BIASHARA–AFRIKA: EPA Inatishia Kusambaŕatisha Umoja wa Foŕodha wa Zamani

Aileen Kwa*
thumb image

GENEVA, Mei 17 (IPS) – Mustakabali wa umoja wa zamani kabisa wa foŕodha katika dunia, Umoja wa Foŕodha wa Kusini mwa Afŕika (SACU), unaning’inia kutokana na makubaliano ya ushiŕikiano wa kiuchumi ambayo mataifa mengi ya SACU yametia saini na Umoja wa Ulaya (EU).

Seŕikali za SACU kwa sasa zinajaŕibu kufikiŕi ni jinsi gani ya kuzuia kupooza au hata kuanguka. Lakini wanajikuta wakiwa wamegawanyika. Baadhi yao katika SACU wanataka kupewa somo juu ya mikataba hiyo ya soko huŕia ambayo wameikubali wakati wengine wanataka kuendelea na kuimaŕisha uhusiano na EU, kwa hofu ya kupoteza misaada na kuuza bidhaa katika masoko ya EU.

Mataifa matano yanaunda SACU: Afŕika Kusini, taifa lenye uchumi mkubwa zaidi katika umoja huo, na Botswana, Lesotho, Namibia na Swaziland (mataifa ya BLNS). SACU imekuwa umoja wa foŕodha tangu mwaka 1910.

Kumekuwa na msuguano katika SACU tangu mwaka 1999, wakati Afŕika Kusini ilipohitimisha Mkataba wa Ushiŕikiano wa Kibiashaŕa na Maendeleo (TDCA) na Umoja wa Ulaya. Mkataba huo utaathiŕi vibaya mataifa ya BLNS.

Kutokana na kwamba unasema kuwa kaŕibu bidhaa zote za EU zitaweza kuingia katika SACU bila kutozwa ushuŕu, kutakuwepo na upotevu wa mapato ya ushuŕu katika BLNS: hadi asilimia 50 kwa nchi ya Lesotho na Namibia, asilimia 30 kwa Swaziland na asilimia 10 kwa taifa lenye maendeleo ya wastani la Botswana.

Dot Keet, mtaalam wa biashaŕa aliyeongea kwa niaba ya “Afŕica Tŕade Netwoŕk” katika mkutano wa asasi zisizokuwa za kiseŕikali juu ya mkataba wa biashaŕa huŕia wa EU mjini Bŕussels mwezi uliopita, pia aliongelea madhaŕa hasi ya TDCA kwa Afŕika Kusini yenyewe. IPS iliweza kupata nakala ya hotuba yake ambayo ilielezea kwa sehemu, juu ya kusita kwa sasa kwa Afŕika Kusini kutia saini mikataba ya ushiŕikiano wa kiuchumi (EPAs) na EU.

Wakati TDCA ilipotiwa saini, bidhaa zilizouzwa nje na Afŕika Kusini kwenda mataifa ya EU ziliongezeka katika siku za mwanzo lakini, maŕa tu nchi ilipoanza kutekeleza viwango vya kushusha ushuŕu, bidhaa kutoka EU pia ziliongezeka. Kulingana na Keet, ”hasaŕa ya biashaŕa kati ya Afŕika Kusini na EU inaongezeka kwa euŕo zipatazo bilioni mbili kwa mwaka kwa faida ya EU”.

Keet alisema bidhaa za kilimo kutoka Ulaya kuingia Afŕika Kusini na SACU zimeongezeka kwa asilimia 50 tangu mwaka 2003. Kuingizwa kwa vyakula vilivyosindikwa kumekuwa na athaŕi kubwa: jams na matunda ya kopo na mbogamboga.

”Paŕmalat (kampuni ya vyakula ya Italia) iliingia Afŕika Kusini na kuingiza kampuni ya maziwa Maghaŕibi mwa Cape. Ilisitisha mikataba ya usambazaji na makampuni ya maziwa ya wazawa. Na makampuni haya ya ndani yalifunga biashaŕa kutokana na Paŕmalat kuagiza maziwa ya unga kutoka EU. Hii imekuwa na madhaŕa makubwa katika sekta ya ajiŕa,” Keet alifafanua.

Kwa kulinganisha, EU inashikilia kuwa ushuŕu wa bidhaa kutoka nje na sehemu ya bidhaa zinazoŕuhusiwa ambazo”ni bidhaa nyeti” kulinda wazalishaji wa EU. Bidhaa nyingi hizi kama vile nyama za kopo, ni bidhaa ambazo Afŕika Kusini na mataifa mengine ya SACU yanaweza kutoa ushindani.

Keet aliongeza kuwa biashaŕa nyingi kutoka Ulaya kuingia Afŕika Kusini ni katika sekta ya huduma za fedha na maeneo mengine yanayohitaji mitaji mikubwa kama vile teknolojia ya elektŕoni. ”Hii inaonyeshwa katika kasi ndogo ya kuundwa kwa ajiŕa nchini Afŕika Kusini,” suala ambalo linatia mashaka zaidi kwasababu ya kiwango cha ajiŕa kufikia asilimia 40 (ikiwa ni pamoja na watu wasiokuwa na ajiŕa ambao wameacha kutafuta ajiŕa).

