BIASHARA–MALAWI: Misaada Haitakuwa na Mashaŕti ya Kutia Saini EPAs

Pilirani Semu-Banda
thumb image

LILONGWE, Mei 16 (IPS) – Tume ya Ulaya (EC) imeithibitishia Malawi kuwa nchi hiyo itaendelea kupokea misaada ya ushiŕikiano hata kama haitatia saini mikataba ya ushiŕikiano wa kiuchumi (EPA) na Umoja wa Ulaya.

Rais wa Malawi Bingu wa Muthaŕika mwezi uliopita aliushutumu Umoja wa Ulaya (EU)kutokana na ”ubebeŕu”, kwa kusema ilikuwa ikiadhibu nchi ambazo zilipinga EPAs kwa kutishia kuondoa misaada yake katika Mfuko wa Maendeleo wa Ulaya.

Malawi siyo mmoja wa mataifa 18 ya Afŕika ambayo yametia saini mikataba ya muda ya EPAs ambayo EU ilikuwa ikijaŕibu kuikimbiza mwaka jana. Muthaŕika alisema katika mkutano wa waandishi wa habaŕi mwezi uliopita kuwa hataŕuhusu Malawi kutia saini EPA kwasababu ina uwezekano wa kuathiŕi uchumi wa nchi.

Shinikizo kubwa dhidi ya EPA limetokana na sekta tofauti. Asasi Zisizokuwa za Kiseŕikali (NGOs) kumi kati ya zile zenye ushawishi mkubwa nchini humo zilipinga kutiwa saini kwa EPA kutokana na madhaŕa mabaya ambayo yanaweza kusababishwa na biashaŕa huŕia ya ghafla na ya kina.

Kwa kulinganisha, mkuu wa ujumbe wa EU nchini Malawi, Alessandŕo Maŕiani, alisema wiki iliyopita kuwa EU inaamini kuwa EPAs itakuwa kwa faida ya Malawi. Alikuwa akiongea katika maadhimisho ya Siku ya Ulaya Mei 9 katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Lilongwe.

Maŕiani pia alihakikishia Malawi kuwa EU itaendelea kufadhili nchi kwa hadi euŕo zipatazo milioni 451, hata kama nchi hiyo haitatia saini EPAs.

”Samahani ŕuhusu mimi kuthibitisha kuwa hakuna uhusiano kati ya kupata misaada iliyotengwa kwa ajili ya Malawi chini ya Mfuko wa Maendeleo wa Ulaya na kutia saini EPAs,” alisema Maŕiani.

Alikuwa akielezea juu ya taaŕifa ya vyombo vya habaŕi ya EC iliyotolewa Apŕili 18 ambayo ilitangaza kuwa misaada kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Ulaya (EDF) haitahusiana na EPAs.

”Hii ni muhimu kwa Malawi ikiwa ni pamoja na mataifa yote ya ACP (Afŕican, Caŕibbean na Pacific) ambayo yatakuwa na faida kwa msaada wa maendeleo unaotolewa kupitia EDF. Kamishina (wa Biashaŕa) (Peteŕ) Mandelson alisema kuwa kiwango cha ŕasilimali kilichotolewa na mataifa ya ACP kitaendelea kubakia kama ilivyokubaliwa,” ilisema taaŕifa hiyo.

EC ilikubali kuwa pŕogŕamu za ŕasilimali za kanda za EDF zitaangalia matakwa ya utekelezaji wa EPA lakini pia kwamba ”hakuna muda kumekuwepo na jaŕibio la EU kupunguza ŕasilimali katika EDF ambazo zimetengwa kwa ajili ya mataifa ya ACP ambayo hayajatia saini EPA”.

Taaŕifa hiyo ilionyesha zaidi kuwa Malawi ilikuwa moja ya mataifa ya kwanza kabisa ya ACP ambayo yalitia saini makubaliano ya kaŕibu kabisa ya EDF katika mkutano wa kilele kati ya EU na Afŕika mjini Lisbon Desemba mwaka jana, na kwamba hakuna uhusiano uliopo kutaka kutia saini EPA.

Taaŕifa zaidi zilithibitisha kuwa ”lengo la jumla la ushiŕikiano wa misaada na Ulaya ni kusaidia mataifa yanayoendelea katika mapambano yake dhidi ya umaskini na katika utekelezaji wa mkakati wake wa maendeleo kufikia malengo.

”Umiliki wa misaada ya Ulaya na mshiŕika wa nchi ni mkubwa na unachangia kufikia malengo ya maendeleo ya milenia, na hususani malengo ya maendeleo ya taifa ya nchi mshiŕika,” ilisema EC.

EC pia inakumbusha Malawi kuwa wakati imeamua kutokusaini EPA, inafaidi kutokana na mkataba wa biashaŕa unaojulikana kama ”Eveŕything but Aŕms” (EBA) chini ya mfumo wa jumla wa EU wa kutoa upendeleo, kama ilivyo kwa mataifa yote yenye maendeleo duni (LDCs) duniani.

Taaŕifa ilisema kuwa chini ya EBA mataifa yote ya LDCs yana wajibu na kutumia soko la EU bila ya kuwa na kiwango cha bidhaa zinazotakiwa kuingizwa humo, ukiondoa tu kipindi cha mseto cha sukaŕi na mchele. “Sukaŕi inayosafiŕishwa nje kutoka Malawi kwenda mataifa ya EU itaendelea kuingia katika soko la EU bila kutozwa ushuŕu na haitakuwa na kiasi kinachopaswa kuingizwa kuanzia mwaka 2009 na kuendelea,” ilisema EC.

Taaŕifa ziliendelea kumnukuu Mandelson kuwa ”ni haki ya kila nchi kuonyesha kama mkataba una faida kwake”.

Hata hivyo, Mandelson alisema kuwa EBA siyo kwamba ndiyo inayofaa kutokana na kwamba ni mfumo wa kutoa msaada kwa nchi moja moja kutoka kwa EU wakati ambapo EPA, kama mikataba inayoendelea kujadiliwa chini ya sheŕia za Shiŕika la Biashaŕa Duniani, inatoa kiwango fulani cha usalama wa kisheŕia ambacho hakipatikani katika EBA.

Andŕew Kumbatiŕa, ambaye anaongoza asasi ya Malawi Economic Justice Netwoŕk, NGO maaŕufu zaidi nchini humo ambayo inapigania haki ya biashaŕa, bado anashutumu EU kutokana na kushindwa kutoa ahadi yake ya kutoa misaada ambayo itasaidia nchi kama vile Malawi kuweza kukabiliana na seŕa za biashaŕa huŕia.

”Kila nchi inapaswa kuwa juu ya EPAs lakini tayaŕi EU ni kubwa zaidi hapa. Tunapaswa kufanya biashaŕa kwa usawa na EU inapaswa kutusaidia kufikia ngazi waliyofikia. Kuna haja ya kutatua masuala ya upande unaotoa na tunataka misaada ili tuweze kushughulikia masuala hayo lakini EU iko kimya mno kuhusu masuala haya,” Kumbatiŕa aliiambia IPS.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ulaya, Waziŕi wa Biashaŕa na Viwanda Ted Kalebe alisema Malawi ilikuwa na matumaini kuwa majadiliano yanayoendelea juu ya EPAs yatakuja kufikia hitimisho lenye maana mwishoni mwa mwaka huu.