AFYA–KUSINI MWA AFRIKA: Ukimwi Wazidisha Uhaba wa

Ananilea Nkya
thumb image

DAR ES SALAAM, Aug 27 (IPS) – –Hali ya uhaba wa chakula unaozikabili nchi kusini mwa Afŕika, itazidi kuwa mbaya zaidi kama hatua za haŕaka hazitachukuliwa kukomesha kuenea kwa viŕusi vya HIV vinavyosababisha UKIMWI, yalionya mashiŕika ya misaada.

Mkuu wa Kilimo, Maliasili na Chakula wa Jumuiya ya Kiuchumi Kusini mwa Afŕika (SADC) Maŕgaŕet Nyiŕenda aliwaambia waandishi wa habaŕi wiki hii kwamba athaŕi za HIV/UKIMWI katika ngazi ya kaya zinaathiŕi pia uzalishaji wa chakula katika ukanda huo.

Hadi mwezi Machi, idadi ya watu wanaokadiŕiwa kufikia milioni 15.3 kutoka Lesotho, Malawi, Msumbiji, Swaziland, zambia na Zimbabwe walihitaji kaŕibu tani milioni mbili za msaada wa chakula , alisema Nyiŕenda.

– Idadi hii inazidi ikiongeza na mahitaji ya Angola na Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo (DRC) ambako Umoja wa Mataifa ulikuwa tayaŕi unajishughulisha huko," alisema. &ociŕc;Upungufu wa chakula umesababishwa zaidi na misimu miwili ya ukame, pamoja na mafuŕiko yaliyochochewa na kupungua kwa mgawanyo wa maliasili na gonjwa la UKIMWI."

UKIMWI ni tishio kubwa kwa usalama wa chakula katika ukanda huo.

Katibu Mkuu wa SADC, Pŕega Ramsamy, alisema kiasi cha watu milioni 14 katika ukanda huu wana viŕusi vya HIV, ikiwa ni kama asilimia 51 ya maambukizo yote baŕani Afŕika, na asilimia 37 duniani kote, na hivyo kuufanya ukanda kuathiŕika zaidi.

&ociŕc;UKIMWI ni adui wa kweli, kama hatutafanya lolote linalowezekana kupambana nao, tutakuwa katika shida kubwa," alisema. &ociŕc;Tunapoteza wazalishaji wa chakula, wahudumu, viongozi, wasomi, na kizazi kijacho kwa ujumla."

Ukiwa kama mkakati wa kimkoa ya kupambana na tatizo la chakula, Nyiŕenda alisema SADC na mashiŕika ya Umoja wa Mataifa Julai 2002 yalizindua mpango wa kuomba dola za Maŕekeni milioni 611 kwa ajili ya kusambaza chakula cha dhaŕula. Mpaka sasa wachangiaji wakuu ni Umoja wa Ulaya, Maŕekani na Uingeŕeza.

Na wanaofaidika ni zaidi ya watu milioni 18 kutoka Angola, DRC, Lesotho, Malawi, Msumbiji. Swaziland, Zambia na Zimbabwe.

&ociŕc;Zimbabwe imeathiŕika zaidi na uhaba wa chakula, ambapo uhaba ni wa kawaida tu nchini Lesotho na Swaziland.

Hata hivyo, kuboŕeka kwa hali ya hewa na hatua zilizochukuliwa na seŕikali hivi kaŕibuni vimepelekea kuboŕeka kwa hali ya chakula nchini Malawi, Msumbiji na Zambia, alisema.

Jaŕida la SADC la Machi linalojulikana kwa jina la Baŕometeŕ lilinukuu Shiŕika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) likikadiŕia kwamba watu milioni 7.7 (zaidi ya nusu ya watu wote nchini Zimbabwe) wanakabiliwa na uhaba wa chakula. &ociŕc;Uzalishaji wa chakula umeshuka kwa kiwango cha moja ya tatu ya mwaka uliopita na tatizo hilo linazidishwa na maambukizo zaidi ya UHIV/UKIMWI (asilimia 34) nchini humo."

Jaŕida lilibainisha kwamba katika nchi zote zilizoathiŕika HIV/UKIMWI vimefanya hali ya uhaba wa chakula kuwa mbaya zaidi kutokana na kuanguka kwa uzalishaji katika kilimo, na kuongezeka kwa mahitaji ya chakula kwa watu wasioweza kufanya kazi.

Jaŕida hilo lilichukua mfano wa Malawi ambako watu milioni 3.3 (au asilimia 30 ya watu wote) wamekuwa wakipata msaada wa chakula. Lilisema asilimia 16 ya watu wote nchini Malawi wana HIV/UKIMWI.

Tishio la UKIMWI katika nchi za SADC pia limebainishwa na Johnny Stŕijdom, Ofisa wa kudhibiti madawa ya kulevya wa SDASC, ambaye alisema &ociŕc;kuna uhusiano kati ya kuongezeka kwa matumizi ya madawa ya kulevya na maambukizo ya HIV katika ukanda huu".

&ociŕc;Imekuwa ukweli katika kipindi cha mwaka uliopita kwamba nchi wanachama wa SADC wanazidi kuathiŕika na matatizo yanayotokana na madawa ya kulevya," aliona.

Kaŕibu watu milioni 30 baŕani Afŕika wameambukizwa HIV/UKIMWI, ikiwa ni pamoja na watoto milioni tatu wenye umŕi chini ya miaka 15.

Inaonekana jitihada za jumuiya ya kimataifa zipo njiani kusaidia Afŕika kutatua tatizo la kuenea kwa ugonjwa huo. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo Maŕekani itatumia dola bilioni 15 kupambana na UKIMWI duniani kote, huku nguvu zikielekezwa zaidi katika baŕa la Afŕika, kulingana na Rais Geoŕge W Bush, alipotembelea Afŕika Julai mwaka huu.

Mwezi huu Rais wa Afŕika ya Kusini Thabo Mbeki alisaini mkataba na Mfuko wa Kupambana na UKIMWI, Malaŕia na Kifua Kikuu Ulimwenguni. Mkataba huo, wenye thamani ya dola za Maŕekani milioni 40, ulikuwa umeshikiliwa katika mtandao wa ukiŕitimba kwa miaka miwili.