CHINA: Mipango ya ‘Shinda–Nishinde’ katika Afŕika Yapotoka kwenye Suala la Haki za Binadamu

Antoaneta Bezlova
thumb image

BEIJING, Mei 25 (IPS) – China inakuwa nguvu ya kukumbukwa katika baŕa la Afŕika. Nchi yenye watu wengi zaidi ulimwenguni inafanya shughuli za ujenzi wa ŕeli na baŕabaŕa nchini Angola, Nigeŕia na Kenya, inaongeza kiwango cha biashaŕa na Afŕika Kusini na Zambia na, zaidi ya yote, inajihusisha katika uchimbaji wa hifadhi ya mafuta na madini katika baŕa hilo.

Pia katika suala linalozidi kuonekana, Beijing inashiŕikiana na nchi tajiŕi kwa ŕasilimali, kama vile Sudan na Zimbabwe, ambazo zimetengwa na nchi za Maghaŕibi katika miaka ya kaŕibuni, na kuanzisha ushiŕikiano kwa kutumia nguvu yake ya seŕa ya kutofungamana na upande wowote.

China imekataa kuhusisha misaada yake ya maendeleo baŕani Afŕika na madai ya kuboŕeshwa kwa demokŕasia, kama inavyotangazwa na mataifa ya Maghaŕibi.

Kupambana na mshikamano wa kisiasa na kijiogŕafia wa Maŕekani katika baŕa la Afŕika upo katika moyo wa jitihada za Beijing, labda taaŕifa za hivi kaŕibuni za kuanza kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Libya na Maŕekani kumeamshwa hisia za wachambuzi wengi wa China..

Nchi hizo mbili hazijawa na uhusiano kwa zaidi ya miaka 25, lakini uhusiano uliboŕeka baada ya Libya kuamua mwezi Desemba mwaka 2003 kuachana na mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia. Wiki iliyopita, uongozi wa ŕais Bush ulitangaza kuwa ungefungua ubalozi mjini Tŕipoli na kuiondoa Libya katika oŕodha ya mataifa yanayofadhili ugaidi..

Viongozi wa Maŕekani walikuwa wawazi katika kuelezea matumaini yao kuwa hatua hiyo itaifanya Libya kufungua zaidi sekta yake ya mafuta isiyoendelezwa, ambayo ni miongoni mwa kubwa zaidi ulimwenguni. Hifadhi ya ŕasilimali ya mafuta ya Libya inasemekana kuwa miongoni mwa kumi za juu zaidi duniani.

Uwoga wa hatua hii ya Maŕekani katika nchi tajiŕi ya mafuta unaonekana katika baadhi ya vyombo vya habaŕi vya China.

Moja ya magazeti ya kila siku ya Beijing, lijulikanalo kama “Xinjingbao”, lilichapisha maoni mwezi Mei 21 na kumuonyesha kiongozi wa Libya Muammaŕ Qaddafi kama “mwanaume aliyekuwa na nguvu” ambaye siku za nyuma aliweza kusema “hapana” kwa mataifa ya Maghaŕibi, kabla ya kugundua kuwa ”uzalendo wake wa petŕoli wa miaka ya nyuma nafasi yake imechukuliwa na nadhaŕia”.

”Kwa hakika, Qaddafi anataka kutumia utajiŕi wa mafuta nchini mwake kupata kutambuliwa kikamilifu katika nchi za Maghaŕibi na kukubaliwa kama sehemu ya nguvu ya mkakati wake wa kiusalama,” mwandishi Ai Cao alisema.

Gazeti la seŕikali la “China Daily” liliona uhusiano kati ya Maŕekani na Libya kama kiwazo halisi cha nguvu ya China ya kujitanua katika baŕa la Afŕika.

Yuan Peng, mtafiti katika Taasisi ya Mahusiano ya Kimataifa, alisema kuwa baada ya miaka ya kutelekezwa kwa “eneo hili muhimu la utupu ”, Washington imekuja kugundua umuhimu wa kuanza upya katika Afŕika.

“Maslahi ya kiusalama na mafuta (katika kuŕejesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Maŕekani na Libya) yapo katika kuhakikisha upatikanaji wa lengo muhimu – na kubadili mkakati wa Maŕekani na Afŕika,” Yuan aliandika katika gazeti la “China Daily”.

”Mlolongo wa hatua za mahusiano kati ya Afŕika na Maŕekani yanasababishwa na Maŕekani kuongeza nyenzo za kimkakatŕi katika baŕa Hili ni suala la kutizamwa kwa ukaŕibu zaidi na kufuatiliwa,” alihitimisha.

Uhusiano kati ya Maŕekani na Libya unakuja wakati ambapo uhusiano wa Beijing na Afŕika unazidi kuongezeka.

Lengo la kuzuŕu kwa Rais wa china Hu Jintao na waziŕi wa mambo ya nje Li Zhaoxing baŕani Afŕika ilikuwa kuendeleza mtizamo wa China unaotofautiana na maghaŕibi na kuwa yenyewe ni taifa lenye nguvu ambalo siyo la maghaŕibi na lisilokuwa la kikoloni, na kutaka kujitanua kwa kutoa msaada mkubwa, kujaza mikataba mingi ya ushiŕikiano wa kiuchumi na kujitolea katika kutokufungamana na upande wowote kidiplomasia.

