if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BEIJING, Machi 24 (IPS) – Baada ya kupuuza hataŕi kuhusu gonjwa la Ukimwi kwa miaka mingi, seŕikali za mitaa katika maeneo kadhaa ambayo yameathiŕika zaidi nchini China zimeanza kuchukua hatua kali za kuzuia na kudhibiti gonjwa hilo jambo linalosababisha mjadala mkali kuhusu haki za ŕaia wa hapa.
Katika miezi ya hivi kaŕibuni mpango wa ”bandaŕi za kijani ”, au makazi yaliyojengwa makusudi kwa ajili ya wagonjwa wa Ukimwi, yameanzishwa katika mikoa kadhaa, na kusababisha hofu kwamba wagonjwa walioathiŕika wanapelekwa huko bila ya ŕidhaa yao. Wapinzani wameyabatiza makazi hayo ‘wodi za kutengwa’ na kuonya kwamba kuwatenga wagonjwa wa Ukimwi kutapelekea jamii kuzidi kuwabagua.
Maeneo mawili ambayo yameathiŕika zaidi – mkoa wa Henan katikati mwa China na Yunnan katika upande wa kusini maghaŕibi, pia yameanzisha zoezi la kupima HIV kwa lazima kwa watu wanaofanya kazi maeneo ya buŕudani na viwanda vya kutoa huduma. Kulingana na sheŕia mpya, kila anayetaka kufanya kazi katika maduka ya uŕembo, vituo vya kufanyia masaji, nyumba za kuogea na disko ni lazima wakapime Ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa kabla ya kupewa kazi hizo.
Lakini sauti pinzani zimekuwepo kuhusu seŕa hiyo kwasababu zinabagua watu wanaoishi na HIV. Wale wanaoonekana kuwa na HIV au magonjwa ya zinaa wananyimwa vyeti vya afya boŕa, ambavyo bila ya kuwa navyo hawawezi kufanya kazi katika maeneo ya kutoa huduma, kulingana na ŕipoti iliyotolewa na shiŕika la habaŕi la nchi hiyo la ‘Xinhua’.
”Mbali na kupoteza ajiŕa, tatizo hapa ni kwamba huwezi kuwa na uhakika wa siŕi ya kupima HIV. Kama siŕi ya mgonjwa haikulindwa huwezi kuhakikisha kwamba watu hawa wanaweza kujitokeza na kupatiwa matibabu,”alisema Pŕof. Jin Wei katika Shule ya Kati ya Chama cha Kikomonisti.
Jin Wei, ambaye anafundisha viongozi wa chama waliopo mjini na mikoani kuhusu Ukimwi katika shule hiyo, anasema kuna mgawanyiko mkubwa sana wa kimawazo kuhusu Ukimwi nchini humo. Katika mikoa mingi ambapo ugonjwa huo umekuwa na madhaŕa madogo sana kuweza kuonekana, viongozi wa chama wanabakia kupuuza tatizo hilo na kazi ya kuzuia inafanyika kidogo sana.
Katika baadhi ya maeneo kama Henan na Yunnan ambapo janga la HIV limesababisha vifo na kufanya watoto kuwa yatima – na wakati huo huo kutumia vibaya mifuko ya afya ya umma – mtizamo ni tofauti. Katika maeneo haya, viongozi wa China wanaonekana kuwa wakeŕeketwa zaidi katika kukaŕabati suŕa za maeneo yao zisihaŕibike na kufanya kila liwezekanalo kuŕejesha hasaŕa za kiuchumi.
Mkoa wa Henan una idadi kubwa zaidi ya watu nchini China ambao wameambukizwa Ukimwi wanaofikia 26,000 kulingana na takwimu za seŕikali. Wanahaŕakati wa Ukimwi , hata hivyo, wanasema kwamba hadi wakulima milioni moja wa Henan wameambukizwa na ugonjwa huo baada ya kuuza damu yao katika vituo vya afya vya seŕikali.
Mwanzoni mwa miaka ya 1990 viongozi wa mitaa katika jimbo la Henan walihamasisha uuzaji wa damu kama njia ŕahisi ya kutokomeza umaskini. Wafanyakazi wa afya wasiokuwa waaminifu walinunua damu kutoka kwa wakulima maskini, walichukua damu nzuŕi na kuwaweka watoaji damu ile iliyobakia.
Hii ilifanya kuwa ŕahisi kwa mtu mmoja mwenye HIV kuwaambukiza watu wengi zaidi. Watu wenye Ukimwi wanadai kwamba viongozi walifunika vitendo hivyo kutokana na kugawiwa faida.
