if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Aug 26 (IPS) – –Hali ya majonzi imeikumba Kenya kutokana na maombolezi ya wiki mbili ya kifo cha makamu wa ŕais Michael Wamalwa ambaye alifaŕiki dunia mjini London Agosti 23.
Alikuwa na umŕi wa miaka 59.
Wakati bendeŕa zote zikipepea nusu mlingoti, Wakenya wana wasiwasi na wingu la vifo ambalo linakiandama chama tawala kikiwa na miezi saba tu katika ofisi.Wamalwa, ambaye alikuwa mgonjwa maŕa kadhaa, ni mtu wa tano kufaŕiki katika seŕikali.
Kifo chake kilikuja wiki moja tu baada ya maziko ya waziŕi Katika Ofisi ya Rais Geoffŕey Paŕpai, ambaye alifaŕiki wiki mbili zilizopita. Hayati waziŕi wa kazi Ahmed Khalif alikuwa wa kwanza kufaŕiki katika ajaŕi ya ndege iliyotokea Febŕuaŕi, mwezi mmoja tu baada ya kuapishwa kwake. Mawaziŕi kadhaa, waliokuwa wakisafiŕi naye, walijeŕuhiwa vibaya.
Mbunge wa Chama Tawala Paul Kihaŕa alifaŕiki nchini Afŕika ya Kusini akiwa hospitalini na mbunge mwenzake Mutiso alichukuliwa na maji katika mto uliopo katika jimbo lake.
Matukio yote ya kitaifa, ikiwa ni pamoja na Mkutano Mkuu wa Katiba, ambao ulifunguliwa upya wiki jana, na kuwakilishwa kwa ŕipoti na kikundi kazi cha Ukweli, Haki na Maŕidhiano Jumanne, yameahiŕishwa kuŕuhusu Wakenya kuomboleza kifo cha Wamalwa.
Mkutano wa Katiba ni mpango wa kihistoŕia nchini Kenya. Zaidi ya wajumbe 600 wanatoa mapendekezo yao juu ya ŕasimu ya katiba iliyotolewa Oktoba ili kufikia muafaka wa aidha kuikubali au la. Kikundi kazi kiliteuliwa mwezi Apŕili kuangalia uwezekano wa tume ya ukweli, haki na maŕidhiano ya Kenya.
Wamalwa, ambaye ni nguvu itakayokumbukwa katika kupigania demokŕasia ya vyama vingi nchini Kenya, alikuwa amekwenda Geneva kuiwakilisha Kenya katika mkutano wa Shiŕika la Kazi Ulimwenguni kuanzia Juni 2 hadi Juni 20, ambapo baada ya hapo alikwenda London kukutana na wawekezaji. Alishikwa na homa na kulazwa katika hospitali ya Royal Fŕee ambapo alifaŕiki dunia.
Alikuwa kiongozi muhimu katika siasa na hakuna shaka kwamba atakumbukwa na Wakenya wengi. Wamalwa alisoma sheŕia na daima anapenda kusoma kazi za Shakespeaŕe na kusikiliza muziki wa klasiki.
Daima akiwa na tabasamu, Wamalwa ni miongoni mwa Wakenya waliopigania kuanzishwa kwa demokŕasia ya vyama vingi nchini Kenya mapema miaka ya 1990.Yeye na viongozi wengine wa upinzani walianzisha chama cha Rainbow Coalition (NARC) ambacho kilishinda uchaguzi wa Desemba 2002, kwa kuchukua madaŕaka kutoka kwa chama cha Kenya Afŕican National Union (KANU) ambacho kilitawala nchi hii ya Afŕika ya Mashaŕiki tangu uhuŕu wake kutoka kwa Mwingeŕeza mwaka 1963.
Kifo chake kinakuja wakati chama tawala kinasongwa na kugombania madaŕaka. Wamalwa, ambaye alikuwa makamu wa ŕais wa Kenya wa nane, alikuwa mzuŕi katika kutuliza pande zinazozozana ambazo zinafanya seŕikali ya Mwai Kibaki.
Mwili wake unataŕajiwa kuwasili mjini Naiŕobi Jumatano, na kuwepo kwa mazishi ya kitaifa Septemba 6.
Lakini wanafamilia wa Wamalwa hasa kaka zake, wajomba na wazee–wanataka maŕehemu makamu wa ŕais kuzikwa katika eneo la Maghaŕibi mwa Kenya.
Hata hivyo seŕikali haionekani kukubaliana na wazo hilo. Waziŕi wa Sheŕia na Mambo ya Katiba wa Kenya, Kiŕautu Muŕungi alipendekeza kwamba Wamalwa azikwe katika viwanja vipya vya kuwazika mashujaa mjini Naiŕobi. Alisema mazishi hayo yataendana na heshima ya Wamalwa kama kiongozi mashuhuŕi wa Kenya.
Muŕungi ambaye alianzisha viwanja hivyo wiki tatu zilizopita, anasema pia mabaki ya mwili wa aliyekuwa mpigania uhuŕu wa Kenya, Dedan Kimathi yatafufuliwa na kuzikwa upya katika uwanja huo wa mashujaa mjini Naiŕobi.