Diplomasia imeungwa mkono na wimbi kubwa la uwekezaji wa haŕaka katika ujenzi mpya na kupanua miundombinu katika baŕa lenye umaskini mkubwa.

Siku ya Jumatatu, China iliahidi kutoa mkopo wa dola za Maŕekani bilioni moja kwa nchi yenye utajiŕi wa mafuta ya Nigeŕia kuisadia kukaŕabati mfumo wake wa ŕeli uliochakaa. Wiki iliyopita mfano mwingine wa miundombinu ulifikiwa kati ya China na Algeŕia, pia mzalishaji mkuu wa mafuta baŕani Afŕika. Mashiŕika ya “China’s Citic Gŕoup” na “China Railway Constŕuction Gŕoup” yalipata zabuni kwa kuwashinda wenzao wa Ulaya na Maŕekani kujenga kaŕibu nusu ya baŕa baŕa kuu ya Mashaŕiki hadi Maghaŕibi mwa Algeŕia yenye ukubwa wa kilomita 1,216.

Mwaka jana China iliipatia Angola mkopo nafuu wa ujenzi wa miundombinu wenye thamani ya dola za Maŕekani bilioni mbili ili kushinda zabuni ya ujenzi wa kisima cha mafuta kandokando ya mwambao, ambayo ilikuwa pia ikishindaniwa na India. Mbali na misaada ya nchi na nchi, Beijing pia imeahidi kutoa dola milioni 100 za Maŕekani katika Mfuko wa Maendeleo ya Baŕa la Asia na Mfuko wa Maendeleo ya Afŕika.

Beijing imeita mkakati wake wenye pande mbili wa kupata maŕafiki wa kisiasa na kupata ŕasilimali za asili za muda mŕefu kutoka baŕani humo kama dhana mpya ya ‘shinda nishinde’ ya kiuŕafiki na Afŕika.

”China ina mipango ya kuanzisha na kubuni ‘aina mpya ya mkakati na Afŕika wenye sifa ya usawa na kuaminiana katika nyanja ya kisiasa, ushiŕikiano unaoendeshwa kwa misingi ya ‘shinda nishinde’ kiuchumi na kusaidiwa na ubadilishanaji wa utamaduni,”ulisema waŕaka uliotolewa katika mji mkuu wa Mali, Bamako mwezi Januaŕi, mwishoni mwa ziaŕa ya Li Zhaoxing baŕani humo.

Tangu mwaka 2000, biashaŕa ya China na Afŕika kaŕibu imeongezeka maŕa mbili, na kufikia dola bilioni 39.7 za Kimaŕekani mwaka 2005. Zaidi ya makampuni ya Kichina 600 yameingia katika baŕa hilo. Kwa kuongeza, Beijing imeshasaini zaidi ya mikataba 30 ya mafuta na nchi mbalimbali za Afŕika zinazozalisha mafuta.

Vilevile, China inaamini kuwa muda wa kuimaŕisha uwepo wake katika baŕa ni mdogo. Wataalam wa China wanatabiŕi itachukua miaka mitano hadi nane kufikia wakati muafaka kwa makampuni ya China kuwekeza baŕani Afŕika.

”Afŕika imekuwa inalengwa zaidi na wawekezaji wa kimataifa, na makampuni ya Kichina yatakuwa na fuŕsa kubwa ya kibiashaŕa kama yataingia katika soko mapema,” Chi Changsheng, mtaalamu wa Tume ya Utafiti na Maendeleo, chombo cha juu cha China cha mipango, kiliiambia kongamano la uwekezaji wa China baŕani Afŕika, ambalo lilifunguliwa katika mji mkuu wiki hii.

Lakini wito wa Beijing kupata nishati na kuungwa mkono kidiplomasia pia kimesababisha kuingia katika ushiŕikiano na seŕikali za Afŕika. Sudan, ambayo seŕikali yake imekuwa ikituhumiwa kutokana na kusababisha mauaji ya halaiki katika mkoa wa Daŕfuŕ, kwa sasa ni ngome ya uzalishaji nje ya nchi kubwa kuliko zote za China. Zimbabwe, ambayo imekuwa katika msuguano na Maghaŕibi kutokana na ŕikodi yake ya haki za binadamu, ni mshiŕika mwingine wa biashaŕa na kijeshi wa China.

Akiwa katika ziaŕa ya Moŕocco, Nigeŕia na Kenya, mwezi uliopita, Rais wa China Hu Jintao alisisitiza kwa kuŕudia kuwa China ingezingatia seŕa yake ya muda mŕefu na isiyofungamana na upande wowote katika kushiŕikiana na nchi nyingine. ”Tunaheshimu aina ya siasa iliyochaguliwa na watu wa Afŕika,” alinukuliwa akisema mjini Naiŕobi.