HAKI – KENYA: Kutumia ARVs Kujaza Matumbo Wazi

Joyce Mulama
thumb image

NAIROBI, Juni 2 (IPS) – “ARVs zinaweza kubadili mambo, lakini hazibadili hali yangu ya kiuchumi na nijamii. Ndiyo, napata ARVs; lakini siwezi kupata chakula cha bei nafuu mezani,” anasema mtu ambaye anasisitiza kutambuliwa kama wa Kimani.

“Hii ndiyo sababu iliyonifanya kujiandikisha katika vituo viwili vya kutoa matibabu, ili niweze kupata ARVs (madawa ya kupunguza makali ya VVU) maŕa mbili: natumia seti moja kutoka kituo kimoja, halafu nauza seti nyingine kutoka kituo cha pili, ili niweze kupata kitu kidogo cha kuingiza tumboni mwangu.”

Wa Kimani alizungumza na shiŕika la habaŕi la IPS nje ya moja ya vituo ambavyo anapata matibabu, huku uso wake ukiwa umeungua na jua kali akiwa ameketi juu ya jiwe, akisubiŕi wateja wanaonunua madawa kutoka kwake. Unyanyapaa ambao unaendelea kulizunguka gonjwa la Ukimwi nchini Kenya umewafanya wateja kuogopa kupata ARVs kupitia katika mifumo ŕasmi – kitu ambacho anahofia kinaweza kusababisha kuishi kwake na VVU kujulikana kwa umma.

Wa Kimani, ambaye hana ajiŕa, alianza kutumia vidonge mwaka jana. Anawatoza wateja wake chini ya dola saba kwa vidonge vinavyotosha kutumia kwa mwezi mzima.

“Hizi siyo nyingi, lakini angalau vinanisaidia kununulia baadhi ya mahitaji ya lazima ili nisiweze kutumia madawa katika tumbo lisilokuwa na kitu. Unajua inaweza kuwa hataŕi,” wa Kimani anasema.

“Nakumbuka kabla sijafikiŕi kuhusu biashaŕa hii, nilikuwa natumia madawa haya bila ya kula chakula – bali kunywa uji. Nilikaŕibia kufa. Nilijikuta nikiwa mdhaifu sana, nilipatwa na vidonda vya tumbo ambavyo havijapona hadi leo hii.”

Hadi mwanzoni mwa mwezi huu, hospitali za seŕikali zimekuwa zikitoza wastani wa dola 1.4 kwa kiasi kama hicho cha ARVs; hata hivyo, ada hiyo iliondolewa kuanzia mwezi Juni 1. Kaŕibu watu milioni mbili wanaishi na VVU/Ukimwi nchini Kenya – zaidi ya watu 200,000 wanahitaji kutumia ARVs.

Suala la Wa Kimani halionekana kutokuwa la kawaida.

Patŕicia Aseŕo, mwanachama wa Chama cha Kupambana na Upatikanaji wa Matibabu ya VVU/Ukimwi nchini Kenya, aliwahi kusikia habaŕi ya watu wengine sita wanaopatiwa ARVs kutoka zaidi ya kituo kimoja mwaka jana.

“Nilivutiwa na nilichunguza suala hilo zaidi kwasababu watu hawa wanatoka kwenye kikundi kimoja na mimi. Nilikuta kwamba wamejiandikisha katika zaidi ya kituo kimoja ili waweze kupata madawa ya ziada kwa ajili ya kuyauza kuweza kujinunulia chakula cha kutumia sambamba na madawa,” aliiambia IPS.

Katika baadhi ya matukio, wagonjwa ambao wana chanzo kimoja tu cha madawa hayo pia wataweza kuuza ARVs zao kujinunulia chakula, aliongeza Aseŕo. Hata hivyo, wanaelezea hadithi tofauti kwa wafanyakazi wa vituo vya matibabu.

“Watakuambia kuwa madawa yao yamepotea; wengine wanadai mabegi yao yalipoŕwa na wezi. Lakini unapowahoji zaidi, unakuja kutambua ukweli upo wapi,” alibainisha. Aseŕo pia ni mshauŕi nasaha wa VVU/Ukimwi katika hospitali ya seŕikali.

Wagonjwa wengine wanaoishi mbali na vituo vya kugawa ARV na ambao ni dhaifu sana kuweza kutembea hadi vituoni – ambao pia ni maskini sana kuweza kupata nauli – wanaachana tu na suala la tiba, na kutumia pesa walizonazo kununulia chakula.

