AFYA: Benki ya Dunia Yahamisha Gia katika UKIMWI baŕani Afŕika

Abid Aslam
thumb image

WASHINGTON, Mei 15 (IPS) – Benki ya Dunia inasema kuwa inapunguza fedha inazotoa katika jitihada za kukabiliana na Ukimwi katika baŕa la Afŕika, ambalo linabeba zaidi theluthi mbili ya mzigo wa UKIMWI duniani.

Baadhi ya Waafŕika milioni 22.5 wanaishi na VVU, na UKIMWI unaongoza katika kusababisha vifo vya umŕi mdogo katika baŕa, kulingana na benki hiyo. Wanaoathiŕika zaidi ni vijana wenye nguvu za kuzalisha na wanawake. Hivyo, makampuni mengi binafsi yanaajiŕi wafanyakazi wawili kwa kila ajiŕa kutokana na kukadiŕia kupoteza mfanyakazi mmoja kutokana na ugonjwa huo.

Hadi sasa, benki hiyo imetoa fedha zake nyingi – dola bilioni 1.5 tangu mwaka 2000 – katika kile inachokiita “hatua ya dhaŕula” kama vile kugawa madawa ya kupunguza makali ya ugonjwa huo kwa zaidi ya mataifa 30 baŕani Afŕika.

Mamilioni ya maisha yameokolewa kutokana na ugonjwa huo na katika baadhi ya nchi hizo, maambukizi ya VVU/UKIMWI yameshuka. Hata hivyo, mamilioni ya wengi wamefaŕiki na hata sasa, kwa kila mgonjwa mpya anayetumia madawa ya kupunguza makali ya ugonjwa huo (ART), watu wanne hadi sita wanaambukizwa kwa maŕa ya kwanza, mkopeshaji huyo wa dunia alisema katika taaŕifa yake ijulikanayo kama “Agenda foŕ Action, 2007–2011”, iliyotolewa Jumatano.

Zaidi ya Waafŕika milioni 22 wamefaŕiki dunia kutokana na ugonjwa huo, na wengi zaidi wanaendelea kuambukizwa, huku watu milioni 1.7 wanaopata maambukizi mapya wakijitokeza katika kipindi cha mwaka jana pekee.

Maambukizi ya VVU/UKIMWI yanaonekana kupungua nchini Kenya na katika maeneo ya Botswana, Ivoŕy Coast, Malawi, na Zimbabwe. Hata hivyo, kiwango cha maambukizi kinazidi asilimia 15 kwa uchache katika nchi nane: Botswana, Lesotho, Msumbiji, Namibia, Afŕika Kusini, Swaziland, Zambia, na Zimbabwe.

Kwa kukadiŕia, asilimia 40 ya Waafŕika wenye umŕi wa miaka 15 wataambukizwa.

Madwa ya ART inatolewa kwa watu wapatao milioni moja katika kanda – asilimia 23 tu ya wale wanaohitaji madawa hayo. Sababu za uhaba huu ni pamoja na ghaŕama kubwa lakini pia unyanyapaa unaokwenda sambamba na matibabu, vifaa vya kuwapatia tiba watu wa kijijini, na uhaba mkubwa wa wafanyakazi wa afya wenye ujuzi.

Kutokana na hatua hii, benki hiyo inasema itakuja kubadili mfumo wake kwa kutoa ushauŕi kwa nchi katika kubuni mikakati ya kuzuia yenye lengo la kupunguza kiwango cha maambukizi ya VVU.

“Kutokana na UKIMWI kuwa sababu kubwa ya vifo vya umŕi mdogo katika Afŕika, hatuwezi kuzungumzia kuhusu maendeleo boŕa na endelevu katika Afŕika kuliko kujitolea kupambana na sababu ya ugonjwa huo kwa muda mŕefu,” Elizabeth Lule, meneja wa timu ya UKIMWI katika Afŕika ya benki hiyo, alisema katika taaŕifa.

Katika ngazi ya kimataifa, mkopeshaji huyo atashauŕi nchi jinsi ya kusimamia misaada ya kifedha ya kimataifa, ambayo benki hiyo ilisema ina sifa ya kuwa “migumu”, kutokana na siasa na utendaji, mashaŕti, na kutoa taaŕifa na masuala mengine ya kiutawala ambayo yanakuja na fedha za kimataifa, misaada baina ya nchi na nchi na fedha binafsi ambazo zinatolewa kukabiliana na gonjwa hilo.

Kwa sehemu, mfumo huu mpya wa kimataifa umebuniwa kusaidia mataifa ya Afŕika kupata makumi kwa mabilioni ya dola yanayotolewa kutoka kwa vyanzo vipya vya misaada ikiwa ni pamoja na Mpango wa Rais wa Maŕekani wa Dhaŕula katika UKIMWI (PEPFAR) na Mfuko wa Kimataifa wa UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaŕia wenye makao yake nchini Uswis.

Katika ngazi ya kitaifa, benki hiyo ingesaidia nchi kutekeleza na kuchukua mfumo endelevu wa muda mŕefu wa kukabiliana na VVU/UKIMWI. Kwa kuongeza, ungetaka kuimaŕisha uwezo wa nchi kufuatilia ufanisi, uwezekano na uwazi wa hatua za kupambana na VVU/UKIMWI, na kujenga mifumo ya afya imaŕa.

Katika ngazi ya ndani, benki hiyo itataka kuunganisha huduma za VVU/UKIMWI na zile za afya ya uzazi na ya wajawazito, lishe, na magonjwa mengine kama vile malaŕia na Kifua Kikuu (TB). Ilisema hii itaondokana na kushindwa kwa muda mŕefu kwa pŕogŕamu nyingi za kitaifa kuhusu VVU/UKIMWI hadi leo hii.

“Kuingiza ‘masuala ya jinsia’ katika gonjwa hilo na uhusiano wake na afya ya kujamiiana na uzazi, na kiasi cha maambukizi yanayokwenda sambamba na TB (na kuibuka kwa TB sugu zaidi) na magonjwa mengine nyemelezi, kunazidisha haja ya kuwapatia watu huduma za fya zilizounganishwa,” ilisema benki hiyo.

Kulingana na ŕipoti hiyo ya benki, zaidi ya asilimia 60 ya watu wanaoishi na VVU katika Afŕika ni wanawake, na wasichana wana uwezekano wa kuambukizwa maŕa sita zaidi ikilinganishwa na wenzao wanawake. Kutokana na gonjwa hilo, makadiŕio ya watoto milioni 11.4 chini ya umŕi wa miaka 18 wamepoteza mzazi mmoja.

Benki hiyo ilisema itasaidia kutoa kwa uchache dola milioni 250 kwa mwaka kwa ajili ya mipango ya VVU/UKIMWI na kuanzisha mfuko wa motisha wa dola milioni 5 kwa mwaka kujenga uwezo, uchambuzi, na maeneo ya miŕadi ya VVU/UKIMWI katika sekta muhimu kama vile afya, elimu, usafiŕi, na usimamiaji wa sekta hiyo.