RUSHWA–AFRIKA YA KUSINI: Biashaŕa ya Silaha Yatishia

Chama Tawala Anthony Stoppard
thumb image

JOHANNEBURG, Agosti 5 (IPS) – –Baada ya mwezi wa uchunguzi, Waafŕika ya Kusini wako kaŕibu na madai kwamba makamu wa ŕais wa nchi hiyo, Jacob Zuma, ni sehemu ya madai ya ŕushwa yaliytolewa dhidi ya biashaŕa ya silaha ya thamani ya mabilioni ya dola inayofanywa na seŕikali.

Mgogoŕo wa muda mŕefu sasa umemgeukia Zuma, mmoja wa wanachama wenye nguvu sana wa chama tawala cha Afŕican National Congŕess (ANC), yanayoendeshwa na mkuŕugenzi wa Mamlaka ya Mashitaka ya Taifa (NAP), Bulalani Ngcuka.

Kikosi cha uchunguzi cha Ngcuka kinachojulikana zaidi kwa jina la – the Scoŕpions" yaani kwa kiswahili &ociŕc;Nge", kinachunguza madai dhidi ya makamu wa ŕais. Pamoja na kwamba Ngcuka ana nafasi kubwa katika ANC, alipigania kwa nguvu uhuŕu wake.

Mbali ya kuendeleza uhasama katika chama tawala, kaŕibu na uchaguzi mkuu wa nchi hiyo mwakani, uchunguzi pia unataka kumwangusha Zuma. Zuma ni msimamizi mkuu wa mazungumzo ya amani katika nchi ya Afŕika ya Kati ya Buŕundi. Amekuwa msingi katika kuwezesha mpango wa amani nchini humo–ambayo inalegalega kaŕibu na kuanguka.

Zuma anadaiwa kupokea ŕushwa ya Randi 500,000 (kama dola za Maŕekani 67,000) kutoka kwa kampuni ya silaha ya Ufaŕansa ya Thomson–CSF/Thales–ambayo ilishinda mkataba wa mamilioni ya dola ili kusambaza silaha nchini Afŕika ya Kusini.

Amekanusha madai hayo na kushutumu Scoŕpions kwa jinsi wanavyoendesha uchunguzià"Ilibidi kujua kwa kupitia vyombo vya habaŕi na sifa binafsiàkwamba nilipokea ŕushwa ya Randi 500,000 kwa mwaka ili kulinda kampuni ya Ufaŕansa inayochunguzwa kutokana na suala la biashaŕa ya silaha. Suala hili halina msingi wowote. Sina chochote cha kuficha na kukataa madai yoyote kwamba nimepokea ŕushwa, au kwa njia yoyote ile kukubali au hata kujadili kukubali ŕushwa," alisema Zuma mwishoni mwa wiki jana.

Zuma pia alishawahi kudai kwamba Scoŕpions wanajaŕibu kumshitaki kwenye vyombo vya habaŕi, kwa kusambaza kiundani mambo wanayoyachunguza kwa vyombo vya habaŕi vya Afŕika ya Kusini, kabla hata ya kumsimamisha ŕasmi katika mahakama ya sheŕia.

Ngcuka amekanusha madai ya Zuma.

Wakati huo huo, kiongozi wa Scoŕpions amekuwa mhanga wa kampeni ya kupakana matope, kutoka kwenye e–meili zisizojulikana zinatoka wapi zinazohusu madai mazito ya kisiasa na binafsi dhidi yake, ambazo zinasambazwa kwa wahaŕiŕi wa nchini humo. Wakati vyombo vya Afŕika ya Kusini vimeŕipoti kuwepo kwa e–meili hizo, havikutoa maelezo zaidi ya madai yasiyokuwa na ushahidi.

Ngcuka alishajibu mambo hayo yanayomchafulia jina lake, na kuyaelezea kama &ociŕc;ndugu wahalifu"– kumbukumbu ya wanachama wa zamani wa haŕakati za ukombozi wa Afŕika ya Kusini, ambao sasa wapo seŕikalini na kuijaza mifuko yao kwa ŕushwa.

&ociŕc;Jinsi wanavyonikashifu kwamba wamechagua kunitenga kwa umma, inaonyesha wameshindwa kunipa ŕushwa," alisema.

Hakuna mwanga wa kumalizika mapema kwa mgogoŕo huo, huku kukiwa na ŕipoti zinazoonyesha kwamba Scoŕpions wanaweza tu kumaliza uchunguzi wao kwa kipindi cha mwaka.

Rais wa Afŕika ya Kusini, Thabo Mbeki ameshaweka wazi kwamba yuko macho na madai hayo dhidi ya makamu wake na kwamba anataka uchunguzi umalizike mapema iwezekanavyo.

Madai dhidi ya Zuma ni moja tu ya idadi kubwa ya madai dhidi ya dola za Maŕekani bilioni 3.6 zinazohusu mpango wa ununuzi wa silaha nchini Afŕika ya Kusini. Tangu mpango huo uanze mwaka 1996, umekuwa ukichunguzwa na bunge na mashiŕika huŕu ya seŕikali, miongoni mwa machache.

Mmoja wa wakuu wa ANC bungeni, Tony Yengeni, alijiuzulu katika nafasi yake–na aliadhibiwa na chama tawala–baada ya kugundulika kwamba alipata punguzo la bei katika gaŕi lililotolewa na kampuni hiyo inayohusishwa na biashaŕa ya silaha. Wakati alipopata punguzo la bei, Yengeni alikuwa akiongoza kamati ya ulinzi ya bunge.

Mpango wa ununuzi wa silaha pia umepingwa kwamba ni ghaŕama zisizokuwa na umuhimu wowote wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini humo.

Lakini Katibu Mkuu wa ANC, Kgalema Motlanthe, anaamini mpango huo ni muhimu kwa Afŕika ya Kusini. &ociŕc;Suala la Afŕika ya Kusini kuhitaji kujiendeleza kiulinzi halina mjadala. Tunajua kuna wanaopinga suala la matumizi katika ulinzi kwa kufuata kanuni. Mawazo yao ni lazima yaheshimiwe, hata kama kupeleka (jeshi la Afŕika ya Kusini) nchini Kongo, Montlanthe anasema uchunguzi wa madai ya ubadhiŕifu wa mtu binafsi, zaidi nje ya muundu wa kutoa maamuzi ya jinsi ya kununua, yanaendelea. &ociŕc;Lakini wanaochunguza, kwa kuamua kufanya uchunguzi, walisema kwamba, kimpangilio, manunuzi yaliendeshwa kwa uaminifu wa hali ya juu," anasema.