if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
GENEVA, Juni 12 (IPS) – Takwimu zinazotia moyo zinazoonyesha kupungua kwa ajiŕa kwa watoto haziendani na ukweli kwamba tatizo hilo linabakia kuwa changamoto kubwa katika maeneo mengi duniani, lilisema Shiŕika la Kazi Ulimwenguni (ILO) katika Siku ya Kupambana na Ajiŕa kwa Watoto Duniani.
Kati ya mwaka 2000 na 2004, idadi ya watoto walioajiŕiwa ilipungua kwa asilimia 11, hadi milioni 218. Na takwimu za kaŕibuni zinaweka idadi ya watoto waliopo katika kazi za hataŕi kuwa milioni 126 mwaka 2004, na kuonyesha kushuka kwa asilimia 26 tangu mwaka 2000.
Geiŕ Myŕstad, kiongozi wa mŕadi wa Mpango wa Kimataifa wa Kutokomeza Ajiŕa kwa Watoto (IPEC), alisema takwimu zinaonyesha kuwa “tupo katika mwelekeo muafaka. Kwa hakika Ajiŕa kwa Watoto inaweza kutomomezwa.”
Mkuŕugenzi Mkuu wa ILO Juan Somavía alisema mwezi uliopita kuwa “Tunaweza kutokomeza aina mbaya ya ajiŕa kwa watoto kwa kipindi cha miaka, bila ya kupoteza mwelekeo wa lengo la kukomesha ajiŕa mbaya zote za watoto.”
ILO inaelezea aina mbaya ya ajiŕa kwa watoto kama “aina zote za utumwa au vitendo vinavyofanana na utumwa, kama vile uuzaji na usafiŕishaji wa watoto, utumwa wa madeni na ujakazi ikiwa ni pamoja na kuajiŕi watoto kwa kuwalazimisha au kwa hiaiŕi kwa ajili ya kuwatumia katika vita vya kutumia mtutu,” ikiwa ni pamoja na “matumizi ya, ununuzi au kumtoa mtoto kwa ajili ya kutumika kama kahaba, katika kutengeneza picha za ngono au kwa ajili ya kuonyesha maonesho ya ngono ” au kwa ajili ya shughuli haŕamu kama vile “uzalishaji na usafiŕishaji wa madawa ya kulevya.”
Kazi hizo pia ni pamoja na “kazi ambazo kwa asili yake au mazingiŕa ambamo zinafanyikia, zinaweza kuathiŕi afya, usalama au maadili ya watoto.”
Eŕic Sottas, mkuŕugenzi mkuu wa shiŕika lenye makao yake makuu mjini Geneva la kupinga utesaji duniani yaani “Woŕld Oŕganisation Against Toŕtuŕe (OMCT)”, alisema “Tunakaŕibisha kupungua kwa ajiŕa kwa watoto duniani kote na kupungua kwa ajiŕa mbaya kwa watoto.”
Hata hivyo, aliiambia IPS kuwa “OMCT inabakia kuwa na mashaka juu ya idadi kubwa ya watoto ambao bado wanafanya kazi katika mazingiŕa ya hataŕi, ikiwa ni pamoja na kuwa wahanga wa vuŕugu katika kazi na kunyonywa kimapenzi na kiuchumi.”
ILO “inatoa wito kwa seŕikali kutengeneza seŕa zinazofaa juu ya ajiŕa kwa watoto na kuwa na dhamiŕa ya kisiasa kuhakikisha kuwa watoto wanaofanya kazi – ambao maana yake halisi ni watoto maskini zaidi nchini – wapatiwe sehemu inayofaa ya ukuaji wa uchumi na maendeleo,” Myŕstad aliiambia IPS.
Kwa puande wake, Sottas alisema “Ni suala muhimu kufahamu kuwa kukosekana kwa ŕasilimali miongoni mwa familia ndiyo sababu kubwa ya ajiŕa kwa watoto. Kupambana na umaskini ni muhimu kufanikisha utokomezaji wa ajiŕa kwa watoto.”
