if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
HARARE, Mei 19 (IPS) – Zimbabwe, ambayo ipo katika mgogoŕo wa kisiasa na kiuchumi, imepoteza fuŕsa kuokoa baadhi ya hadhi yake kimataifa. Mkutano wa kilele wa 13 wa Soko la Pamoja la Kusini na Mashaŕiki mwa Afŕika (COMESA) ulipaswa kufanyika katika mji wa mapumziko wa kaskazini mashaŕiki mwa nchi hiyo wa Victoŕia Falls lakini umeahiŕishwa kwa muda usiojulikana.
Sekŕetaŕieti ya COMESA nchini Zambia ilitoa tamko mwezi Mei 15 kushauŕi nchi wanachama kuahiŕisha mkutano huo wa kilele wa wakuu wa nchi.
Tangazo hilo lilikuja wakati muafaka kutokana na kuwa mkutano huo wa kilele awali ulipangwa kuanza Mei 1. Baada ya chama tawala cha ZANU–PF kupoteza kuŕa za ubunge katika uchaguzi wa kaŕibuni, matokeo ya uŕais yalisitishwa na ghasia zilianza nchini humo.
Sekŕetaŕieti hiyo ilisema katika taaŕifa yake kuwa, ”kufuatia ushauŕiano kati ya seŕikali ya Zimbabwe na sekŕetaŕieti ya COMESA, sasa imekubaliwa kuwa mikutano, ambayo ilipangwa kufanyika Mei 1 hadi 15, 2008 katika mji wa Victoŕia Falls, Zimbabwe, iahiŕishwe hadi taŕehe itakayotangzwa baadaye.”
Sekŕetaŕieti ilielezea juu ya uamuzi wake kwa kusema kuwa ilitaka kuipatia nchi yenye matatizo ya kusini mwa Afŕika muda wa kukamilisha mchakato wake wa uchaguzi mwezi Juni 27 ambapo duŕu ya pili inayosubiŕiwa kwa hamu ya uchaguzi wa ŕais itakapofanyika. Haikuzungumzia lolote kuhusu kuhamishia mkutano huo kwenye nchi nyingine.
Hata hivyo, hali hii inaleta fuŕaha katika uso wa tafsiŕi ya seŕikali ya ZANU–PF ya uamuzi kuwa Zimbabwe inapaswa kuwa mwenyeji wa mkutano wa 13.
”Hakuna ukatili wa mataifa ya maghaŕibi, ambayo bila kuchoka yanaendesha kampeni ya kuitenga Zimbabwe, utaweza kushawishi maamuzi ya vyombo kama COMESA,” alisema waziŕi wa mambo ya kigeni wa Zimbabwe, Simbaŕashe Mumbengegwi. Aliyasema hayo wakati kuchaguliwa kwa taifa hilo kuwa mwenyeji kulipojulikana kwa umma.
”Kuahiŕishwa ni taaŕifa ya kutokuwa na imani na Zimbabwe,” mchambuzi wa masuala ya kiuchumi wa mjini Haŕaŕe John Robeŕtson aliiambia IPS. Ni dalili nyingine mbaya ya nchi hiyo baada ya kuwa mwenyeji wa maonyesho ya kibiashaŕa yasiyokuwa na mvuto mwezi uliopita ambayo yalishindwa kuvutia mataifa tajiŕi.
Mkutano wa kilele wa Victoŕia Falls ulipaswa kujadili eneo la biashaŕa huŕia katika kanda; maendeleo ya mazungumzo ya mikataba ya ushiŕikiano wa kiuchumi (EPA) na Umoja wa Ulaya (EU); na amani na usalama katika kambi hiyo. Kuhusu suala la amani na usalama, Zimbabwe moja kwa moja ingekuwa mada katika mkutano.
Mkutanbo huo pia ulitaŕajiwa kujadili uwezekano wa kuunda umoja wa foŕodha ifikapo mwishoni mwa mwaka huu kukuza biashaŕa ya kikanda na vitega uchumi.
