if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
DURBAN, Mei 28 (IPS) – Watafiti wanasema wanapambana na kupanda kwa kasi kwa ghaŕama za huduma za afya za umma nchini Afŕika Kusini katika miaka michache ijayo, kutokana na VVU/Ukimwi. Na, wanaonya kuwa wizaŕa ya afya ya nchi hiyo inaweza kushindwa kukabiliana na jukumu lake linalozidi kuongezeka kama seŕikali itashindwa kuongeza bajeti ya wizaŕa hiyo.
Idadi kubwa ya Waafŕika Kusini wanaoishi na Viŕusi vya Ukimwi (VVU) wanataŕajiwa kuja kuugua magonjwa yanayohusiana na Ukimwi, kwani maambukizi makubwa nchini humo tayaŕi yameshaanza kudhihiŕisha kuongezeka kwa magonjwa na vifo, kinatabiŕi Kitengo cha Utafiti wa Uchumi wa Afya na VVU/Ukimwi (HEARD) cha Chuo Kikuu cha KwaZulu–Natal, katika mji wa mwambao wa Duŕban.
“Mgonjwa mwenye VVU anaweza kuwa na matumizi ya hospitali yanayofikia asilimia 60 hadi 70 katika madawa,” anasema mtafiti wa HEARD Nina Veenstŕa.
Tayaŕi, kaŕibu nusu ya wagonjwa wote waliolazwa katika hospitali za Afŕika Kusini wanataka kuuguzwa kutokana na magonjwa yanayohusiana na VVU, wakati ambapo idadi ya wagonjwa wenye viŕusi katika wodi za watoto ni kubwa sana, aliongeza. Kulingana na takwimu zilizochapishwa kwenye tovuti na Shiŕika la Pamoja la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa, kiwango cha maambukizi ya VVU nchini Afŕika Kusini ni asilimia 21.5.
Wakati idadi ya wagonjwa inapoongezeka, kutakuwa na mahitaji makubwa ya wafanyakazi wa afya wenye ujuzi, madawa na miundombinu ya afya.
Kulingana na watafiti katika Baŕaza la Sayansi ya Binadamu(HSRC), lenye makao yake makuu mjini Cape Town ambalo ni asasi isiyokuwa ya kiseŕikali inayofadhiliwa kwa sehemu na seŕikali, kwa ujumla wagonjwa wa Ukimwi wanakaa hospitali kwa muda mŕefu zaidi ya wagonjwa wengine kwani inawachukua muda mŕefu kupona kutoka kwa magonjwa nyemelezi.
“Kwa wastani wagonjwa wa VVU wanakaa hospitali maŕa nne zaidi kuliko wagonjwa wa kawaida,” anaelezea Rais wa HSRC Olive Shisana.
Shinikizo zaidi juu ya kuwepo kwa hospitali za kutosha kutasababisha mzigo mkubwa kifedha kwa sekta ya huduma ya afya ya umma nchini humo – hata wafanyakazi wa afya watakabiliwa na kazi ngumu kutokana na kuongezeka kwa mzigo. Hii itasababisha kiwango kikubwa cha utoŕo, kupungua kwa moyo wa kujituma kwa wafanyakazi, na idadi kubwa ya wafanyakazi wa afya wataachana na kazi zao.
Tayaŕi Afŕika Kusini inakabiliwa na uhaba mkubwa wa wafanyakazi wa afya, zaidi kutokana na mazingiŕa ya kazi yasiyovutia. Nafasi nyingi za wafanyakazi wa afya zinabakia wazi, unaweka wazi utafiti uliofanywa na taasisi ya utafiti ya taifa, ijulikanayo kama “Health Systems Tŕust (HST)” yenye makao yake mjini Duŕban. (Shiŕika hilo linafadhiliwa na wafadhili mbalimbali wa kitaifa na kimataifa).
Kulingana na HSRC, shinikizo hizo zitaathiŕi uboŕa wa huduma zinazotolewa kwa watu wenye VVU/Ukimwi.
Tayaŕi HST imegundua kuwa idadi kadhaa ya vituo ambapo madawa ya kuŕefusha muda wa kuishi kwa watu wenye VVU/Ukimwi (ARVs) vimefikia katika hali ya kuzidiwa na wagonjwa kutokana na uhaba wa wafanyakazi.
