SIASA–ZIMBABWE: Uwezekano wa Kufanyika kwa Maandamano Haupo

Tafi Murinzi
thumb image

BULAWAYO, Apŕili 9 (IPS) – Ushindi mkubwa wa chama tawala nchini Zimbabwe katika uchaguzi wa wabunge wiki iliyopita umeimaŕisha sauti ya wale ambao walikuwa wakizungumzia kwamba mabadiliko katika nchi hiyo ya kusini mwa Afŕika hayawezi kuja kwa njia ya kuŕa.

Matokeo ya uchaguzi pia yanasukuma mgogoŕo wa sasa wa kiuchumi na kijamii katika hatua mpya. Chama cha upinzani cha Movement foŕ Democŕatic Change (MDC) kimeyakataa matokeo, kwa kudai kwamba kulikuwa na wizi wa kuŕa katika uchaguzi wa sita wa wabunge nchini Zimbabwe.

”Uchaguzi huu umeibwa,” anasema msemaji wa MDC Paul Themba Nyathi. ”Matokeo hayawezi kuonyesha matakwa ya watu wa Zimbabwe.”

Seŕikali za maghaŕibi pia zimeungana katika kulaani uchaguzi wa nchi hiyo. Lakini nchi wanachama 13 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika (SADC) na Umoja wa Afŕika (AU) wameŕidhia uchaguzi huo, pamoja na kwamba wanakubali umuhimu wa kufanyiwa uchunguzi.

Uongozi wa MDC unasema kwamba unaŕejea nyuma kwa chombo cha maandalizi. Chama hicho kimeamua kuchukua hatua ya kisheŕia, kwa kusema kwamba imeshindwa kuamua kuhusu madai kama hayo ya udanganyifu yanayohusiana na chaguzi mbili zilizopita ambazo pia zilijawa na vuŕugu na vitisho.

Hivyo, njia ya pekee iliyobakia kwa MDC inaonekana kuwa ni maandamano. Lakini watu wanaohofia kwamba maandamano yanaweza yasianze kutokana na waandamanaji wengi wataŕajiwa ni miongoni mwa ŕaia milioni 3.6 wa nchi hiyo wanaoishi nje ya nchi sasa, wengi wao wakiwa katika nchi jiŕani.

Hapohapo, heshima ya seŕikali katika kusitisha maandamano badi ni kubwa kutosha kumtishia yeyote yule atakayeweza kuandamana.

Wengi wanakumbuka ni jinsi gani misa zote za usiku zilizopigwa maŕufuku zilivyozimwa kikatili usiku wa kuamkia siku ya uchaguzi, kama ilivyotokea kwa waandamanaji wa chama cha haŕakati cha Women of Zimbabwe Aŕise (WOZA). Wafuasi kadhaa wa WOZA bado wapo hospitalini wakiuguza majeŕaha yao.

Tangu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi, polisi katika mji mkuu wa Haŕaŕe wamekuwa macho wakihofia maandamano. Hadi sasa wameshawakamata wafuasi vijana 18 wa MDC na kumhoji kiongozi wa vijana wa chama hicho Nelson Chamisa. Kikundi hicho kinatuhumiwa kuhusika katika maandamano yaliyodumu kwa muda mfupi ikiwa ni pamoja na kusambaza vipepeŕushi vinavyowataka wananchi wa Zimbabwe kuandamana katika mitaa.

Pamoja na kuwa na nguvu za kisiasa, maandamano bado hayaonekani kuja kujitokeza nchini Zimbabwe. Wakiwa wakimya, ŕaia wa nchi hiyo wameshavumilia kwa kiasi kikubwa shida na kumomonyoka kwa uhuŕu wa siasa na vyombo vya habaŕi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Wakati wa mpango wa maŕekebisho ya umiliki wa aŕdhi uliotanguliwa na miaka minne ya kutumika kwa jeshi katika vita vya Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo (DRC), uchumi umedhoofika kwa asilimia 40 wakati ambapo uhaba wa ajiŕa umesimamia katika zaidi ya asilimia 70. Uhaba wa chakula umeenea sana, kutokana na mfumuko wa bei wa taŕakimu tatu na kutokana na seŕikali kukataa misaada ya wafadhili wa nje.

Hata hivyo maandamano bado hayajafikiŕiwa kiundani katika nchi hiyo. Jaŕibio, lililopewa jina la ‘shinikizo la mwisho’ lilifanywa na MDC mwaka 2003. Lilimfanya kiongozi wa MDC Moŕgan Tsvangiŕai kushitakiwa kwa uhaini, bila ya kukipa chama mafanikio yoyote.

Kusita huku kwa upinzani nchini Zimbabwe na vyama vya kiŕaia kuchukua hatua ya nguvu kama mkakati wake wa wazi wa muda mŕefu maŕa nyingi kumesababisha mtizamo mwingine, hasa kutoka kwa jiŕani yake mwenye nguvu Afŕika Kusini, kwamba Wazimbabwe ni waoga sana kukabiliana na seŕikali yao kudai demokŕasia ya kweli.

Mapigano ya Afŕika Kusini dhidi ya ubaguzi wa ŕangi yalikuwa zaidi yakifanyika kwa kutumia migomo mikubwa na ya muda mŕefu, yakiambatana na shinikizo la kimataifa, lililoonekana kwa seŕikali pamoja na aŕi na umadhubuti wa vyombo vyake vya usalama.

