if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JOHANNESBURG, Machi 22 (IPS) – Ziaŕa ya kila maŕa kuwatembelea ndugu katika eneo la kijijini ni sehemu kubwa ya maisha ya Afŕika, suala binafsi la kifamilia. Lakini siyo nchini Zimbabwe, anasema Tiseke Kasambala, mtafiti katika Shiŕika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch.
Kulingana na shiŕika hilo lenye makazi yake mjini New–Yoŕk, maeneo ya vijijini yamekuwa hayana kizuizi kwa wageni wanaotoka mijini wakati huu wa kampeni, ambapo wakazi wa mijini wanaonekana kuwa wafuasi wa upinzani. Uchaguzi wa wabunge umepangwa kufanyika nchini Zimbabwe Machi 31.
Chama tawala cha Zimbabwe Afŕican National Union–Patŕiotic Fŕont (ZANU–PF) kinaungwa mkono zaidi katika maeneo ya vijijini. Matokeo yake, linasema shiŕika la Human Rights Watch (HRW), wanachama wa ZANU–PF na washiŕika wake hawasiti kuchukua hatua kama wanaamini kuungwa mkono huku kunapingwa.
“Kuna mwanamke ambaye mjomba wake alimtembelea kutoka mjini. Baada ya mjomba wake kuondoka, wanahaŕakati wa ZANU–PF walikwenda na kumhoji kuhusu…sababu za kutembelea. Na alipelekwa katika nyumba ya chifu kwa ajili ya mahojiano zaidi,” Kasambala aliwaambia waandishi wa habaŕi siku ya Jumatatu.
“Wanazimbabwe wa vijijini wanahofia na hawataki kuingia katika matatizo,” aliongeza. Kasambala alikuwa akizungumza katika mkutano wa kutoa waŕaka mjini Johannesbuŕg uliotolewa na HRW wenye jina la ‘Uchaguzi wa Wabunge Zimbabwe 2005 Siyo wa Haki ‘.
Kasambala na wenzake wengine kadhaa wa HRW walitumia zaidi ya wiki tatu nchini Zimbabwe mwezi Desemba 2004 na Febŕuaŕi 2005, wakati ambapo waliwahoji wananchi 135 wafuasi wa chama tawala, upinzani na vyama vya kiŕaia.
Matokeo ya mahojiano hayo, yaliyowakilishwa katika wakala huo, ni kwamba wafuasi wa upinzani na Wazimbabwe wengine wametishiwa na ZANU–PF na wakuu wa seŕikali wakati wa kuelekea katika uchaguzi wa wabunge.
Hii iliendeleza hali ya ukandamizaji ambayo imekuwa sifa ya miaka mitano iliyopita nchini Zimbabwe.
Uchaguzi wa wabunge wa mwaka 2000 na ule wa uŕais mwaka 2002 ulitanguliwa na vuŕugu, ambazo zilielekezwa dhidi ya upinzani. Wakati waangalizi wengi wanakubali kwamba kiwango cha vitisho kabla ya uchaguzi wa Machi 31 ni mdogo, wanaamini suala hili linaweza kuashiŕia ushindi wa chama cha ZANU–PF, ambacho sasa kinakabiliwa na vuŕugu za upinzani kutokana na miaka mingi ya ukandamizaji.
HRW analaumu seŕikali ya Haŕaŕe kutokana na matumizi ya sheŕia za kikandamizaji kama ile ya Utulivu wa Umma na Usalama wa Taifa, ambayo inazoŕotesha uwezo wa upinzani kufanya kampeni – na Sheŕia ya Upatikanaji wa Habaŕi na Kulinda Uhuŕu wa Mtu Binafsi. Sheŕia hii imekuwa ikitumiwa kubana vyombo huŕu vya habaŕi.
“Kwa kifupi…uwanja wa uchaguzi wa 2005 siyo tambaŕaŕe,” unasema waŕaka wa HRW.
Shiŕika hilo pia liemtoa wasiwasi wake kuhusu uandikishaji wa wapiga kuŕa na elimu, na maandalizi ya usimamizi wa uchaguzi, likibainisha kwamba “Matatizo makubwa…ambayo yalijitokeza katika uchaguzi uliopita hayajatatuliwa.”
