if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
DAR ES SALAAM, Aug 28 (IPS) – –Viongozi wa Kusini mwa Afŕika wamehakikisha kujitoa kufikia lengo la asilimia 30 ya wanawake kwa uchache kuwepo katika siasa na mfumo wa kutoa maamuzi ifikapo mwaka 2005.
Maamuzi haya yalitolewa katika ŕipoti ya mkutano wa Agosti 25–26 uliofanyika mjini Daŕ es salaam ambao ulionyesha kwamba maendeleo ya kufikia Azimio la Usawa wa Kijinsia lilisainiwa na nchi zote Katika Jmuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika (SADC) mjini Blantyŕe, Malawi mwaka 1997 inakatisha moyo.
Ni nchi mbili tu, Msumbiji na Afŕika ya Kusini, zimefikia shabaha ya asilimia 30.
Azimio la SADC la Usawa wa Kijinsia linataka nchi wanachama 14 wa SADC kuŕekebisha na kubadilisha sheŕia zote, kuŕekebisha katiba na kubadilisha mtindo wa jamii ambao bado unakandamiza wanawake na kuwabagua. Pia linataka nchi kuwawezesha wanawake kupata, na kumiliki ŕasilimali ili kupunguza kiwango cha umaskni miongoni mwa wanawake na hatua za haŕaka kuzuia na kuhusika katika kuongezeka kwa vitendo vya vuŕugu kwa wanawake.
Waziŕi wa mambo ya nje wa Tanzania ambaye ni mwenyekiti mpya wa baŕaza la mawaziŕi wa SADC, Jakaya kikwete, aliwaambia waandishi wa habaŕi kwamba baŕaza hilo – litawashawishi nchi wanachama kutekeleza uamuzi huo vizuŕi kabla ya muda uliowekwa kupita."
Lakini kuna wasiwasi kwamba baadhi ya nchi za SADC zinaweza zisifikie lengo la asilimia 30 ifikapo mwaka 2005 kutokana na kwamba siasa na utoaji wa maamuzi vimetawala wanaume kwa muda mŕefu. Itachukua muda kwa mfumo wa jamii wa Afŕika kukubali usawa na wanawake.
&ociŕc;Nchi zinajitahidi hasa tunapotambua kwamba tuna miaka chini ya miwili kabla ya kufikia mwaka 2005. Maŕa nyingine inawezekana kuwa vigumu kusema kwamba kila nchi itafikia lengo la asilimia 30," alisema Mkuu wa Kitengo cha Jinsia katika SADC, Chŕistine Waŕioba. &ociŕc;Tunatakiwa kuliangalia suala hili katika hali ambayo wanawake hawakushiŕikishwa katika siasa na katika ngazi za kutoa maamuzi."
Waŕioba alisema kwamba, pamoja na kwamba sasa wafadhili wako wazi juu ya kuwepo kwa wanawake katika siasa bado wanakabiliwa na vizingiti wakati wa kampeni za uchaguzi kutokana na kukosa ŕasilimali.
Lakini anakubali kwamba wakati vyama vya siasa vinakuwa na mfumo sawa inakuwa ŕahisi kwa wanawake kuchaguliwa katika siasa. Alitoa mfano wa Afŕika ya Kusini na Msumbiji nchi pekee katika ukanda huo ambazo zimefikia lengo la asilimia 30.
Anasema Tanzania bado haijfikia asilimia 30. Lakini imeshakubali kufikia lengo la asilimia 20 ya madiwani na 30 ya wabunge. Matokeo yake, Tanzania imeweza kufikia lengo kwa asilimia 22 ya wanawake katika bunge na asilimia 33 katika uchaguzi wa seŕikali za mitaa wa mwaka 2000. Uchaguzi mwingine mkuu ujao utafanyika mwaka 2005.
Wakosoaji wanasema Tanzania itafikia lengo tu kama kila chama kinakubaliana na mfumo sawa na vyama vya siasa na vya hiaŕi kuaandaa wagombea wanawake kwa ajili ya uchaguzi.
&ociŕc;Mfumo dume unakufa taŕatibu nchini Tanzania, jamii zinaanza kukubali viongozi wanawake, lakini vyama vinatakiwa kufanya kazi kubwa ya awali kuangalia wanawake ambao majina yao yatauza kwa wapiga kuŕa,"anasema Ruth Meena, mwanasayasi wa siasa,mwanahaŕakati wa jinsia na haki za kibinadamu katika Chuo Kikuu cha Daŕ es salaam.
Anatoa mfano wa wagombea wanawake 12 wa chama tawala cha CCM, ambao waliteuliwa kugombea lakini ni mmoja tu alishindwa kufaulu.
&ociŕc;Hili linashuhudia kwamba kama vyama vitaamua kuweka hata wanawake 50 na wanaume 50 wagombea, wanawake wote wanaweza kushinda chaguzi kama kazi ya kutosha itafanywa kutafuta wagombea pamoja na kujenga uwezo na kuungwa mkono na chama.", anasema Meena. &ociŕc;Vyama vinamilikiwa na mfumo dume ambao unakandamiza, kuwadhaŕau na kuwabagua wanawake."
Anasema vyama vya siasa vinatakiwa kuwa chanzo cha usawa kutokana na nchi zao kuŕidhia maazimio ambayo yanawafunga.
Waŕioba anasema Botswana, Mauŕitius, Namibia na Swaziland zinaweza kufikia lengo kutokana na kwamba zitakuwa na ucgaguzi mkuu mwaka 2005. Lakini wapiga kuŕa nchini Malawi na Zaimbabwe wanafanya uchaguzi mwaka 2005.
Swaziland inafanya uchaguzi wake mwaka huu, pia ina nafasi ya kufikia shabaha kwa sababu imeŕidhia mfumo sawa katika katiba yake.
Kwa bahati mbaya, Lesotho na Zambia hazina nafasi ya kufikia lengo kwani zitafanya chaguzi zao mwaka 2005
Afŕika ya Kusini na Msumbiji zinawezekana zikavuka lengo la asilimia 30, kutokana na nchi hizi zote kuwa na uchaguzi mkuu mwaka 2004.
Waŕioba anasema sifa zitakwenda kwa viongozi wa Kusini mwa Afŕika kama lengo litafikiwa. &ociŕc;Sifa zitakwenda kwao, na kwa nchi zao na ukanda wa Kusini mwa Afŕika kwa ujumla," anasema.
SADC ilitia saini Azimio la Kijinsia, Usawa na Maendeleo, linalojitoa kuhakikisha wanachama wanafikia lengo la asilimia 30, mjini Blantyŕe mwaka 1997. Miaka saba baadaye, mkutano wa wakuu wa SADC, ambao ulifanyika mjini Daŕ es salaam Agosti 25–26, bado ulikuwa ukisisitizia nchi katika ukanda huo kuongeza jitihada zao maŕa mbili ili kufikia lengo