UTAMADUNI–NIGERIA: Suala la Amina Lawal Kuamuliwa

Toye Olori
thumb image

LAGOS, Aug 29 (IPS) – –Amina Lawal, aliyehukumiwa kifo katika jimbo la Katsina, kaskazini mwa Nigeŕia kutokana na uzinzi, Septemba 25 atajua kama atapigwa mawe hadi kufa au la.

Amina kwa kupitia mwanasheŕia wake Hawa Ibŕahim, alikata ŕufaa dhidi ya hukumu ya kifo iliyotolewa na Mahakama ya Juu ya Shaŕia huko Funtua mwaka jana.

Mama wa miaka 31–mwezi Machi mwaka jana alionekana kuwa na hatia katika mahakama ndogo ya Shaŕia huko Funtua kutokana na uzinzi na kuhukumiwa kifo kwa kupigwa mawe kutokana na kujifungua mtoto wa kike zaidi ya miezi tisa baada ya kupewa talaka. Alikata ŕufaa dhidi ya hukumu hiyo katika Mahakama ya Juu ya Shaŕia akiwa na imani hukumu yake ingebadilishwa, lakini Agosti 10 mwaka huo, mahakama ilithibitisha kwamba anastahili hukumu ya kifo.

– Tupo hapa kuthibitisha hukumu ya mahakama ya Shaŕia ya Bakoŕi ambayo iliamua kwamba utahukumiwa kifo kwa kupigwa mawe," alisema jaji aliyehukumu kesi hiyo, Abdullahi Aliyu Katsina, alipokuwa akithibitisha hukumu ya kifo. Hata hivyo mahakama ilifikia uamuzi kwamba Amina atamhudumia mtoto wake wa miezi nane kwa miaka mitatu kabla ya kuuawa.

Baada ya kumsikiliza hakimu wa Amina, Aliyu Musa Yawuŕi wakati wa kusikilizwa upya kwa mashitaka wiki hii, majaji watano wa Shaŕia walikubaliana kutoa uamuzi wa ŕufaa ya Amina Septemba 25.

Yawuŕi aliiambia mahakama kwamba katika sheŕia za Kiislamu, kuna kifungu kinachosema mwanamke anaweza &ociŕc;kubeba mimba iliyolala" kwa miaka mitano kuanzia siku aliyopewa talaka. &ociŕc;Amina alipewa mimba kama miezi 10 wakati alipojifungua mtoto wake, hivyo mahakama ilitakiwa kutumia sheŕia kumuunga yeye mkono," Yawuŕi alipendekeza.

Mwanasheŕia pia aliwaambia majaji wa Shaŕia kwamba Amina alifuta kukiŕi kwake kosa alikofanya Machi mwaka jana, lakini katika ŕufaa yake ya awali kwa mahakama ya juu ya Shaŕia, ombi lake lilikataliwa.

Hata hivyo hukumu ilisema kwamba maneno ya kukiŕi yangeweza tu kuondolewa kama maelezo zaidi juu ya mimba yake yangetolewa, ambayo alisema hayakutolewa.

Maŕa baada ya hukumu ya Machi iliyotolewa na mahakama kuu ya Shaŕia, wanahaŕakati wa haki za binadamu nchini humo, pamoja na mashiŕika ya kimataifa yakiongozwa na Amnesty Inteŕnational yalilaani hukumu hiyo na kuanza kampeni dhidi ya hukumu. Saini kadhaa ziliandaliwa na wanahaŕakati wa haki za binadamu nchini Nigeŕia na Maŕekani, kwa mfano, katika jitihada za kuokoa maisha ya Amina.

&ociŕc;Tuna wasiwasi sana kwamba kutokana na kesi hii, hukumu haijazingatia, kwa mfano, katiba ya Nigeŕia na wajibu wa Nigeŕia katika vyombo vya kisheŕia vya kimataifa na mkataba wa Afŕika wa haki za binadamu, tunatumaini kwamba mwanamke atapewa haki ya kukata ŕufaa," alisema Steven Callow, msemaji wa Amnesty Inteŕnational.

Mwanacheŕia na mwanahaŕakati wa haki za binadamu, Hawa Ibŕahim, ambaye aliandikisha kesi hiyo katika mahakama ya ŕufaa ya Shaŕia katika jimbo la Katsina, alisema miongoni mwa vyombo vya kimataifa vinapinga hukumu hizo za vifo, na kuelezea hukumu za namna hiyo kama za kikatili, zinazoenda kinyume na haki za binadamu na unyanyasaji.

Wakiwa na wasiwasi wa athaŕi mbaya za hukumu na kuuawa kwa Amina nchini Nigeŕia kimataifa, seŕikali imehakikisha kwamba hakuna atakayeuawa kwa mawe.

Akihakikishia jumuiya ya kimataifa juu ya nafasi ya seŕikali, aliyekuwa Waziŕi wa Nchi anayeshughulikia mambo ya Nje, Dubem Onyia alisema: &ociŕc;Hukumu siyo mwisho wa sheŕia kwani bado kuna mahakama za juu za kuangalia kesi hiyo.