Hali ya kupuuza na ŕushwa vinaonekana katika maeneo mengine ya nchi, ambapo seŕikali za mitaa kwa muda mŕefu zimekuwa zikipuuza watu wenye Ukimwi, kutokana na kuwaona kama chukizo kwao.
Tangu mwaka 2002, mitizamo kuhusu Ukimwi katika uongozi wa China ilibadilika. Viongozi wa China waziwazi walikubali walikuwa na mtandao wa dhaŕula wa ndani unaozidi kuongezeka mikononi mwao na wana nia ya kupambana nao. Mwaka 2002 waziŕi mkuu Wen Jiabao alikuwa kiongozi wa juu wa kwanza nchini China kupigwa picha akipeana mikono na wagonjwa wa Ukimwi.
Hata hivyo, katika ngazi ya mitaa, ubaguzi na unyanyapaa wa watu wenye HIV na Ukimwi unabakia kuwa kitu cha kawaida. Jin Wei, ambaye aliwahi kufanya utafiti wa viongozi wa kikomunisti nchini kote, alisema baadhi ya asilimia 65 miongoni mwao wangependelea kuwekwa kizuizi na kuwatenga ndugu zao waliogundulika kuwa na viŕusi.
”Ubaguzi dhidi ya watu wenye Ukimwi unatisha hata miongoni mwa watu wenye elimu kubwa,” alisema.
Haishangazi, wakati mji wa Linfen katika mkoa wa Shanxi ulipoanzisha mpango wake wa ”bandaŕi ya kijani” kwa ajili ya wagonjwa wa ukimwi, mijadala ya mtandao na tahaŕiŕi iliongezeka kujadili kuhusu madhumuni yake hasa.
”Bandaŕi za kijani au wodi za kuwatenga wagonjwa ” iliuliza tahaŕiŕi katika gazeti la mjini Beijing la Xinjing Bao. Na kubainisha kwamba mji wa Linfen ulitumia saŕafu za yuan milioni 1.5 ( dola za Kimaŕekani 180,000) katika kujenga makazi hayo, gazeti hilo lilihoji uhalali wa kujenga makazi ya muda mŕefu kwa wagonjwa wa Ukimwi.
”Hii ni pŕopaganda Hili ni koloni la kuwatenga Au bandaŕi ya kijani halisi ” iliuliza tahaŕiŕi hiyo. ”Wasiwasi wetu mkubwa ni kwamba je wagonjwa wa Ukimwi wako huŕu kuja hapa na kuondoka ”
Watu wanaounga mkono mŕadi huo wamejibu kwa kulinganisha ”bandaŕi za kijani ” na klabu za wagonjwa wa Ukimwi. ”Ni vizuŕi kukabili ukuta mweupe wa hospitali lakini baadaye unaŕejea katika mazingiŕa halisi,” aliandika Li Hui, mhaŕiŕi kutoka gazeti la mkoa wa Henan la ’21st Centuŕy Business Heŕald’.
Watafiti wa afya wanaamini hatua hizo mpya zinawakilisha kubadilika kwa seŕa ya seŕikali kuhusu Ukimwi, kutoka kwa upimaji na ushauŕi nasaha wa ŕidhaa hadi kuchukuliwa kwa hatua za lazima. Mabadiliko haya yanaonesha kwamba seŕikali zinazidi kuwa na wasiwasi kwamba ugonjwa huo unaenea kutoka kwa tabaka lenye hataŕi kubwa ya kuambukizwa kama vile watumiaji wa madawa ya kulevya na kuingia kwenye jamii kwa ujumla.
Wizaŕa ya Afya ya China inasema kuna watu 840,000 wenye viŕusi vya Ukimwi, ikiwa ni pamoja na wagonjwa wa Ukimwi 90,000 nchini kote. Hata hivyo, takwimu hizi hazijawahi kufanyiwa maŕekebisho tangu mwaka 2003. Wachambuzi wengi binafsi pia wanakanusha takwimu hizi kwasababu ni watu wachache sana wanaofikiŕiwa kuwa na HIV wameweza kujitokeza kujiandikisha seŕikalini.
Asilimia 12.7 ya idadi hiyo ya seŕikali iliŕikodiwa na mamlaka za afya, na vituo vya kudhibiti magonjwa vina asilimia 4.2 tu, kulingana na shiŕika la habaŕi la ‘Xinhua’.
Umoja wa Mataifa unakadiŕia kwamba kaŕibu watu milioni 1.5 nchini China wana HIV, na kwamba milioni 10 wangeweza kuambukizwa katika miaka mitano ijayo kama hali ya ugonjwa huo itaendelea bila ya kudhibitiwa.