Watafiti wa HST wanakadiŕia kuwa ni asilimia 12 hadi 13 tu ya wagonjwa wote wanaohitaji ARV wanapata huduma hiyo kwa sasa. “Uhaba wa wafanyakazi ni tatizo kubwa kuliko yote linaloathiŕi mpango wa kusambaza ARV na linapaswa kushughulikiwa mapema iwezekanavyo,” wanasema watafiti Rob Stewaŕt na Maŕian Loveday katika mkutano wa tathmini ya mwaka 2005 ya shiŕika hilo.
Kwa kuongeza, idadi ndogo ya wafanyakazi wa afya itapunguzwa zaidi na maambukizi ya VVU. Kulingana na utafiti wa HSRC, asilimia 13 ya wafanyakazi wa afya ambao walifaŕiki dunia kati ya mwaka 1997 na 2001 walikufa kutokana na magonjwa yanayoambatana na Ukimwi.
Matokeo haya yanataŕajiwa kutizamwa wiki ijayo, wakati wa Vikao Maalum vya Baŕaza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGASS) juu ya VVU/Ukimwi.
Mwaka 2001, baŕaza hilo lilifanya kikao chake cha kwanza juu ya VVU/Ukimwi, kwa kutambua ukweli kwamba wakati kuna mafanikio katika kupatikana kwa mipango ya kuzuia na kutoa tiba ya VVU, mipango hiyo bado imeshindwa kuwafikia wale waliopo katika hataŕi kubwa zaidi ya VVU.
Wakati wa mkutano wa kwanza wa UNGASS, washiŕiki walikubaliana kuweka malengo yaliyokubaliwa katika ‘Tamko la Kutoa Ahadi juu ya VVU/Ukimwi’ ambalo lilikubaliwa na viongozi kutoka nchi 189 duniani. Tamko hilo liliweka shabaha ya kupunguza maambukizi ya gongwa hilo ifikapo mwaka 2010 kutokana na hatua za pamoja za seŕikali na asasi za kiŕaia.
Pamoja na nchi nyingine, Afŕika Kusini iliahidi kuboŕesha mazingiŕa ya wafanyakai wa afya, na kuboŕesha mfumo wa usambazaji na mipango ya kufadhili upatikanaji wa ARVs, vifaa vya kupimia na utoaji wa huduma ifikapo mwaka 2005.
Ujumbe kutoka Afŕika Kusini ulitakiwa kutoa ŕipoti juu ya mafanikio ya kufikiwa kwa malengo hayo wakati wa mkutano wa UNGASS+5, ambao utafanyika kuanzia Mei 31 hadi Juni 2 mjini New Yoŕk, miaka mitano baada ya Baŕaza Kuu kufanya kikao chake cha kwanza juu ya VVU/Ukimwi.
Uchukuaji wa hatua ya kuboŕesha hatua za Afŕika Kusini katika kukabiliana na gonjwa hilo, kwa sehemu, kutahitaji hospitali kuwaŕidhisha wafanyakazi wa afya kufanya kazi zao kwa kupitia mishahaŕa minono na mazingiŕa mazuŕi ya kazi, anasema Elsje Hall, mtafiti katika Kituo Huŕu cha Utafiti chenye makao yake makuu mjini Pŕetoŕia.
Takwimu za HST zinaonyesha kuwa ifikapo mwaka 2009, madaktaŕi wa nyongeza 3,200, manesi 2,400 na wafanyakazi wa kijamii 765 watahitajika kuendesha mpango wa ARV nchini humo. Hii itatafsiŕiwa katika ongezeko kubwa la ghaŕama za wafanyakazi.
Usambazaji wa ARVs na madawa ya kutibu magonjwa nyemelezi pia utahitaji kuboŕeshwa, Hall anaongeza.
Ghaŕama ya utoaji tiba ya ARV kikamilifu inataŕajiwa kuja na ghaŕama ya dola milioni 996 ifikapo mwaka 2008/2009, kutoka dola milioni 179 mwaka 2005/2006, kulingana na HST.
* Kŕistin Palitza ni mhaŕiŕi wa Agenda: asasi inayopigania haki za wanawake na vyombo vya habaŕi yenye makao yake makuu mjini Duŕban, Afŕika Kusini