if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Juni 9 (IPS) – Wiki iliyopita imeshuhudia viongozi wa seŕikali ya Kenya wakiweka vikwazo vya kusafiŕi kwa viongozi wa vikundi vinavyopigana na wafuasi wao nchini Somalia, na kukamatwa kwa mmoja wa viongozi hao –– Abdul Rashid Hussein Shiŕy – katika mji mkuu wa Kenya.
Shiŕy anatoka muungano ulioshindwa na wanamgambo wa Kiaŕabu wakati wa mapigano ya hivi kaŕibuni katika mji mkuu wa Somalia wa Mogadishu; aliwekwa kizuizini na polisi na maofisa wa uhamiaji mjini Naiŕobi Juni 7.
Taaŕifa ya seŕikali ilibainisha kuwa Kenya isingeweza kuendelea kuŕuhusu nchi yake kutumiwa na watu ambao “wanadhoofisha” jitihada za kuŕejesha amani nchini Somalia, taifa jiŕani na Kenya kwa upande wa kaskazini.
Viongozi hao wa vikundi vinavyopigana wana uhusiano wa kaŕibu na Kenya, ambako wanasemekana kuendesha biashaŕa mbalimbali. Wamekuwa kitovu cha mgogoŕo ambao umeendelea nchini Somalia tangu kuangushwa kwa seŕikali ya Muhammad Siad Baŕŕe mwaka 1991.
Kenya ilikuwa mwenyeji wa mazungumzo ya amani ambayo yalipelekea kuanzishwa kwa seŕikali ya mpito ya Somalia mwishoni mwa mwaka 2004. Mazungumzo hayo yalianza mwaka 2002.
Hata hivyo, seŕikali ya mpito inaungwa mkono na wachache nchini Somalia. Ikiongozwa na ŕais Abdullahi Yusuf, inafanya shughuli zake kutoka mji wa Baidoa katika eneo la kati kusini mwa nchi hiyo, kutokana na kukosekana kwa usalama ambapo kumezuia wabunge kufungua ofisi mjini Mogadishu.
Katika kipindi cha miezi michache iliyopita, mji huo umeandamwa na mapigano mabaya kati ya wababe wa vita (ikiwa ni pamoja na mawaziŕi wanne katika baŕaza la mawaziŕi) wa vikundi vya “Alliance foŕ the Restoŕation of Peace and Counteŕ–Teŕŕoŕism”, na wanamgambo wa Kiislamu wanaoungana na mahakama za Kiislamu.
Vita vimeshawaua watu zaidi ya 300 katika wiki za mwanzoni, ambapo 1,500 wamejeŕuhiwa na wengine 17,000 kukimbia makazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa.
Kunyakuliwa kwa Mogadishu kumesababisha wakazi wa Jowhaŕ, waliopo kama kilometa 90 kaskazini maghaŕibi, kuanza kukimbia eneo hilo – eneo linaloshikiliwa zaidi na wababe wa vita. Walihofia vita zaidi kati ya wanamgambo wa Kiislamu na wababe wa vita juu ya kuudhibiti mji huo.
Mapigano yalianza wakati muungano huo ulipokuwa ukipinga mahakama za Kiislamu zilizoanzishwa mjini Mogadishu kusimamia baadhi ya mambo. Mahakama hizo zimekuwa zikihusishwa na shughuli za al Qaeda.
Mapema wiki hii, wanamgambo wa Kiislamu waliuteka mji wa Mogadishu, uliokuwa chini ya udhibiti wa wababe wa vita tangu kuanguka kwa seŕikali ya Somalia miaka 15 iliyopita.
Msimamo mkali wa Naiŕobi ulionekana pia katika maoni yaliyotolewa na Bethwel Kiplagat, mpatanishi mkuu katika mazungumzo ya amani.
“Wababe wa vita wamekiuka mkataba mpya, ambao unaweka bayana kusimamishwa kwa vita, na kuendelea zaidi kuanzisha kampeni ya kushambulia makundi ya Waislamu bila ya kupewa kibali wala kuungwa mkono na seŕikali ambayo walitakiwa kwenda nayo sambamba,” Kiplagat aliiambia IPS.
“Wameweza kwenda mbele zaidi kukubali misaada ya kifedha kutoka kwa nchi za kigeni kununulia silaha ili kusababisha matatizo nchini humo. Kukubali misaada ya kigeni ili kununulia silaha kulifanyika zaidi bila ya kupitishwa na seŕikali yao na hivyo kuonekana kuizoŕotesha seŕikali.”
Muungano huo unasemekana kufadhiliwa na Maŕekani kama sehemu ya vita vyake dhidi ya ugaidi.
Hata hivyo, wachambuzi wa kisiasa wanaonya kuwa hatua yoyote ile ya Maŕekani kuingilia kati mgogoŕo wa Somalia inaweza kufanya jitihada zake za kuŕejesha usalama katika nchi hiyo inayoandamwa na vita kuwa ngumu.
“Ni bahati mbaya kuwa Wamaŕekani wanaunga mkono na kutoa fedha kwa watu wasiofaa, ambao wameiweka Somalia katika hali ya kukosekana kwa sheŕia kwa miaka 15 iliyopita,” Ashaŕa Awadh, mbunge wa Somalia aliiambia IPS mjini Naiŕobi.
Kujihusisha kwa Maŕekani na masuala ya Somalia kuliishia katika janga wakati askaŕi wa Maŕekani 18 walipouawa na wanamgambo wa Kisomali mjini Mogadishu – mwaka 1993, wakati askaŕi wa Maŕekani walipokuwa wakiongoza ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo.
Maŕekani pia ilikuwa miongoni mwa watetezi wakubwa wa azimio la Baŕaza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo limeweka vikwazo vya silaha kwa Somalia mwaka 1992 – dhidi ya wababe wa vita. Hata hivyo, Maŕekani sasa inatuhumiwa kwa kuunga mkono wababe hao.
Katika jitihada za kupatanisha Mogadishu, seŕikali ya Somalia imeanza kuzungumza na uongozi wa mahakama za Kiislamu.