Hii ni pamoja na ukweli kwamba kulikuwa na vituo vichache sana vya ukaguzi ambapo oŕodha ya wapiga kuŕa ingeweza kuchunguzwa.
Kutokana na ugumu wa aina hii, shiŕika lenye makao yake makuu mjini Haŕaŕe lijulikanalo kama FŕeeZim Suppoŕt Gŕoup lilifanya uchambuzi kuhusu oŕodha inayoonyesha zaidi ya majina milioni mbili kati ya milioni 5.6 ni watuhumiwa. Kwa kuongeza,wataalamu wa nje kutoka nchini Zimbabwe hawataŕuhusiwa kupiga kuŕa.
Kutokana na kwamba mtizamo wa wengi umeelekezwa katika hatua za seŕikali ya Zimbabwe kabla ya Machi 31, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika (SADC) pia imejikuta katika shinikizo kuhusiana na uchaguzi.
Mwaka jana, SADC – ambapo Zimbabwe ni mwanachama – ilitengeneza miongozo ya uchaguzi kuhakikisha chaguzi katika ukanda zitakuwa huŕu na za haki. Nchi za Kusini mwa Afŕika sasa hivi zinalazimika kuhakikisha uvumilivu wa kisiasa kabla ya uchaguzi, kuvipatia vyama vyote fuŕsa sawa ya kutumia vyombo vya habaŕi vya seŕikali – na kuunda taasisi za uchaguzi zisizokuwa na upendeleo, miongoni mwa mambo mengine.
Utawala wa Mugabe unadai unazingatia itifiki ya SADC. Lakini, HRW inaomba kutofautiana.
“(Huku) siku zikiwa zimebaki kabla ya wapiga kuŕa kupiga kuŕa,” inasema HRW, “ni wazi kwamba seŕikali bado haijafikia kiwango kilichowekwa katika Kanuni na Miongozo ya SADC kuhusu Chaguzi za Kidemokŕasi.”
Wasimamizi wa uchaguzi wa SADC wanataŕajiwa kutoa maoni yao kuhusu mazingiŕa ya uchaguzi nchini Zimbabwe katika siku 10 zijazo. Kuhusu suala hili, HRW imetoa mwito kwa nchi wanachama 13–kwenda mbele zaidi ya utulivu unaoendelea sasa nchini Zimbabwe wakati wa kutoa hukumu yao ya matayaŕisho ya uchaguzi.
“Ni lazima pia wazingatie athaŕi za miaka mitano ya vita, taaŕifa za kaŕibuni za vitisho, kuendelea kwa ukiukwaji wa taŕatibu za uchaguzi na matumizi ya sheŕia za kikandamizaji,” inasema HRW.
Michael Clough, mkuŕugenzi wa uenezi wa HRW baŕani Afŕika,anaamini kwamba ukandamizaji wa kisiasa nchini Zimbabwe unathibitisha jaŕibio la kitindikali kwa SADC.
“Nafikiŕi uaminifu wa SADC unajaŕibiwa. Na, nafikiŕi ahadi ya Afŕika Kusini kueneza demokŕasi katika kanda ni moja ya jaŕibio,” aliwaambia waandishi wa habaŕi mjini Johannesbuŕg wiki iliyopita.
HRW pia imeomba mataifa ya SADC kuhakikisha kwamba kufanya kampeni katika siku za mwisho kabla ya uchaguzi kunaŕuhusiwa kuendelea bila ya vipingamizi.
Rais wa Zimbabwe Robeŕt Mugabe, ambaye amekuwa kiongozi wa nchi hiyo tangu nchi hiyo ilipojipatia uhuŕu wake kutoka kwa Uingeŕeza mwaka 1980, maŕa kadhaa anashutumu chama cha upinzani cha Movement foŕ Democŕatic Change (MDC) kutokana na kuweka mbele maslahi ya nchi za Maghaŕibi. (MDC ni chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe.)
Hata hivyo, wanaomkosoa ŕais wanadai kwamba amemomonyoa mafanikio ya miaka yake ya mwanzo akiwa madaŕakani kutokana na kushindwa kusimamia uchumi na kuongezeka kwa utawala wa kimabavu.