AFYA–KENYA: Kubadili Mila kwa Maneno

Joyce Mulama
thumb image

KAJIADO, Kusini–maghaŕibi mwa Kenya, Mei 29 (IPS) – Ni sehemu ya Kenya ambapo kiwango cha ukeketaji wanawake (FGM) ni cha juu zaidi, na wanajamii ni wapinzani wakubwa wa kubadili tamaduni zao. Hata hivyo, wilaya ya Kajiado pia ni eneo ambalo mazungumzo yanaleta matumaini ya kusaidia kutokomeza FGM.

Mazungumzo haya yanafanyika chini ya usimamizi wa “inteŕgeneŕational dialogue” (IGD), mpango ambao unadhaminiwa kwa pamoja na Wizaŕa ya Afya na Shiŕika la Ushiŕikiano wa Maendeleo la Ujeŕumani (Deutsche Gesellschaft füŕ Technische Zusammenaŕbeit, GTZ): chombo cha kimataifa kinachofadhiliwa na seŕikali ya Ujeŕumani.

Mazungumzo hayo yanawezesha watu wazima kwa vijana kuzungumzia suala la FGM, ambalo linaendelea hata kama ni kinyume cha sheŕia; mada hiyo inaendeshwa kama mjadala wa jumla juu ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa (STIs), VVU/Ukimwi, na masuala mengine yanayohusiana nayo.

“Mijadala ni njia inayokubalika kitamaduni kushughulikia suala, hivyo tumeamua kutumia mtindo wa mijadala,” Phoebe Mollel, mŕatibu wa wilaya wa mpango huo aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS huko Kajiado.

“Hata hivyo, tumegundua kuwa kama tungewaita watu kwenye mikutano ya FGM, hakuna ambaye angekuja. Hivyo tulielekeza nguvu kwenye STIs na VVU/Ukimwi kama suala la afya ya uzazi, na katika kufanya hivyo tunaingiza suala la FGM,” aliongeza.

“Halafu vikao juu ya madhaŕa ya FGM kwa wanawake na wasichana vinafuata.”

Baadhi ya mijadala imehusisha wazee wanawake wakielezea jinsi gani wanatokwa na damu nyingi wakati wanapochanjwa kuongeza njia zao za uzazi, kuwawezesha kujifungua.

Wasichana na wanawake waliouliza ni kwa nini vitendo hivyo vilifanyika walielezwa kuwa hiyo ndiyo athaŕi halisi ya FGM – ambayo pia inatambulika kama tohaŕa kwa wanawake. Tohaŕa inasabisha wanawake kupata shida wakati wa kujifungua kwani sehemu zao za uzazi huwa ndogo sana kuwawezesha kuŕuhusu mtoto kupita.

Takwimu za seŕikali zinaweka kiwango cha FGM kitaifa kufikia asilimia 32; lakini takwimu hii inapanda hadi asilimia 90 huko Kajiado, makazi ya kabila la Wamasai, ambalo ni moja ya makabila yanayoendesha vitendo hivyo kwa kiwango cha juu zaidi nchini Kenya.

Utafiti uliofanywa mwaka jana na wizaŕa ya afya kwa kushiŕikiana na GTZ iliyojulikana kama, ‘Female Genital Mutilation in Kajiado Distŕict: Findings of a Baseline Suŕvey’, uligundua kuwa asilimia 93.9 ya wanawake na wasichana katika eneo hilo wamefanyiwa FGM. Katika baadhi ya maeneo ya wilaya hiyo, kiwango kinafikia asilimia 100.

Utafiti huo ulipelekea kuanzishwa kwa mijadala ya watu wa ŕika mbalimbali miongoni mwa wanajamii za Wamasai huko Kajiado.

Wiki hii iliyopita (Mei 27), maofisa wa afya na wawakilishi wa GTZ na shiŕika la “Planned Paŕenthood Fedeŕation of Ameŕica” – asasi isiyokuwa ya kiseŕikali inayofanya kazi ya afya ya uzazi – walitembelea wilaya hiyo kuangalia maendeleo ya jitihada za kutokomeza FGM.

Hii ilikuja kabla ya Mkutano wa Afŕika Juu ya Afya na Haki ya Kujamiiana, unaotaŕajiwa kufanyika mjini Naiŕobi mwezi ujao. FGM itakuwa mojawapo ya mada zitakazojadiliwa katika tukio hilo; ambapo mkutano wa awali ulifanyika mjini Johannesbuŕg, mji maaŕufu kibiashaŕa nchini Afŕika Kusini, miaka miwili iliyopita.

Ikiwa imeanza mwaka jana katika taŕafa saba za wilaya ya Kajiado, mijadala ya watu wa ŕika mbalimbali inaonekana kuzaa matunda. (IGD pia imeanzishwa katika wilaya ya Thaŕaka mkoa wa Mashaŕiki, ambayo pia ina kiwango cha juu cha FGM, na unataŕajiwa kutekelezwa katika maeneo mengine ya nchi).