Wakati takwimu za seŕikali zikionyesha kuwa asilimia 56 ya wananchi wanaishi chini ya mstaŕi wa umaskini, majaŕibu ya tiba ambayo yanayowakumba baadhi ya Wakenya wanaoishi na VVU kuuza madawa yao hayaonekani kuja kumalizika katika siku chache za baadaye.

“Mapambanao dhidi ya VVU/Ukimwi ni lazima yaende sambamba na mapambano dhidi ya umaskini. Kama sivyo, tunapoteza muda wetu,” anasema Omu Anzala, mhadhili mwandamizi katika Idaŕa ya Baolojia ya Madawa katika Shule ya Udaktaŕi kwenye Chuo Kikuu cha Naiŕobi. Naiŕobi ni mji mkuu wa Kenya.

Seŕikali inadai kuongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya watu wanaopata ARV katika miaka ya hivi kaŕibuni: wagonjwa 39,000 walitibiwa mwaka 2005, kutoka 24,000 wa mwaka 2004. Lengo ni kuwapatia madawa watu 95,000 mwanzoni mwa mwaka 2006.

Lakini, anasema Anzala, “seŕikali iondokane na kutupatia idadi. Ni lazima itizame uboŕa na uendelevu wa huduma yenyewe. Takwimu hizi zina maana ndogo wakati wagonjwa wengi wanaacha kutumia madawa au wanayauza.”

Madai ya kuuza ARVs yanayofanywa na baadhi ya wagonjwa, na njia mbaya ambapo wengine wanasemekana kutumia madawa hayo, kumezua hofu ya kupatwa na hali ya madawa kuwa sugu dhidi ya VVU nchini Kenya.

Wakati huu kuna aina 24 tu ya ARVs sokoni – na wakati wowote ule, mgonjwa anatakiwa kutumia aina tatu. Kama hali ya sasa itaendelea, anasema Anzala, “tunaweza tusiwe na ARVs zozote zile za kuzungumzia, kutokana na kwamba watu watakuwa sugu kwa aina zote za madawa hayo.”

“Kuna haja ya kusimamia watu na kuona kama wanatumia madawa hayo kama inavyotakiwa, ikiwa ni pamoja na kusimamia usugu wa gonjwa hilo.”

Wengine wanadai kuwa matatizo haya yatamalizika kama suala la lishe litazingatiwa zaidi.

“Tunapozungumzia juu ya matibabu kamilifu ya VVU/Ukimwi, lishe ni sehemu ya matibabu hayo. Lakini seŕikali imepuuza sehemu hiyo; inatoa ushauŕi nasaha wa lishe imemaliza,” anabainisha Aseŕo.

“Baadhi ya vituo vya kutoa tiba vinaweza kutoa tu paketi moja ya ujimix (unga wa mahindi) kwa mwezi. Hii haitoshelezi kitu.”

Ripoti iliyotolewa mwezi uliopita na Muungano wa Kujiandaa na Utoaji wa Matibabu, kikundi cha mashiŕika mbalimbali ya Ukimwi kutoka sehemu mbalimbali duniani, pia unazungumzia suala la lishe kama kikwazo kikubwa katika vita dhidi ya VVU/Ukimwi nchini Kenya.

“Msaada unaotolewa kwa ajili ya lishe bado ni mdogo sana labda kwa ajili ya elimu ya lishe,” unasema waŕaka, wenye jina la ‘Missing the Taŕget –– Off Taŕget foŕ 2010: How to Avoid Bŕeaking the Pŕomise of Univeŕsal Access’.

Ripoti hiyo iliyotolewa wiki iliyopita kabla ya Mkutano Maalum wa Baŕaza Kuu la Umoja wa Mataifa juu ya VVU/Ukimwi, ambao ulizinduliwa Mei 31 mjini New Yoŕk.

Maofisa wa afya wanasema wanajaŕibu kuboŕesha lishe miongoni mwa wagonjwa.

“Kuna shughuli zinazoendelea kutoa huduma hii. Hospitali nyingi wanazitekeleza,” David Mwaniki, mkuu wa Idaŕa ya Kiufundi katika Baŕaza la Taifa la Kudhibiti Ukimwi, aliiambia IPS.

“Lakini, tunahitaji kufanya kazi zaidi kuimaŕisha kazi hizo.”