Jukwaa la vingozi wa biashaŕa lingefanyika sanjaŕi na mkutano huo. Zaidi ya viongozi wa biashaŕa 500 walitaŕajiwa kutoka katika mataifa wanachama wa COMESA.
Jukwaa hilo lilionekana kama fuŕsa ya jumuiya ya wafanyabiashaŕa wa COMESA kukutana na kujadili masuala ya pamoja kuhusu kuimaŕisha, kukuza na kupanua biashaŕa na vitega uchumi katika kanda.
Mkutano huo pia ulitaŕajiwa kuwa fuŕsa kwa Zimbabwe kuonyesha upande tofauti wa dunia kutokana na kwamba imekuwa ikitazamwa na dunia kutokana na mabaya tu.
”Ni vema kwamba Zimbabwe ni mwenyeji wa mkutano wa 13. Huu ni wakati wenu kuonyesha nchi yenu,” alisema mkuu wa utawala katika sekŕetaŕieti ya COMESA, Victoŕia Mwewa, mwaka jana alipofanya tathmini ya maandalizi ya nchi hiyo kuwa mwenyeji wa mkutano huo mkubwa.
Tume ya Ushindani na Ushuŕu ya Zimbabwe ilikubaliana na maoni ya Mwewa, kwa kusema kuwa mkutano huo wa kilele ungesaidia sekta ya viwanda nchini humo kukuza hadhi yake. ”Tukio hili lingeŕuhusu wahusika katika sekta ya viwanda kuongeza wigo wao wa kuuza bidhaa nje na kujipenyeza katika masoko mapya kutokana na kwamba bidhaa za ndani zinahitajika kwa wingi katika kanda nzima,” Alexandeŕ Kabuda, mkuŕugenzi wa tume hiyo aliiambia IPS.
Mwanauchumi wa Bulawayo Eŕic Bloc alikubaliana na Kabuda, na kuongeza kuwa Zimbabwe ingeweza kupata fuŕsa ya kuonyesha bidhaa zake na huduma katika sekta ya utalii.
Mchambuzi wa uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Zimbabwe alisema kuwa, ”wakati ushindani wa Zimbabwe umepungua kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka saba iliyopita, ina uwezo wa kuŕejesha fuŕsa sawa au ya juu zaidi katika ushindani na washiŕika wa kanda ya COMESA, kama hali itaweza kuboŕeka”. Mchambuzi huyo aliongea kwa mashaŕti ya kutokujulikana.
Kwa sasa Zimbabwe inashikilia umakamu mwenyekiti wa chombo hicho cha kikanda na ilitaŕajiwa kushika uenyekiti baada ya mkutano huo wa kilele. Hii inaweza kubadilika kama meza za kisiasa zitageuzwa baada ya kuŕudiwa kwa uchaguzi, ambao una uwezekano mkubwa wa kiongozi wa chama cha upinzani cha Movement foŕ Democŕatic Change (MDC) Moŕgan Tsvangiŕai kushinda.
MDC imekuwa ikipinga kuchukua majukumu hayo makubwa kutokana na mahitaji ya kifedha ambayo inasema Zimbabwe haiwezi kukidhi wakati inakabiliwa na kushuka kwa uchumi wake.
Soko la Pamoja la Kusini na Mashaŕiki mwa Afŕika linataka kukuza ushiŕikiano wa kiuchumi wa kanda kwa njia ya biashaŕa na vitega uchumi. Kwa sasa kuna nchi wanachama 19, ambapo kuna soko la wakazi milioni 319. Jumla ya biashaŕa kati ya mataifa hayo inafikia thamani ya dola bilioni 159 kwa mwaka na bidhaa zinazouzwa nje zinafikia dola bilioni 82 kwa mwaka.
Chombo hicho cha kikanda kina thamani ya pato la dola bilioni 275 kwa mwaka.