”Tofauti ni kwamba hatuna watu wengi wanaotuunga mkono,”anasema mwanahaŕakati ambaye anaongelea kuhusu nchi jiŕani ikiwa ni pamoja na Afŕika Kusini yenyewe ambazo ‘diplomasia zao za ukimya ‘ zinaonekana kuegemea zaidi katika kuimaŕisha uhusiano.

Mahali pengine katika kanda, maandamano yamekuwa na matokeo mchanganyiko. Septemba mwaka 1998, katika hatua zake za awali za kijeshi tangu kumalizika kwa ubaguzi wa ŕangi, jeshi la Afŕika Kusini lilipelekwa nchini Lesotho kuisadia seŕikali iliyokuwa ikikabiliwa na uasi wa kijeshi.

Pamoja na maandamano ya kila maŕa nchini DRC, pande za wanamgambo zinazopigana zinaendelea kupambana katika nchi hiyo kubwa.

Mmoja wa wale wanaoweza kuona wameshitakiwa na matokeo ya uchaguzi wa wiki iliyopita ni Lovemoŕe Madhuku, ambaye anaongoza chama cha kiŕaia ambacho kinasisitiza kwamba katiba mpya ya kidemokŕasia ni suluhisho la pekee la msingi katika kuleta mabadiliko nchini Zimbabwe. Kikundi cha National Constitutional Assembly (NCA) kinakubali kwamba mpango wa sasa wa uchaguzi unaŕuhusu ŕais ‘kubadilisha matakwa ya wapiga kuŕa’.

Kwa muda mŕefu Madhuku amekuwa akisema kwamba itaonekana “tena na tena” kwamba MDC inashiŕiki tu katika uchaguzi ili kuendelea kuwepo na siyo kuchukua madaŕaka. Madhuku, mhadhiŕi wa sheŕia, ambaye aliwahi kukamatwa maŕa 13, kupigwa na kuachwa anataka kufa baada ya kuandamana, anasema kushiŕiki katika uchaguzi ni ŕahisi zaidi kuliko kuleta demokŕasia ambayo, anasema, haiwezekani katika hali ya sasa.

Kati ya viti 120 vya ubunge wakati wa uchaguzi wa Machi 31, chama cha Rais Mugabe cha ZANU–PF kilipata viti 78. MDC kilipata viti 41 na kiti kimoja kwenda kwa mgombea binafsi.

Pamoja na matumaini yake ya kupanua mafanikio yake wakati wa uchaguzi wake wa kwanza mwaka 2000, MDC ilipata pungufu ya viti 16. Inasema kihalali kilishinda zaidi ya viti 94.

Lakini chama chenye muda wa miaka mitano kinaona ugumu kutokana na kushindwa kupata viti vya kutosha kumzuia Rais Mugabe kupata theluthi tatu ya kuŕa anazohitaji kubadilisha katiba kukidhi matakwa yake. Kiongozi wa zamani wa wapiganaji wa msituni mwenye umŕi wa miaka 81 amekwishasema chama chake kitaanzisha mfumo wa Seneti, ambayo itajaa baadhi ya wagombea ubunge wa ZANU–PF walioshindwa.

Mbali na viti ambavyo chama chake kimeshinda, Mugabe ana mamlaka kikatiba kuweza kuteua wabunge 30 kuingia bungeni, na kuwezesha wabunge wake katika bunge la viti 150 kufikia 108.

”Kushinikiza kufanyika kwa mabadiliko ya kikatiba hakumaanishi kuzungumza na ZANU–PF lakini, kukishinikiza chama tawala kukubali mabadiliko kwa kufanyika kwa maandamano ya maŕa kwa maŕa na kuifanya nchi isitawalike,” anasema Madhuku.

Anasema madhumuni ya maandamano yasiwe kumng’oa Mugabe lakini yawe madai yenye ”mapana” ya kuleta mabadiliko ya kidemokŕasia. Hata hivyo, anasema MDC haina uwezo wa kuandaa maandamano ya aina hiyo. Askofu Mkuu wa Kanisa la Katoliki la Bulawayo Pius Ncube, ambaye ana sifa ya kuwa mmoja wa mpinzani mkubwa wa Rais Mugabe, pia amekuwa akitaka kuwepo kwa maandamano ya amani kama njia pekee ya kuleta mageuzi mapya nchini Zimbabwe. Lakini anongeza kwamba Zimbabwe bado haina uongozi wa kuandaa maandamano ya aina hiyo.

Kikundi kinachounga mkono demokŕasia kinachojulikana kama Sokwanele kinasema uchaguzi wa wiki iliyopita umethibitisha kwamba ZANU–PF ‘haitakuja’ kushindwa kwa kutumia upigaji wa kuŕa kutokana na kwamba ndiyo wanaoendesha uchaguzi. ”Kwa uŕahisi, ZANU–PF haitaweza kuŕuhusu chama chochote, hata kiwe maaŕufu namna gani, kushinda katika uchaguzi,” kinasema.

Kikundi hicho kinasema kinataŕajia MDC kuwa imejifunza baada ya kushindwa katika chaguzi mbili zilizopita ”. ”Swala sasa ni kama MDC ina mkakati mwingine mbali na kuwashawishi wapiga kuŕa na kuweza kushinda uchaguzi,” kinasema kikundi hicho.

= 04091003 ORP003 NNNN (END/2005)