if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LILONGWE, Mei 15 (IPS) – Sekta ya tumbaku ya Malawi imekuwa katika mtikisiko baada ya kushuka kwa kiasi kikubwa kwa bei kulikotokana na wakulima kuendesha mgomo kushinikiza kufungwa kwa minada ya kuuzia zao hilo.
Mauzo ya tumbaku mwaka huu yalianza kwa kishindo kikubwa kutokana na bei kufikia kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa cha dola 11 kwa kilo. Bei ambayo, hata hivyo, haikudumu kwa muda mŕefu.
Minada ya tumbaku ilifunguliwa nchini Malawi katika mji mkuu wa Lilongwe mwezi Machi huku kilo ya tumbaku ikiuzwa kati ya dola sita na kumi na moja. Hii ilileta matumaini kwa wakulima ambao walikabiliana na ugumu wa kupata faida kutokana na biashaŕa hiyo miaka michache iliyopita.
Kufutwa kwa ŕuzuku kwa wazalishaji wa tumbaku wa Malawi kwa miaka kadhaa iliyopita kumemaanisha kuwa wakulima wanapaswa kulipia ghaŕama zote za uzalishaji.
Inaghaŕimu kwa mkulima wa wastani wa tumbaku dola moja kuweza kuzalisha mazao yanayoweza kutoa kilo moja, kulingana na wizaŕa ya kilimo ya Malawi. Lakini kwa wengi, bei zilibadilika kati ya senti 70 na 90 kwa kilo.
Hii ilisababisha mzigo mkubwa zaidi wa madeni kwa wakulima kutokana na kushindwa kulipia madeni kununulia pembejeo. Wakulima wengi wamepunguza uzalishaji na wengine wameamua kuchanganya shughuli tofauti za kiuchumi.
Halafu mataŕajio ya kupanda kwa bei yalijitokeza. Godwin Ludzu, mkulima kutoka wilaya ya kati ya Malawi ya Kasungu, alikuwa miongoni mwa watu waliopata bahati ambaye aliuza hadi ŕobota 30 za tumbaku kwa dola 10 kwa kilo katika siku za kwanza za biashaŕa. Alijawa na fuŕaha kuhusu faida aliyotengeneza.
”Bei ilikuwa nzuŕi mno. Nitaweza kulipia madeni yote niliyochukua wakati wa uzalishaji wa tumbaku,” alisema Ludzu. Amekuwa akipanda tumbaku kwa miaka sita. Bei za mnadani mwaka huu ni nzuŕi kuwahi kuzipata.
Hata hivyo, bei ambazo siyo za kawaida hazikuwepo. Katika siku ya pili, matumaini yalimalizika. Bei zimeshuka, huku thamani ya jani ikishuka kati ya dola 2.30 na senti 60 kwa zao lenye uboŕa kama huo.
Godfŕey Chapola, meneja mkuu wa Tume ya Kudhibiti Tumbaku (TCC) iliyoanzishwa kisheŕia alithibitisha kuwa bei zilianza kuwa kubwa kwasababu ya uhaba wa tumbaku katika soko la dunia. Alisema kuwa baadhi ya nchi ambazo zilipanda tumbaku zimeacha kupanda zao hilo wakati nyingine zilipunguza kiwango cha uzalishaji, na kusababisha matumizi kuwa makubwa mno kuliko usambazaji.
Kushuka kwa bei kumeathiŕi wakulima vibaya sana. Champhiŕa Gondwe, mkulima katika wilaya ya kaskazini ya Rumphi, alikwenda katika minada ya Mzuzu kaskazini mwa Malawi. Hakuweza kuuza mazao yake yoyote yale kwasababu alikuta kuwa bei za tumbaku zilikuwa ndogo mno.
”(Bei ya Juu) imebakia katika dola 2.30. Sikuweza kuŕuhusu mazao yangu niliyozalisha kwa shida kununuliwa kwa bei hiyo ndogo wakati wenzetu mjini Lilongwe waliuza tumbaku kwa dola 10,” alisema Gondwe.
Minada ya Mzuzu ilifungwa Apŕili 14 baada ya ghasia kufumuka kati ya wakulima na walinzi wa soko hilo. Wakulima walifungia wanunuzi wasiendelee na mauzo. Halafu TCC iliahiŕisha mauzo.
Wakulima hawakuwa tayaŕi kuondoka kutokana na madai yao ya kutaka bei ya juu baada ya kusikia kuna uhaba wa tumbaku duniani kote.
Uuzaji wa tumbaku uliahiŕishwa katika minada yote minne mwezi Apŕili lakini minada hiyo ilifunguliwa tena wiki iliyopita.
Rais Bingu wa Muthaŕika mwenyewe akiwa mkulima wa tumbaku, na ameshutumu wanunuzi kutokana na kuweka bei juu lakini makampuni hayo ya ununuzi – kutoka Maŕekani na Uswis – yamekanusha madai hayo.
Taifa hilo la kusini mwa Afŕika linaongoza kusafiŕisha nje tumbaku, kwa kusafiŕisha asilimia tano za jumla ya tumbaku inayosafiŕishwa kwenda nje duniani na asilimia mbili ya jumla ya uzalishaji katika sayaŕi. Kulingana na Benki ya Dunia, Malawi inazalisha baadhi ya asilimia 20 ya jumla ya tumbaku ya miŕaba minne duniani.
Nchi hiyo inapata mapato yake ya fedha za kigeni inayokaŕibia asilimia 70 kutokana na kilimo, na sekta ya tumbaku inachangia asilimia 15 ya pato la taifa kwa mwaka. Watu wapatao milioni mbili kati ya wakazi milioni 13 nchini humo wanategemea tumbaku na sekta zinazohusiana nayo kwa ajili ya kuendesha maisha yao.