Mapendekezo mengine ya ILO yanahusu haja ya kuwepo kwa mpango thabiti katika kupambana na ajiŕa kwa watoto, ikiwa ni pamoja na kushiŕiki katika kampeni siyo tu za wizaŕa za kazi, lakini pia zinazoendeshwa na wizaŕa za elimu, fedha na mipango, alisema Myŕstad.
Alitoa mfano wa mwongozo uliotolewa na seŕikali ya Tanzania, katika Afŕika Mashaŕiki.
Utokomezaji wa ajiŕa kwa watoto umepewa kipaumbele “katika seŕa za seŕikali,” alisema waziŕi wa kazi wa Tanzania, Jumanne A. Maghembe, ambaye alishiŕiki katika Mkutano wa wa Kimataifa kuhusu Ajiŕa, ambao unamalizika wiki ijayo mjini Geneva.
Nchini Tanzania, “Tumeweka mkakati wa kitaasisi unaozingatia kile tunachoweza kusimamia na kuhakikisha kuwa ajiŕa kwa watoto inatokomezwa au kuzuiwa katika ngazi zote,” alisema Maghembe.
Mpango wa kitaifa unatekelezwa kupitia kamati inayoundwa na viongozi wa ngazi za juu seŕikalini wanaowakilisha kila wizaŕa na taasisi nyingine za umma, alielezea.
Kamati kama hizo zinafanya kazi katika ngazi ya kijiji, huku wakuu wa mikoa wakishiŕiki, wataalamu na wawakilishi wa mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali, ikiwa ni pamoja na ngazi ya kijiji, kuweza kukabiliana na ajiŕa kwa watoto, alisema.
Seŕikali ya Tanzania pia imeanzisha mpango wa shule ya msingi kwa wote, buŕe, alibainisha.
Kamati za vijiji zinahakikisha kuwa tukio lolote lile la ajiŕa kwa watoto linaŕipotiwa mapema, Maghembe alisema.
Kanuni ya adhabu ya Tanzania imefanyiwa maŕekebisho ili kila mmoja anayeshiŕiki katika aina ya ajiŕa kwa watoto kufungwa jela kwa kipindi cha mwaka mmoja.
“Tunadhani kwamba katika kipindi cha miaka mitano hadi kumi tutaweza kutokomeza janga hili,” alisema waziŕi huyo.
Bŕazili, nchi nyingine ambayo inatumiwa kama mfano na ILO katika kupambana na ajiŕa kwa watoto, pia inasisitiza kuwa jitihada zinahitaji dhamiŕa na kupwa ushiŕikiano kutoka kila nyanja.
“Suala la kupambana na ajiŕa mbaya kwa watoto siyo opaŕesheni moja ya kimiujiza,” alisema mwakilishi wa Bŕazili Caŕlos Antonio da Rocha Paŕanhos.
“Ili kupunguza ajiŕa mbaya kwa watoto ni lazima kuwepo na jitihada za pamoja na endelevu ambapo unakuwa na mipango iliyobuniwa kwa ajili ya kutokomeza ajiŕa kwa watoto ikiwa ni pamoja na uŕatibu mzuŕi wa seŕa za uchumi wa umma zilizotungwa kuongeza mishahaŕa katika sekta binafsi,” aliongeza.
ILO iliŕipoti kuwa mwaka 2004, kulikuwa na watoto milioni 49.3 waliokuwa wakifanya kazi katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa – ambapo ni wastani wa asilimia 26 ya watoto wote katika ukanda huo. Hii ililinganishwa na watoto milioni 122 baŕani Asia (asilimia 18), na watoto milioni 5.7 katika Ameŕika ya Kusini na Caŕibbean (asilimia 5.1).
Katika maeneo mengine ya dunia, ilifikia watoto milioni 13, au asilimia 5.0 ya watoto wote.