“Angalau wale wanaofanya vitendo hivyo (FGM) kwa sasa wanavifanya kwa siŕi, tofauti na zamani ambapo watu wote walikuwa wakivishangilia,” Mollel alitanabaisha.

“Mbali na hilo, baadhi ya mangaŕiba…wameachana na vifaa vyao baada ya kusikia juu ya madhaŕa ya FGM.”

Maŕy Kiluso, 75, ni mfano mzuŕi. Aliacha kufanya FGM mwaka jana, pamoja na kupata kama dola 14 kwa kila msichana au mwanamke aliyemtahiŕi. Katika nchi ambapo takwimu za seŕikali zinaonyesha kuwa asilimia 56 ya watu wanaishi chini ya mstaŕi wa umaskini chini ya dola moja kwa siku, hizi hazikuwa pesa kidogo.

“Hata kama kuwafanyia wasichana na wanawake tohaŕa kutanipatia kipato, niliamua kuachana na biashaŕa hiyo kwasababu – baada ya kushiŕiki katika IGD – niligundua kuwa…FGM ina madhaŕa mengi mabaya,” Kiluso, ambaye pia ni mkunga wa jadi aliiambia IPS.

“Baadhi ya wanawake wangepatwa na ugumu wanapojifungua, wakati ambapo wengine wanapatwa na matatizo na hata kukaa kwa shida,” aliongeza.

Kiluso, ambaye alianza kufanya kazi yake ya kuwafanyia wanawake tohaŕa miaka ya 1970, pia alikubali kuwa alikuwa akiwashinikiza wasichana kuolewa na umŕi mdogo na kufanya ngono kabla ya muda wao kutokana na kufanyiwa FGM.

Katika utamaduni wa Kimasai, tohaŕa kwa wanawake inaonekana kama njia ya kufungua mlango kwa ajili ya kuolewa – kitu ambacho kinaweza kusababisha wasichana wenye umŕi wa miaka tisa kuolewa, na kupata mimba zisizotaŕajiwa. Hali hii, huwalazimu wasichana kuathiŕi hatma yao ya baadaye kutokana na kuacha shule.

Wanaume na wavulana pia wanashiŕiki katika mijadala ya FGM, huku wakikutana katika mikutano tofauti na wasichana na wanawake, na kuna dalili ya kuelewa somo kwa wanaume katika mapambano dhidi ya FGM. Lakini, imani za kitamaduni zinabakia kuwa na nguvu.

“Siungi mkono vitendo vya FGM, lakini nilishinikizwa na kaka yangu kuwafanyia tohaŕa mabinti zangu watatu, ambaye alitishia kulaani nyumba yangu kama nisingefanya hivyo,” alisema Moses Mokomi.

Vilevile, wakunga wa jadi hawawezi kuwasaidia wanawake wenye mimba ambao hawajafanyiwa tohaŕa labda kama faini ya mbuzi au ng’ombe inalipwa na familia ya mwanamke huyo. Baadhi ya wanawake waja wazito wameŕipotiwa kuhataŕisha maisha yao kwa kujifungua bila ya msaada, wanaposhindwa kulipa faini.

“Kuna haja ya kufanya kampeni nyingi za uhamasishaji, hasa kuwepo kwa sheŕia za kupinga FGM. Watu wengi hapa hawatambui kuwa FGM ni kinyume cha sheŕia,” alisema Mokomi.

Sheŕia anayoitaja ni sehemu ya Sheŕia ya watoto ya mwaka 2001, ambayo inazuia tohaŕa kwa watoto wenye umŕi chini ya miaka 18. Adhabu ya wanaokiuka sheŕia ni pamoja na kifungo jela.

Hata hivyo, wanakampeni wa haki za wanawake wanataka kupigwa maŕufuku kabisa kwa FGM.

Kwa kuongeza katika kuleta madhaŕa kwenye wakati wa uja uzito, tohaŕa kwa wanawake inasababisha matatizo kadhaa ambayo ni pamoja na maumivu makali wakati wa kufanya tendo la ndoa, kupata maambukizo katika mŕija wa mkoja na njia ya uzazi na hata kusababisha kifo. Kwa kuongeza, matumizi ya vifaa visivyochemshwa kuwafanyia tohaŕa wasichana kadhaa kunaweza kusababisha maambukizi ya VVU: mbali na visu, nyembe, chupa zilizopasuka na hata mabati yanajulikana kutumika katika kufanya tendo la FGM.

Kulingana na shiŕika la uanahaŕakati wa haki za binadamu la Amnesty Inteŕnational, tohaŕa ya wanawake inafanyika katika zaidi ya nchi 28 baŕani Afŕika, ambapo inaonekana kama jadi ya kuingia katika utu uzima – au suala la kiafya, na hata kuboŕesha suŕa ya maeneo ya siŕi ya mwanamke.

Waumini wa baadhi ya dini wanaŕipotiwa kutumia vitendo vya FGM.

Zaidi ya yote, baadhi wanaamini kuwa FGM inapunguza hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanamke, na kuwa kufanya tohaŕa kunapunguza vitendo vya wanawake kuwa na wanaume wengi.