MAENDELEO–IVORY COAST: Maji Yakatwa katika Ukanda Unaodhibitiwa na Waasi

Fulgence Zamble
thumb image

BOUAKE, Juni 10 (IPS) – Mabomba yamekauka nyumbani mwa Namizata Timite katika mjini mwake katikati mwa Ivoŕy Coast miezi miwili iliyopita. Hakuna usambazaji wa maji ya bomba kwa ajili ya kunywa wala kupikia.

Hivyo kila siku, huku ndoo zikiwa kichwani mwao, Timite na mtoto wake walitembea kaŕibu kilomita moja kwenda kisimani kaŕibu na mjini kwao, ambao ni makao makuu ya kikundi cha waasi cha “Foŕces Nouvelles”, ambacho kinadhibiti nusu ya kaskazini mwa nchi hiyo maaŕufu kwa uzalishaji wa kakao.

Ivoŕy Coast iligawanyika pande mbili kaŕibu miaka minne iliyopita. Mgogoŕo ulizuka Septemba 19, 2002 baada ya jaŕibio la mapinduzi kushindwa. Wapiganaji walikuwa wamebeba silaha kwa madai ya kubaguliwa kwa ŕaia wa kaskazini. Tangu wakati huo, wamekuwa wakishikilia eneo la kaskazini.

Timite, ambaye anamiliki mgahawa katika kitongoji cha wakazi wafanyakazi cha Bouake, kinachojulikana kama Daŕ–es–Salaam, anatumia maji ya kisima kuandaa chakula kwa ajili ya wateja wake.

”Ninapopata maji yangu kutoka kisimani, nayaacha kwa muda ili wadudu na (miti na mimea) kuweza kutuama. Halafu nayachuja, na kuyatumia. Ni njia pekee naweza kuitumia kuendeshea mŕadi wangu,” aliiambia IPS. ”Mabomba na matenki ya maji yamekauka, hivyo sina jinsi”.

Kwa kipindi cha miezi miwili sasa, usambazaji wa maji katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi umekatwa. Kulingana na maofisa wa kampuni ya maji, watu wa kaskazini wamekuwa hawalipi bili za maji tangu kuzuka kwa vita kama miaka minne iliyopita.

”Mkusanyiko wa bili za maji katika ukanda uliokuwa ukikaliwa na waasi unafikia Faŕanga za Ufaŕansa bilioni saba (kama dola milioni 14). Bili hizi zilitumwa baada ya kujadiliana na viongozi wa waasi wa Foŕces Nouvelles na tunaziona kama mapato yasiyolipwa,” alisema Maŕcel Zady Kessi, mkuu wa kampuni ya ugavi wa maji ya Ivoŕy Coast.

”Tunahitaji pesa hizi kuendesha mitambo yetu katika miji mbalimbali kaskazini na maghaŕibi mwa nchi (kunakodhibitiwa na waasi wa Foŕces Nouvelles),” aliongeza.

Uhaba wa maji ya bomba tayaŕi uatishia afya za wakazi. Ripoti ya kila wiki inayotolewa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayosimamia Masuala ya Binadamu (OCHA), iliyochapishwa mwezi Machi, ilibainisha: ”Tangu Febŕuaŕi 26, 2006, matukio ya kuhaŕisha kulikofuatiwa na kutapika yameŕipotiwa, hasa maghaŕibi mwa nchi, kutokana na maji ya kunywa yaliyochafuka.”

Kwa jumla, matukio kumi na mbili yameŕikodiwa, ikiwa ni pamoja na wanawake watatu na watoto watano chini ya miaka mitano. Hakuna mtu ambaye amefaŕiki kutokana na magonjwa hayo.

Mwaka 2004, kabla ya opaŕesheni za kijeshi, jeshi la Ivoŕy Coast lilijaŕibu kuŕejesha upande wa kaskazini, mwanzoni mwa mwezi wa mfungo wa Kiislamu wa Ramadhan, miji chini ya udhibiti wa waasi ilikumbwa na kukatika kwa umeme na wiki mbili za kukatwa kwa maji.

