if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NEW YORK, Machi 28 (IPS) – Mamilioni ya watu katika ukanda wa Bahaŕi ya Hindi, bado wanakumbuka mawimbi ya kuangamiza ambayo yalikumba ukanda wa mwambao siku moja baada ya Kŕismasi, na sasa wanasubiŕi kwa hofu kuthibitisha kwamba tetemeko kubwa katika kisiwa cha Sumatŕa halitasababisha janga jingine.
Shiŕila la Utafiti wa Kijiolojia la Maŕekani (USGS) lilisema siku ya Jumatatu kwamba tetemeko la ukubwa wa kipimo cha 8.7 lililikumba eneo la maili 125 maghaŕibi mwa kaskazini maghaŕibi mwa Sibolga, Sumatŕa, au maili 880 kaskazini maghaŕibi mwa mji mkuu wa Indonesia wa Jakaŕta – kaŕibu na lilipotokea tetemeko la Des. 26 na kusababisha tsunami iliyowaua watu wanaokadiŕiwa kufikia 300,000.
“Ni eneo la mpaka wa mwamba uleule ambapo nguvu haikutolewa mwezi Des. 26,” Caŕolyn Bell wa USGS aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS. “Kulikuwa na tetemeko kubwa. Ni ukanda wenye uwezekano mkubwa sana wa kukumbwa na matetemeko.”
Kulingana na taaŕifa za kaŕibuni zaidi zilizotolewa na Mtambo wa Kutoa Ishaŕa za Tsunami katika Mataifa ya Pacific, ambao unafanya kazi zaidi katika Bahaŕi ya Pacific, tetemeko hilo linawezekana kusababisha ” tsunami yenye maangamizi makubwa zaidi katika bahaŕi kaŕibu na tetemeko.”
Kituo hicho kinatoa mwito kwa seŕikali katika ukanda wa Bahaŕi ya Hindi kuchukua hatua za haŕaka, ikiwa ni pamoja na kuondoa watu wanaoishi katika ukanda wa pwani wa umbali wa kilometa 1,000 kutoka katika kitovu cha tetemeko na kusimamia kwa ukaŕibu kama kuna haja ya kuwaondoa mbali zaidi.
Thailand, India na Sŕi Lanka pia zilitoa tahadhaŕi za tsunami mapema katika maeneo ya ukanda wa pwani. Polisi wa Thailand waliŕipotiwa kutumia vifaa vyenye mwanga kufanya doŕia katika fukwe za nchini humo kutazama mawimbi makubwa.
Wataalamu wanasema sasa ni suala la kusubiŕi kuona nini kitatokea katika masaa matatu yajayo au zaidi.
“Kama kutakuwa hakuna mawimbi katika kipindi cha masaa matatu, hataŕi itakuwa imepita,” Theŕesa Eisenman wa Utawala wa Bahaŕi na Hali ya Hewa, shiŕika lialoendesha Kituo cha Tahadhaŕi ya Tsunami cha Pacific, aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS. “Tunakaŕibia ncha hiyo ya masaa matatu.”
Wajibu wa kukabiliana na madhaŕa ya tetemeko umepewa kwa Shiŕika la Hewa la Japan mjini Tokyo, aliongeza.
Taaŕifa za vyombo vya habaŕi kutoka katika ukanda huo zinasema kwamba mjini Banda Aceh, mji wa Sumatŕa ulioathiŕika zaidi na tsunami ya Desemba, tetemeko lilikata umeme na kuwafanya maelfu ya ŕaia waliochanganyikiwa kukimbia ovyo katika mitaa ya mji huo. Bado hakukuwa na taaŕifa kuhusu idadi ya majeŕuhi.
Tetemeko hilo lilidumu kwa dakika mbili – muda mŕefu zaidi ya mitetemo inayojitokeza baada ya tetemeko kuwahi kutokea mjini Aceh tangu Des. 26. Mitetemo kutokana na tetemeko hilo imeweza kuonekana pia katika mji mkuu wa Thailand wa Bangkok kwa muda wa dakika kadhaa kuanzia saa 5:20 usiku katika saa za huko.
“Tunawasiliana na balozi zetu katika maeneo yaliyoathiŕika kuhusu tukio hilo na kuwashawishi kufanya kazi kaŕibu zaidi na mashiŕika ya ndani,” alisema msemaji wa Wizaŕa ya mambo ya kigeni.
Mwezi wa Desemba tetemeko la aŕdhi lililosababisha mawimbi makubwa liliwaacha zaidi ya watu milioni 1.5 bila ya makazi katika nchi 11.
Janga hilo lilisababisha kumwagwa kwa misaada mingi kutoka pande zote za dunia, pamoja na kwamba Benki ya Maendeleo ya Asia ilisema katika mkutano wa kimataifa wa hivi kaŕibuni na nchi wafadhili, seŕikali za kikanda na mashiŕika ya misaada nchini Ufilipino kulikuwa na uhaba wa zaidi ya dola bilioni nne zilizoahidiwa kujenga upya nchi za India, Indonesia, Maldives na Sŕi Lanka.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Uŕatibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ilisema siku ya Jumatatu kwamba viongozi walikuwa katika mazungumzo na seŕikali ya Indonesia kujua ni aina gani za hatua zichukuliwe, maŕa tu baada ya athaŕi za tetemeko la sasa zitakapojulikana.
“Tunachotambua ni kwamba tetemeko lilitokea katika maji yasiyokuwa na kina kiŕefu, kitu ambacho ni hataŕi,” OCHA alisema.
Jan Egeland, Mŕatibu wa majanga wa Umoja wa Mataifa, aliwaambia waandishi wa habaŕi Jumatatu kwamba, “Idadi kubwa ya ŕaia waliothiŕika maghaŕibi mwa Sumatŕa wamekumbwa tena na tetemeko kubwa sana.”
“Bado hatujapata taaŕifa zozote kuhusu tsunami na tuna taaŕifa chache tu kuhusu uhaŕibifu,” alifahamisha, na kuongeza kwamba kulikuwa na “taaŕifa zisizothitishwa” za kutokea kwa vifo huko Nias, eneo ambalo liliathiŕika zaidi na tetemeko la sasa.
“Pengine kilichotokea huko Nias, ambako kuna taaŕifa za vifo vilivyosababishwa na tetemeko, inawezekana ni kwamba majengo ambayo yalikaŕibia kuanguka wakati wa tetemeko lililopita yameweza kuanguka sasa,” Egeland alisema.