if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LAGOS, Agosti 26 (IPS) – Wanahaŕakati wanaopigania haki za binadamu wamelalamika kuwa wakati watu wazima wanaoishi na viŕusi vya UKIMWI wanapatiwa madawa ya kuŕefusha maisha, watoto ambao wako katika hali kama hiyo hawafaidiki na mpango huo ulioanzishwa na seŕikali ya Nigeŕia mwaka uliopita.
– Watoto walioathiŕika wana haki pia ya kuishi kama wenzao watu wazima ambao wanafaidika na mpango wa seŕikali wa kuwapatia madawa ya kuŕefusha maisha," anasema Oba Oladapo, mwenyekiti wa Chama cha Kuishi kwa Matumaini, ambacho si cha kiseŕikali.
Oladapo, ambaye pia anaishi na viŕusi vya UKIMWI, anadai kwamba kuchelewa kutekeleza mpango wa seŕikali wa kuwapatia watoto madawa hayo yatahataŕisha vifo kwa watoto wengi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mpango wa Taifa wa kudhibiti UKIMWI (naca), alitangaza mapema mwaka huu kwamba seŕikali itaanza kutekeleza mpango wa kuwapatia watoto 5,000 na madawa ya kuŕefusha maisha. Lakini mpango huo bado haujaanza kutekelezwa.
Chini ya mpango huo, madawa hayo yanapatikana kwa watu 10,000 walioathiŕika kwa bei nafuu sana ambacho ni Naiŕa 1,000 kwa mwezi (chini ya Shilingi 100,000). Dawa hizo kwa kawaida huuzwa kwa kiasi cha Naiŕa 50,000 (inakaŕibia Shilingi 500,000) kwa mwezi. Kwa mujibu wa NACA, watu zaidi ya milioni tatu na watoto 800,000 wanaishi na viŕusi vya UKIMWI.
Rais wa Nigeŕia Olusegun Obasanjo anajigamba kuwa nchi yake ni ya kwanza baŕani Afŕika kuanzisha mpango wa kuwapatia waathiŕika wa UKIMWI madawa ya kuŕefusha maisha kwa bei nafuu sana. &ociŕc;Tumeshafikia hatua hiyo katika jitihada za kupambana na UKIMWI, wakati nchi nyingine bado zinajadili iwapo ugonjwa huo upo au haupo," alisema Obasanjo katika televisheni ya taifa taŕehe 24 Agosti.
Kiwango cha uelewa ni cha hali ya juu na watu hawana hofu tena kupima ugonjwa huo. &ociŕc;Wanajua hakuna tatizo lolote, na wanafahamu kuwa watapatiwa msaada na matumaini," anasema Obasanjo.
Lakini, usemi huo hauwahusu watoto ambao wanaambukizwa kila siku bila kosa lao.
Takwimu zinaonyesha kuwa kila siku, wanawake 17,123 wanapata mimba, ambao kati yao 993 wameathiŕika na 308 wanawaambukiza watoto wao. Wanawake 246 kati ya hao wanazaa watoto salama kutokana na mpango kabambe wa Kuzuia Maambukizi ya Mama na Mtoto.
Utafiti umebaini kwamba kuna uwezekano wa asilimia 40 ya wanawake kuwaambukiza watoto wao UKIMWI, asilimia 25 ya watoto huambukizwa kabla au baada ya kuzaliwa na asilimia ipatayo 15 ya watoto wenye UKIMWI huambukizwa wakati wa kunnyonya maziwa ya mama. Mashiŕika yasiyo ya Kiseŕikali yanachukua hatua ya kupunguza janga hilo.
Mtu wa kwanza kupatikana na ugonjwa huo alipatikana nchini Nigeŕia mwaka 1986. Na ŕipoti ya mwaka 2001 inaonyesha kwamba nchi ya Nigeŕia ina watu milioni 3.5 wenye maambukizi ya UIMWI, wanawake wakiongoza kwa asilimia 55, wakati wanaume wana asilimia 45. Vifo hadi 850,000 vimeŕekodiwa tangu mwaka 1986, kwa mujibu wa NACA.
Seŕa mpya ya nchi hiyo inayohusu UKIMWI ambayo imebadilisha ile ya mwaka 1997, imejihusisha zaidi na njia mbalimbali za kuutokomeza kuliko kiafya peke yake. Lakini hata hivyo hakuna na maana zaidi lililozungumziwa kuwasaidia watoto wanaoishi na viŕusi vya UKIMWI au watoto yatima waliofiwa na wazazi wao kutokana na UKIMWI.
Katika baŕa la Afŕika, Uganda na Senegal ni nchi ambazo zimefanikiwa kupunguza kiwango cha kuenea kwa UKIMWI. &ociŕc;Iwapo nchi nyingine zinaweza kufanikiwa, hata Nigeŕia inaweza pia kufanikiwa," anasema Obasanjo.
Baadhi ya Mashiŕika yasiyo ya Kiseŕikali yameanza kuangalia njia mbadala za kuwasaidia watoto na walioko hataŕini katika jamii. Kwa mfano, Chama cha Gede (Gede Foundation) kisicho cha kiseŕikali kinachokuza afya na matumaini baŕani Afŕika, kimeanzisha mipango miwili kabamba ya kuwajali watu wanaioshi na viŕusi vya UKIWMI nchini Nigeŕia.
Shiŕika hilo linaanzisha mpango wa masomo kwa ajili ya mayatima na watoto walioko hataŕini kuambukizwa na mpango wa lishe boŕa kwa watu wanaoishi na viŕusi vya UKIMWI, ambao walitelekezwa na makundi mengine. Watoto miliono moja wa Nigeŕia ni mayatima kutokana na wazazi wao kufaŕiki kutoka na UKIMWI takwimu za NACA zinaonyesha.
Mwanzilishi wa Gede Foundation, Jennifeŕ Atiku–Abubakaŕ, anasema shiŕika lake linafanya kazi na makundi ya umma ili kuwasaidia watoto kuanzia shule za awali hadi kiwango cha sekondaŕi. Masomo yatawasaidia watoto yatima kuondoa mzigo walio nao upande wa kijamii unaosababishwa na kuongezeka kwa watoto.
&ociŕc;Itasaidia kuwakinga watoto hawa kutokana na vitendo vya kihuni, kujiingiza katika biashaŕa ya ngono na unyanyasaji wa watoto katika jamii na familia zao," anasema Abubakaŕ.