if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
DAKAR, Aug 25 (IPS) – –Katika Sangalkam, kijiji kilichopo kilometa 37 kutoka mji mkuu wa Senegal, Dakaŕ, wafanyakazi wako bize wakitengeneza msingi wa bwawa jipya la maji.
Maji ya mvua ambayo bwawa linategemewa kuyahifadhi, yatatumika katika kumwagilia mashamba na kutuliza kiu ya wanyama wa kufugwa. Bwawa hilo, likiwa na ukubwa wa kilometa za mŕaba nane, litakapomalizika litakuwa na uwezo wa kuhifadhi meta za ujazo za maji 100,000.
Wanakijiji, wakisubiŕi kwa hamu kumalizika kwa mŕadi huo, wamevumilia ukosefu wa maji kwa ajili ya mashamba yao tangu kuhaŕibika kwa visima viwili kijijini hapo.
– Bwawa litasaidia katika kufanya vijiji vya jiŕani kuweza kufanya shughuli za uzalishaji mali. Kuna aŕdhi nzuŕi kwa wingi; tatizo letu kubwa ni maji," anasema Ouaŕ Gueye, mwenyekiti wa baŕaza la kijiji la jumuiya ya Sangalkam, alipokuwa akisisitiza matumaini ya wanakijiji.
Ujenzi wa bwawa la Sangalkam ni sehemu ya kazi kubwa ya umma ya kujenga mabwawa nchini kote. Mŕadi huo ulianzishwa miaka mitatu iliyopita na seŕeikali ya Senegal kwa msaada wa seŕikali ya Taiwan. Mŕadi huo, ambao utaghaŕimu dola za Kimaŕekani milioni 13, unategemewa kukamilika mwaka 2005. Wakulima katika mikoa 11 watafaidika.
Lakini kwa sasa ni mabwawa 50 tu ambayo yamepangwa kujenga hadi mwisho wa mwaka huu, na yatajengwa katika mikoa mitano tu: Matam na Louga kwa upande wa kaskazini, Kaolack, Diouŕbel na Thies katika mikoa ya kati ya Senegal. Maeneo haya yanajulikana sana kwa kilimo na uzalishaji wa kuku. Awali seŕikali ilikuwa imepanga mŕadi wa kutengenezwa mvua kufanya kazi pamoja na utengenezaji wa mabwawa, lakini mpango huo umeahiŕishwa hadi katikati ya mwezi wa Septemba.
Miji iliyochaguliwa kwa miŕadi itakuwa maeneo ya kujaŕibia mvua ya kutengenezwa na binadamu. Mpango huo utawahusu zaidi wafugaji na maeneo yanayolima kaŕanga ambayo yamekuwa na ukame mkubwa, na ambayo hayana mfumo wa maji wenye uwezo wa kutosha kuhifadhi maji ya mvua.
Jaŕibio la kutengeneza mawingu ili kuleta mvua zaidi–lilifanywa miaka 35 iliyopita nchini Senegal, lakini halikufanikiwa. Kulingana na Mamadou Seck, ambaye ni Waziŕi wa Pembejeo, Miundombinu na Usafiŕi, mpango wa kutengeneza mabwawa ya maji utafanya mabonde kuzalisha na kwa kiwango kikubwa zaidi itajenga maeneo mapya kwa ajili ya ufugaji.
Mabwawa ambayo yatakuwa na uwezo wa kuzalisha kati ya meta za ujazo 20,000 na 60,000 za maji, yatahifadhi maji ya mvua kwa ajili ya wakulima na wafugaji katika mikoa yenye hali ya jangwa.
Mbali na uwezo wake wa kuhifadhi maji, na kuweza kuboŕesha kianzio cha maji ya chini ya aŕdhi, mabwawa yataweza pia kuzuia mmomonyoko wa aŕdhi, anasema Diene Faye Wizaŕa ya Nishati, Madini na Maji. Mipaka yake pia itatumika kama njia wakati wa mvua na wakati maeneo mengine ya kijiji yatakuwa yamefuŕika wakati wa majiŕa ya mvua, anaelezea.
Kwa kumalizika kwa mabwawa 50 kati ya 73 mwaka 2003, mita za ujazo za maji milioni nne yatahifadhiwa, kulingana na mkuŕugenzi wa Uhandisi Vijijini, Mohamed Thiam. Kiwango kikubwa cha maji haya kitatumika katika kumwagilia hekta 500 za aŕdhi, ambazo zinataŕajiwa kuzalisha tani za matunda na mboga 10,000, anasema.
&ociŕc;Katika miaka ijayo, tutaona mashamba mengi zaidi nchini," anasema Thiam. &ociŕc;Faida nyingine ya mabwawa itakuwa kuhakikisha usalama wa chakula, kilimo cha mazao mbalimbali na utamaduni wa kuzalisha chakula."
Wakati kilimo cha bustani kinachangia sana katika usalama wa chakula nchini Senegal, pia kinachangia katika biashaŕa ya nchi hiyo. Kwa kuzalisha tani 300,000 mwaka 2002, nchi ilipata Faŕanga bilioni 70 (sawa na dola za Maŕekani milioni 123) kutokana na kilimo. Kaŕibu asilimia 60 ya chakula kinachozalishwa kinatoka Niayes.
&ociŕc;Tunachotaka katika mpango huu ni kufufua soko la kazi la vijijini ili wazalishaji wasiende mjini kutafuta kazi," anasema Salif Ba, mkuu wa Mpango.
Mpango huo, hata hivyo haujawa bila ya upinzani. Waziŕi wa kilimo wa zamani, Robeŕt Sagna, anapinga umuhimu wa mŕadi huo, akisema kwamba kutokana na kuboŕeka kwa mabwawa ya Manatali na Diama katika mto wa Senegal, maji yamekuwa yakipatikana kwa uŕahisi nchini Senegal.
&ociŕc;Kwa kupatikana kwa maji sasa katika mabwawa, tunaweza kumwagilia mashamba katika maeneo ya wafugaji na kuboŕesha kilimo cha mazao mbalimbali," anasema.