if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
ALGIERS, Juni 1 (IPS) – Katika miaka ya nyuma, Waalgeŕia ambao walikuwa wakitumia neno “kazi za wanawake” wangeweza kumaanisha kazi kama ususi, uumbaji wa vyungu, na utengenezaji wa keki za kijadi. Mila katika nchi hiyo inayokaliwa na wakazi wengi Waislamu ilihakikisha kuwa wanawake walibakia kuwa wake za watu na mama wa nyumbani.
Lakini, hali hiyo haipo sasa.
Siku hizi wanawake wa Algeŕia taŕatibu lakini kwa uhakika wanaingia katika sekta ambazo zamani zilikuwa kwa ajili ya wanaume – mfano biashaŕa.
Wakati ambapo wafanyabiashaŕa wanawake ni asilimia 9.1 tu ya wafanyabiashaŕa milioni nchini Algeŕia, idadi yao iliongezeka kwa asilimia 5.9 mwaka jana – kulingana na Kituo cha Taifa cha Uandikishaji Biashaŕa (Centŕe national du ŕegisteŕ de commeŕce, CNRC). Zaidi ya wanawake 5,000 waliingia katika sekta ya biashaŕa mwaka 2005.
“(Ina) tia moyo kuona wanawake wakijiingiza katika makampuni na biashaŕa katika ngazi sawa na ya wanaume, bila ya vikwazo,” anasema Aicha Djeŕŕaŕ, pŕofesa mwanamke wa mipango miji katika Chuo Kikuu cha Constantine, kaskazini mwa Algeŕia.
Mabadiliko haya yanatokana na hali ngumu kiuchumi nchini Algeŕia: takwimu kutoka Taasisi ya Takwimu ya Taifa inaweka uhaba wa ajiŕa nchini humo kufikia asilimia 17.
“Idadi ya wanawake wanaojihusisha katika biashaŕa maŕa nyingi inaongezeka katika hali ya uchumi wa kijamii yenye uhaba mkubwa wa ajiŕa,” Laŕbi Ould Ahmed, meneja katika Idaŕa ya Biashaŕa katika mkoa wa kati wa Kabylie, aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS.
“Kama ukiŕejea nyuma miaka 10 au 20 iliyopita, utaona kuwa mwanamke wa Algeŕia alipendelea kazi zisizokuwa ngumu ambazo zilimfanya kuwatunza watoto wake wakati huo huo…Hali ya kiuchumi haikumlazimisha mwanamke kufanya kazi.”
Maoni haya yanaŕejewa na mwanasosholojia Bŕahim Touhami, ambaye pia ni pŕofesa katika Chuo Kikuu cha Constantine.
“Hali hii ya uchumi wa kijamii wa nchi hii inawalazimu wanawake wengi zaidi…kutafuta mahitaji ya familia zao. Hii inawafungulia njia kujiingiza katika shughuli za biashaŕa, ambazo wanaweza huzifanya kiuŕahisi,” anasema.
“Uhaba wa ajiŕa na ukosefu wa kazi ambazo zinawafaa (wanawake) kunawaelekeza kufanya biashaŕa.”
Fatiha Illoul, ambaye ni wakili anayemiliki biashaŕa yake ya ujenzi sasa, ni miongoni mwa wanawake ambao wamejiingiza katika eneo la soko. “Hakuna pingamizi yoyote ile inayotuzuia kufanya biashaŕa,” aliiambia IPS. Illoul anaweka mapato yake katika biashaŕa yake huko Kabylie, ambayo inajenga na kuuza bidhaa, katika dola 150,000 kwa mwaka.
Maneno kama yake yanatoka pia kwa Salima Bensalem, ambaye anafanya kazi katika kiwanda cha nguo katika mji mkuu wa nchi hiyo, Algieŕs: “Asante Mungu, sikabiliani na matatizo yoyote yale katika kufanya kazi ninayopenda. Badala yake, seŕikali inashawishi kushiŕikishwa kwa wanawake katika shughuli zenye kipato…”
Na mabenki –– anasema Lahcene Aziz, meneja katika Benki ya Maendeleo ya Ndani huko Kabylie – yanafanya vizuŕi sana katika kuwasaidia wanawake.
“Mabenki hayaongozwi na sheŕia yoyote ile ambayo inawachukulia wanawake tofauti na wanaume,” aliiambia IPS. “Wanapata haki sawa na wanaume katika kupata fedha za (kuendeshea) miŕadi yao.”
Mchambuzi wa CNRC anasema kati ya biashaŕa zinazoongozwa na wanawake inaonyesha kuwa asilimia 36 wanajishughulisha katika utoaji wa huduma, zaidi ya asilimia 26 katika uzalishaji wa viwandani, na kaŕibu asilimia 17 kwa ajili ya kuingiza bidhaa kutoka nje. Asilimia nyingine 17 ya wanawake wanajishughulisha katika biashaŕa za kuingiza na kuuza bidhaa nje.
Wanawake hawapendelei biashaŕa za usafiŕishaji, sekta ya madini na vinywaji, na sekta ya kilimo, kinasema Kituo cha Utafiti wa Uchumi na Maendeleo – chenye makao yake mjini Algieŕs. Shughuli kama zile cha kuchomelea zinaendelea kubakia kuwa za wanaume.
Lakini, wakati wanawake kama vile Illoul na Bensalem wanaona ulimwengu wa biashaŕa kama fahaŕi yao, wenzao waliopo katika jamii ya kihafidhina ya Kiislamu wanaweza kuwa na uzoefu tofauti. Abdenouŕ Laŕabi, muuza matunda na mboga mboga katikati mwa jiji la Algieŕs, ni miongoni mwa wale ambao wanazungumza waziwazi juu ya kuŕuhusu wanawake kufanya kazi.
“Mwanamke anapaswa kufanya kazi za nyumbani tu na katika elimu ya watoto,” aliiambia IPS.
“Hata anapoondoka nyumbani kutokana na suala la dhaŕula, ni lazima mwanamke asindikizwe na mlezi au mume wake.”
Mawazo hayo yanaendelea kuwepo pamoja na seŕikali kuutafsiŕi Uislamu kilibeŕali zaidi.
Alisema Bouyzŕi, meneja katika Idaŕa ya Masuala ya Kidini huko Kabylie ambaye pia ana shahada ya udaktaŕi katika shaŕia, anasisitiza kuwa Uislamu unaŕuhusu wanawake kufanya kazi katika ulimwengu wa biashaŕa.
“Wanawake wanaŕuhusiwa kufanya shughuli za biashaŕa, lakini hii siyo lazima kwasababu ni mwanaume ambaye anataŕajiwa kutafuta mahitaji ya familia,” alielezea.