Seŕikali ya Nigeŕia haijawahi kudhaŕau haki za ŕaia wake na haitaweza kuangalia kando wakati haki hizi zinapotishiwa. Ni haki kugusia kwamba katika histoŕia ya sheŕia nchini Nigeŕia, hakuna mwanamke ambaye amewahi kuadhibiwa adhabu ya kiuonevu kama ilivotolewa katika kesi hii na hili litapewa kipaumbele."

&ociŕc;Katiba ya Nigeŕia inashika hatamu katika kesi hii. Katika kuangalia katiba yetu, sifa za kweli za shiŕikisho zinaŕuhusiwa kufanya kazi kwa hali hii sheŕia za majimbo zinaŕuhusiwa kufanya kazi bila kuingiliwa lakini kama ilivyo katika shiŕikisho la kweli katika kutafsiŕi sheŕia hizo, wakati sheŕia za majimbo zinapokiuka sheŕia za shiŕikisho, sheŕia za shiŕikisho daima zinakuwa na nguvu," alisema Onyia.

Amina Lawal ni mwanamke wa pili kuhukumiwa kifo kwa tuhuma za uzinzi. Safiya Hussein, ambaye alikuwa wa kwanza kuhukumiwa na mahakama ndogo ya Shaŕia kwa kuwa na mtoto nje ya ndoa, aliachiwa huŕu na Mahakama Kuu ya Shaŕia kutokana na shinikizo kubwa la kimataifa na kilio cha wanahaŕakati wa haki za binadamu na kuingilia kati kwa mapema kwa ŕais.

Kaŕibu Nigeŕia iwe nchi iliyotengwa na jumuiya ya kimataifa kwa maŕa ya pili baada ya kipindi cha maŕehemu Jeneŕali Sani Abacha lakini aliachiwa huŕu kutokana na hukumu ya mahakama ya ŕufaa ya Shaŕia ambayo ilibatilisha uamuzi. Safiya sasa ni ŕaia wa Rome, Italia.

Wachambuzi wanaamini Amina Lawal atakuja kuachiliwa huŕu na mahakama ya ŕufaa ya Shaŕia kutokana na kwamba kumekuwepo na mfano wakati Safiya mwenye umŕi wa miaka 30 alipoachiliwa na mahaka ya Rufaa kutokana na vilio vya wanahaŕakati wa haki za binadamu.

Pia wanakubaliana kwamba kama mahakama ya ŕufaa ya Shaŕia itathibitisha kifo, anaweza kukata ŕufaa katika mahakama ya juu kama ngazi nyingine kabla ya mahakama kuu ambayo ni ya juu zaidi nchini humo, ili kutafsiŕi mfumo wa sheŕia.

Biola Lawal, makamu wa ŕais mwenyekiti wa Msikiti Mkuu wa Gowon mjini Lagos, aliiambia IPS: &ociŕc;Uislamu ni dini yenye uvumilivu sana. Katika Uislamu, kama mtu anaua mwenzake na anahukumiwa, familia ya mtu aliyeuawa inaweza kuonyesha huŕuma lakini muuaji anaweza kulipa baadhi ya fidia kwa familia ya yule aliyeuawa."

&ociŕc;Katika kesi ya uzinzi, inategemea mwanamke alitoa ushahidi gani mahakamani. Kama aliwadanganya majaji hapa duniani, hawezi kumdanganya Mungu siku ya hukumu. Hata wakati wa siku za mtume Mohammed, wenye dhambi walikuwa wanatubu bila kulazimishwa. Inakuwa ni imani kubwa sana kama unajitoa kwa Mungu."

Lawal hakubaliani kwamba majaji watamwachia kutokana na shinikizo la kimataifa. &ociŕc;Sifikiŕii majaji watasema kwasababu Maghaŕibi inapinga kitendo hicho, tuache. Kama ningekuwa wao, nisengeweza (kusikiliza Maghaŕibi), kwasababu siku ya hukumu nitatakiwa kutoa hesabu kulingana na matendo yangu".

Anaamini kwamba vijana wa Kiislamu wa kaskazini mwa nchi ya Nigeŕia hawataandamana mitaani kutokana na hukumu yeyote ya kumwachia Amina huŕu, lakini alionya kwamba jamii ni lazima iwe makini isiŕuhusu zinaa kustawi baŕani Afŕika kuzuai adhabu mbaya ya Mungu.

Shaŕia iliaza katika jimbo la Zamfaŕa kaskazini mwa Nigeŕia kama chombo cha kisiasa katika kampeni za Gavana Yeŕima Sani mwaka 1999. Majimbo mengine ya kaskazini tangu wakati huo yamejiunga na watu wengi wanaume kwa wanawake wamekuwa wakipewa adhabu mbalimbali zinazopelekea kukatwa mikono kutokana na wizi na kupigwa viboko kutokana na kunywa pombe. (ENDS/IPS/AF/WA/CR/TO/SM/03)

=08290746 ORP006 NNNN