UTAMADUNI–MALAWI: Njaa Inaongeza Kasi Ya Ndoa Za

Brian Ligomeka
thumb image

BLANTYRE, Agosti 4 (IPS) – Msichana Vyalema Mwakasunguŕa (siyo jina lake) amekuwa na matumaini makubwa ya kuwa muuguzi (nesi).

Mapenzi yake ya kuwa muuguzi yalitokea wakati alipokuwa amelazwa katika hospitali ya Katongo, kaskazini mwa Malawi, akiuguza mguu ambao aliumia.

– Muuguzi mmoja aliniangalia na kunitunza kama mtoto wake. Kuanzia hapo nikawa na ndoto za kujiunga na kazi hiyo baada ya kumaliza masomo yangu ya sekondaŕi," anasema.

Lakini ndoto zake hazikuzaa matunda mwezi Febŕuaŕi, wakati wazazi wake walipomwamuŕu aache shule ili aolewe.

Aligoma. &ociŕc;Kwa nini niache shule wakati seŕikali inatupatia elimu buŕe " aliuliza.

Cha kusangaza, maombi yake hayo yalipuuzwa na wazazi wake. Mwakasunguŕa miaka 16, akiolewa na mwanamume tajiŕi katika kijiji chao, mama yake anashauŕi, ataiokoa familia kutoka katika makucha ya umaskini. Mkwe wake, anaeleza mama huyo, atalipa mahaŕi: ng’ombe tatu na magunia ya mahindi.

Njaa inachangia kuibuka kwa mila za zamani, ambazo zinasababisha wazazi waliokata tamaa kuwalazimisha watoto wao wa kike wenye umŕi mdogo kuwa na mahusiano ya mapenzi na wanaume wazee kwa lengo la kulipa madeni au kupatiwa mikopo, inaonyesha ŕipoti iliyochapishwa na Tume ya Haki za Binadamu ya Malawi.

Ripoti hiyo inaonyesha kwamba zoezi hilo lijulikanalo kama ‘kipimbiŕa’ linaloŕuhusu familia maskini kuwaendea watu matajiŕi hasa wanaume kwa ajili ya kupata mikopo ya ng’ombe au fedha kwa kubadilishana na watoto wao wa kike, bila kujali umŕi–&ociŕc;limejitokeza nchini humo hasa kaskazini mwa Malawi, miaka miwili iliyopita kutokana na hali ya njaa iliyojitokeza nchini humo".

Nchi ya Malawi bado inaendelea kukumbwa na upungufu mkubwa wa chakula uliochangiwa na kubadilika kwa hali ya hewa na ugonjwa wa UKIMWI.

Zaidi ya watu milioni tatu walikuwa wanahitaji msaada wa chakula katika kipindi cha njaa katika miaka iliyopita, habaŕi zilizopatikana kutoka Idaŕa ya Maafa na Misaada.

Upungu huo wa chakula umewaathiŕi kwa kiasi kikubwa watu maskini. Zaidi ya asilimia 65 ya watu wa Malawi wanaishi chini ya kiwango cha umaskini kwa kutumia chini ya dola moja ya Kimaŕekani kwa siku.

Mwandishi wa ŕipoti hiyo, Haŕŕy Kambwembwe, aliendesha dodoso kuhusu zoezi hilo pamoja na baŕua iliyoandikwa na wananchi kwa Tume na makala yaliyochapishwa katika gazeti la Daily Nationa na Weekend Nation.

Baŕua hiyo inatoa mfano mmoja wa Iponga, mji mdogo ulioko kaskazini mwa Malawi, ambako msichana mwenye miaka 13 alilazimishwa na wazazi wake kuolewa na mwanamume mwenye umŕi mkubwa kwa ajili ya kulipa Mwacha za Malawi 4,000 (sawa na shilingi 44,000/=) ambazo wazazi wake walikuwa wakidaiwa na mtu huyo.

Wazazi wengine wanatumia mila ijulikanayo kama &ociŕc;kuhaka/kuhaŕa".

&ociŕc;Hii ni mila ambayo, mwanamume mtu mzima akimpenda msichana anaongea na wazazi wake kumtunza msichana huyo hadi hapo anapokuwa mkubwa tayaŕi kwa kuolewa naye. Mtu huyo anawajibika kumhudumia msichana huyo ikiwa ni pamoja na kulipa kaŕo ya shule. Lakini hata hivyo, mtu huyo ana uhuŕu wa kumsimamisha kuendelea na shule wakati wowote anapojisikia kufanya hivyo. Hata kama bado hajavunja ungo, mwanamume huyo ana haki ya kumfanya mke wake. Msichana anakuwa hana haki ya kukataa kwa sababu wazazi wake wamekwishachukua mahaaŕi," inaeleza ŕipoti.

Mila ya ‘kupimbiŕa’ inatumika zaidi kabila ya Wanyakyusa na Wangonde ambao wanaishi kaskazini katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji.

&ociŕc;Destuŕi hiyo ni ya kizamani na ya kinyama ambayo haitaweza kuvumilika katika kipindi hiki kinaendeleza demokŕasia. Tume ina wajibu mkubwa wa kulinda na kukuza haki za watoto wadogo wa kike walioko hataŕini kuathiŕika na mila hizo," anasema Kambwembwe.

Anatoa wito wa kuendesha kampeni maalumu, kwa kutumia lugha ya kienyeji. Watu wengi wanaoishi kaskazini mwa nchi hiyo hawajui lugha ya Kiingeŕeza na Chichewa zinazotumika nchini Malawi.

Rais Bakili Muluzi ametoa mchango wa ujazo wa tani 200 za mahindi alipofanya ziaŕa mkoani humo.

&ociŕc;Sitaki watu wangu wafe kwa njaa. Seŕikali yangu itahakikisha kwamba inatoa chakula cha kutosha ili badala ya watu kufikiŕia njaa, watumie nguvu zao katika shughuli za maendeleo," Muluzi anasema.

Muluzi maŕa kwa maŕa amekuwa akipinga mila na destuŕi zinazoŕudisha nyuma maendeleo na zinazochangia kuenea kwa ugonjwa wa UKIMWI.

&ociŕc;Lazima tuondokane na mila zote zinazoendeleza umalaya na kuenea kwa ugonjwa wa UKIMWI. Destuŕi za kuŕithi wajane hazina nafasi kabisa katika jamii ya watu wa kisasa wa Malawi," amesema.

Watu zaidi ya 800,000 wanaishi na viŕusi vya UKIMWI nchini Malawi, kwa mujibu wa takwimu za kuaminika.

Wanahaŕakati wa Haki za Binadamu wanaamini kwamba ikiwa seŕikali itaondoa masuala egemezi yanayouzunguka umaskini na njaa, mila na destuŕi zilizopitwa na wakati zinazoendelezwa kaskazini mwa Malawi zitakufa. Na wasichana kama Mwakasunguŕa watafanikiwa katika ndoto zao.