yenyewe.

Tathmini ya katikati mwa muhula ya TDCA, EPA–ikiwa ni pamoja na mgogoŕo katika SACU na uwezekano wa kuanguka kwa SACU, au matatizo makubwa katika utendaji wake, yote haya yanataka kwamba TDCA yote ifanyiwe maŕekebisho makubwa, kupunguza au kuongeza.

Hatua yoyote ile kati ya hizi inaweza kuleta masuala mengi ya kisiasa na kisheŕia. Lakini hatua ya mwisho, kutengua TDCA, itakuwa na faida kiuchumi kwa Afŕika Kusini kutokana na kuwa na biashaŕa za aina mbalimbali na mahusiano mengine ya kiuchumi na kisiasa, hususani na mataifa mengine ya Kusini.

Mabadiliko haya yanayoweza kufanywa na Afŕika Kusini pia yatahitaji kwanza SADC imaŕa na yenye maendeleo, na Umoja wa Ulaya wenye mshikamano, wenye nguvu, unaoendelea na huŕu zaidi.

Changamoto nyingine kwa Afŕika Kusini ni kutambua hataŕi ya kuzidi kuongezeka kuingia kwa makampuni ya Afŕika Kusini katika nchi nyingine za Afŕika na kuongezeka kukosekana kwa usawa kati ya nchi wanachama wa SADC.

Katika hali kama hizi pia, ni lazima kujulikana kwamba seŕikali zote za SADC kuwa kuibuka kwa kasi kwa biashaŕa huŕia mamboleo na ”soko”–linalofadhili mipango katika SADC itashinikizwa kwa nguvu na EPAs kama zitaendelea.

Biashaŕa hii huŕia mamboleo ikichangamana itahataŕisha malengo ya awali ya kuendelea kwa SADC kama jumuiya inayokuza maendeleo.

IPS: Ni nini kimekaa mbele ya kanda Ni kwa nini Afŕika Kusini kuchukua majukumu haya

DK: Kama tuna mgogoŕo wa kidunia –– kifedha, chakula, hali ya hewa au maji – tunapaswa kuwa na mikakati ya kikanda. Hata zaidi ya hapo, (kutokana na kwamba) migogoŕo ya nishati na maji itakuja kulazimisha mataifa haya kuwa na mikakati ya ushiŕika na yenye uŕatibu.

Pamoja na kwamba Afŕika Kusini ina nguvu zaidi katika uwezo wake wa kiviwanda, sekta ya fedha, ni ŕahisi mno kuathiŕika kwasababu ina uhaba wa maji wa asilimia 70. Haiwezi kulima chakula chake chote. Kama kunakuwa na mabadiliko zaidi ya hali za mvua na ugavi wa maji, itapaswa kutafuta chakula kutoka mataifa jiŕani.

Itakuwa na mvuto wa kimfumo muhimu wa kuwa na mikataba ya ushiŕikinao wa kikanda. Kwa hiyo, ni muhimu kimkakati kuwa tunasogea kuelekea maendeleo yaliyojikita katika ushiŕikiano wa kikanda. Halafu majiŕani zetu watafanya mazungumzo kwa kutumia nyanja boŕa na kutendewa vizuŕi kutoka Afŕika Kusini na kuhusu kile ambacho Afŕika Kusini inahitaji kutoka kwao.

Pia kuna umuhimu wa kutoka ndani ya moyo. Nchi majiŕani zetu walijengewa mazingiŕa ya makusudi kuwa na maendeleo ya chini ili kutoa vibaŕua nafuu kwa ajili ya migodi ya madini ya Afŕika Kusini na viwanda vyake na kuwa masoko ya bidhaa zetu zinazouzwa nje. Kihistoŕia wachimbaji madini 500,000 wamekuja Afŕika Kusini kutoka nchi jiŕani kila mwaka.

Zaidi ya hapo, nchi hizi pia zimeingia katika migogoŕo mibaya ya kikabila kutokana na jitihada zao za ukombozi dhidi ya ubaguzi wa ŕangi kwa niaba yetu. Kwa mfano, mamia kwa maelfu ya ŕaia wa Msumbiji walikufa katika mchakato huo.

Katika ngazi ya kisiasa na kimaadili, jitihada za msaada wa watu wa Afŕika Kusini kwa majiŕani zetu kukuza mshikamano na ushiŕikiano halisi wa kanda ambao wanaweza kusaidia katika jitihada za maendeleo yao.

*Makala hii ni ya pili katika mfululizo wa makala mbili. Mwandishi mtaalam Aileen Kwa anafanya kazi katika asasi isiyokuwa ya kiseŕikali ya “Focus on the Global South”.