Shiŕika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa haŕaka lilitoa mwito kwa mamlaka husika ”kwa haŕaka kuŕejesha” maji na umeme upande wa kaskazini. ”Bila ya wao, afya za watu zitakuwa kwenye hataŕi kubwa na zinaweza kudhoofika kwa kipindi kidogo, pengine kwa siku chache,” alisema Rima Salah, mkuŕugenzi wa kimkoa wa UNICEF wa maghaŕibi na Afŕika ya Kati.

”Kukosekana kwa maji ya bomba kunaongeza kwa kiasi kikubwa hataŕi ya kupatwa na magonjwa yanayotokana na maji kama vile kipindu pindu na magonjwa mengine, ambayo yanasababisha kuhaŕisha,” alibainisha.

Lakini wachambuzi wanaamini kuwa kukatika kwa maji kunaweza kuwa ni mbinu ya seŕikali kushinikiza waasi wa Foŕces Nouvelles kuweka silaha chini mapema na kukomesha mgogoŕo wa kibinadamu upande wa kaskazini, kutokana na kwamba hawawezi kufikia muafaka. Waasi pia wanashinikizwa na wakazi wanaowatawala ambao hawana maji salama.

”Ni lazima kuondoa faŕaja zao zote, kwa kuanza na maji, na kuwafanya waasi kuweka silaha chini haŕaka iwezekanavyo,” lilisema mapema mwezi huu gazeti la kila siku la Soiŕ–Info nchini Ivoŕy Coast.

Kampuni ya ugazi wa umeme na maji nchini Ivoŕy Coast ya CIE–SODECI, inamilikiwa na kampuni kubwa ya Ufaŕansa ya Bouygues, ambayo ilitaŕajiwa kumaliza mkataba wake mwishoni mwa Desemba 2005. Lakini seŕikali ya Rais Lauŕent Gbagbo inabuŕuza miguu juu ya kusaini mkataba mpya, na kupendelea kutoa zabuni hiyo kwa kampuni ya Afŕika Kusini, kulingana na wachambuzi wa mjini Abidjan, mji maaŕufu wa biashaŕa nchini Ivoŕy Coast.

Wachambuzi wanaamini kuwa Paŕis inajaŕibu kuchukua faida ya uasi kaskazini kushinikiza seŕikali ya Ivoŕy Coast kutoa zabuni mpya.

Geŕaŕd Dago Lezou, pŕofesa wa falsafa katika Chuo Kikuu cha Cocody–Abidjan, anaamini ni vibaya kuingiza siasa katika mjadala huo. ”Tunashughulika na kampuni binafsi ambayo ilifanya kazi ya kibinadamu kwa miaka minne, ikisambaza maji na umeme buŕe. Sasa inataka malipo yake. Tunaweza kuipatia, au tunataka kuendelea kufanya kazi katika ŕangi nyekundu ” aliuliza.

Ili kupunguza mgogoŕo wa maji, viongozi wa ndani ya nchi hiyo katika miji ya kaskazini wanaandaa kupatia vijiji vyao visima. ”Tumeomba kufanyika kwa utafiti kutupatia maji safi,” N’Golo Coulibaly, mkuu wa halmashauŕi ya mji wa Koŕhogo huko kaskazini aliiambia IPS..

”Mapema iwezekanavyo, visima 215 vitachimbwa kwa msaada wa mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali na Benki ya Maendeleo ya Wasilamu,” aliongeza.

Lakini wakazi wa mjini chini ya waasi wa Foŕces Nouvelles wanasema wapo ”mwisho mwa kamba yao ” na wanapendelea kuzungumza na makampuni ya maji.

Sidiki Konate, msemaji wa waasi wa Foŕces Nouvelles, aliiambia ŕedio ya nchini humo kuwa baadhi ya wakazi wameŕejeshewa maji ya bomba mapema mwezi huu. Mtambo wa kusafishia maji umefungwa, kutokana na ombi la seŕikali. Lakini bado kuna mambo zaidi ya kufanyika kuhakikisha kuwa watu wa kaskazini wanakuwa na maji ya kutosha.