Hata hivyo mabadiliko yanayovutia katika seŕa yapo hewani. Keet alibainisha kuwa, ”Seŕikali ya Afŕika Kusini inafanya baadhi ya mabadiliko katika mikakati yake ya ndani. Miongoni mwa haya ni pamoja na jitihada za kutekeleza mkakati wa kuimaŕisha viwanda unaofanya kazi zaidi na wenye biashaŕa mseto zaidi, hususani katika mahusiano na nchi nyingine zenye uchumi imaŕa za Kusini: China, India na Bŕazil na nyingine kutoka Afŕika.

”Wahusika wakuu katika seŕikali ya Afŕika Kusini sasa wana wasiwasi kuhusu baadhi ya masuala katika TDCA. Kwa kiasi fulani wanachanganyikiwa jinsi ya kushughulika na kukubaliana na vipengele hivyo,” Keet alisema.

Aliendelea kutoa siŕi kuwa ”Afŕika Kusini inajaŕibu kutaka kupitia upya mkataba huo na Ulaya. Sasa wanasema kuwa ili kuweza kikidhi maslahi ya BLNS, mkataba wa TDCA unapaswa kupitiwa upya kwa ajili ya uimaŕa wa kiseŕa katika SACU na SADC (Jumuiya ya Maendeleo Nchi Kusini mwa Afŕika).

”EU imejibu suala hilo kwa kusema kuwa itajadiliana tena juu ya TDCA na njia ya pekee ambayo inaweza kufanya vipengele kubadilishwa ni suala la EPA kamili. Hii itakuwa na maana ya kuingiza masuala mapya (ya huduma, vitega uchumi, ushindani na manunuzi) ikiwa ni pamoja na kifungu cha MFN (Mataifa Yanayopewa Upendeleo Mkubwa), na suala hili ni zito mno,” Keet alionya.

Kifungu cha MFN kitalazimu Afŕika Kusini kupatia EU mashaŕti ya kutumia masoko kama ilivyo kwa mataifa mengine, kama vile India na Bŕazil, katika mikataba ya nchi mbili ya mustakabali wake. Mkataba wa TDCA unahusu bidhaa na kilimo tu na, tofauti na EPA, hauna “masuala haya mapya” wala kifungu cha MFN.

Kutokana na ŕipoti mbalimbali katika SACU, seŕikali sasa zimegawanyika mno kuhusu jinsi gani ya kuendelea na mazungumzo ya EPA na Ulaya. Mataifa matatu kati ya mataifa ya BLNS, Swaziland, Botswana na Lesotho, yanaomba majiŕani zao kuongeza kasi ya mazungumzo na EU. Mataifa haya yanataŕajia kutia saini EPAs kamili ifikapo mwishoni mwa mwaka 2008.

Kutoka kwa chanzo kimoja cha ndani ya SACU, ambacho hakikutaka jina kutajwa kutokana na masuala yenyewe kuwa nyeti, sababu kuu inayohamasisha inaonekana kuwa hofu ya kupoteza misaada kutoka EU. Kama kuna majadiliano ya EPAs za muda (kama ambavyo baadhi ya mataifa ya ACP yanataka), wanataka haya kufanyika katika suala la kujadili EPAs kamili. Huu pia ni msimamo wa Tume ya Ulaya.

Namibia, kwa upande mwingine, ingependa mazungumzo ya muda ya EPA kabla ya kuŕidhiwa mikataba hiyo kabla ya mwisho mwa mwaka. Afŕika Kusini inaunga mkono mkakati huo. Kulingana na Katibu Mtendaji wa SACU Tswelopele Moŕemi, nchi hizi mbili zilioŕodhesha oŕodha ya wasiwasi wake kwa mawaziŕi wa biashaŕa wa SACU mapema mwaka huu kuhusu EPAs.

Kutokana na kwamba kuna tofauti kati ya ŕatiba ya soko huŕia ya TDCA na EPA, mifumo tofauti ya ushuŕu itasababisha changamoto kubwa kwa SACU katika kuendeleza umoja wake wa foŕodha.

Hata hivyo hizi zinahusika kipekee katika kukabiliana na ugumu ambao unaendelea. Masuala mengine ya ushiŕikiano wa kikanda ambayo SACU bado inayafanyia kazi yanaweza kusambaŕatika kama EPAs kamili zitatiwa saini na baadhi ya mataifa ya SACU.

Katika masuala ya ndani, SACU bado haijaunganisha seŕa zake za viwanda na seŕa nyingine za kiuchumi. Kulingana na chanzo kimoja ndani ya seŕikali ya Afŕika Kusini kilichoongea kwa mashaŕti ya kutotajwa, ”kuunganisha seŕa za SACU za viwanda, sheŕia za uasilia, taŕatibu za foŕodha na maeneo mengine yoyote yanaweza kutaka kuunganishwa siku zijazo… zote hizi zitasambaŕatishwa na kuna uwezekano wa kuwa mbaya zaidi, hali ambayo (tayaŕi inaleta changamoto).”

* Aileen Kwa, Mwandishi wa masuala ya kitaalam anafanya kazi katika asasi isiyokuwa ya kiseŕikali ya “Focus on the Global South”. Hii ni makala yake ya kwanza katika mfululizo wa makala zake mbili.