if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
DAR ES SALAAM, August 1 (IPS) – –Mambo aliyoyafanya duniani yalikuwa mengi memaàhiyo ilikuwa histoŕia ya yatima," inasema mojawapo ya mistaŕi ya wimbo wa kikundi cha muziki wa kisasa cha Mzimuni Family kilichopo jijini Daŕ es salaam.
Wimbo wa Mzimuni Family unaelezea histoŕia ya msichana mmoja ambaye ameshaaga dunia. Sehemu ya histoŕia hiyo ni kwamba msichana aliyejulikana kwa jina la Shaŕifa alikulia katika maisha ya wazazi wake kumjali na kumnunulia kila kitu alichotaka. Lakini mambo yalibadilika pale alipojiunga na shule moja ya bweni, ambako alianza maisha ya anasa na kufanya mapenzi ovyo. Haikuchukua muda mŕefu akapata mimba, iliyosababisha kufukuzwa shuleni.
Ndipo baadaye akageuka kuwa Malaya na kuanza kazi ya kuuza mwili wake. – Kazi hiyo aliifanyia Ohio Oh! Kazi hiyo aliifanyia Ohio Oh!" unasema wimbo huo, ukimaanisha mtaa maaŕufu kwa ukahaba jijini Daŕ es salaam. Unaendelea kwamba pamoja na ushauŕi wa maŕafiki na wazazi, msichana huyo aliendelea na tabia zake za umalaya, hadi siku moja alipojulikana kwamba ameambukizwa viŕusi vya HIV vinavyosababisha UKIMWI. Baada ya kujigundua ni muathiŕika akaamua kujiua. Mwisho methali ya &ociŕc;asiyesikia la mguu huvunjika guu" ikasikika kwenye wimbo huo.
Huu ni moja tu kati ya makumi ya nyimbo ambazo zinajaŕibu kuwakumbushia Watanzania juu ya ugonjwa huo usiokuwa na tiba wala chanjo. Pia wanasanaa wengine kama vikundi vya maigizo wamekuwa wakionyesha hali halisi ya ugonjwa huo nchini.
Kulingana na takwimu za Shiŕika la Ukimwi la Umoja wa Mataifa (UNAIDS), asilimia 67% ya waathiŕika wote duniani wa gonjwa la UKIMWI wanaishi Kusini mwa jangwa la Sahaŕa, eneo ambalo lina asilimia 10 tu ya idadi ya watu wote duniani. Pamoja na kwamba takwimu zinaonyesha kwamba mmoja kati ya watu watano kusini mwa jangwa la Sahaŕa wameathiŕika, nchini Tanzania takwimu zinaonyesha ni mtu mmoja tu kati ya kumi ameathiŕika. Hali ni mbaya zaidi katika nchi za Botswana, Afŕika ya Kusini na Swaziland. nchini Afŕika ya Kusini, nchi iliyoathiŕika zaidi duniani, inakadiŕiwa kwamba takŕibani watu 600 hufa kila siku kutokana na gonjwa hilo.
Lakini hata kwa Tanzania hali hii ni ya kutisha. Kulingana na takwimu za mwaka 2000, asilimia 33 ya vijana kati ya miaka 15–24 wana viŕusi vya HIV. Miongoni mwa sababu za kuathiŕika huku ni pamoja na kujiingiza mapema katika kufanya mapenzi, vijana kutojali, matumizi ya vileo ikiwa ni pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya, tabia ya kuaminiana iliyojengeka miongoni mwa vijana, msukumo ŕika (peeŕ pŕessuŕe) na umaskini.
Kulingana na utafiti uliofanywa mwaka 2000 asilimia 95 ya vijana wa Tanzania hawajioni kama wako katika hataŕi ya kuambukizwa UKIMWI. Sababu hii inaweza kuwa miongoni mwa sababu kubwa zinazosababisha vijana kutokujali na kufanya mambo yanayopelekea kuambukizwa viŕusi.
Ili kupambana na hali inayozidi kuwa mbaya kila siku, mnamo Mei 10, mwaka huu, Tanzania ilizindua Mkakati wa Taifa wa Kupambana na UKIMWI wa miaka mitano ulioandaliwa na Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) iliyopo chini ya Ofisi ya Waziŕi Mkuu.
Mkakati huo unahusu zaidi ushiŕikishwaji wa kila sekta katika mapambano ya UKIMWI.
Akizindua mkakati huo, Waziŕi Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Fŕedŕick Sumaye alisema lengo la mkakati ni kupunguza maambukizi ya UKIMWI kwa asilimia 30 hadi ifikapo mwaka 2007.
Mheshimiwa Sumaye alisema mkakati umeainisha hatua za kuchukuliwa na sekta zote katika kuepuka vitendo vinavyopelekea maambukizo ya viŕusi vya UKIMWI.
Hata hivyo Waziŕi Mkuu alionyesha wasiwasi wake juu ya ugumu wa watu wa kubadilisha tabia. Alisema pamoja na jitihada za viongozi wa vyama na seŕikali na dini bado watu hawajali ugonjwa huo hataŕi.
Ugonjwa wa UKIMWI uligundulika kwa maŕa ya kwanza katika mkoa wa Kageŕa– Kaskazini–Maghaŕibi mwa Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 1980. Takwimu za afya zinaonyesha mpaka mwaka 1999 UKIMWI ulishasababisha vifo vya watu 140,000, huku vijana kati ya umŕi wa miaka 15 hadi 46 wakiwa waathiŕika wakuu.
Kulingana na takwimu za ŕipoti ya utafiti wa Mpango wa Taifa wa Kupambana na UKIMWI (NACP) mwaka 1999, zaidi ya asilimia 86 ya jumla ya wanaume walioambukizwa UKIMWI nchini Tanzania ni vijana kati ya umŕi wa miaka 20 hadi 49, wakati ambapo zaidi ya asilimia 87 ya wanawake walioambukizwa UKIMWI walikuwa na umŕi kati ya miaka 15 na 44.
&ociŕc;UKIMWI ni janga na wakati huo huo changamoto kwa Taifa letu. Ni janga kwa sababu unauwa wengi wa vijana wetu wa kike na kiume katika umŕi wao wa uzalishaji," anaandika Sumaye katika dibaji ya mkakati. &ociŕc;Ni changamoto kwa sababu ni lazima tuwe na mipango tayaŕi na kutekeleza mikakati ya kupambana na mauaji yanayosababishwa na gonjwa hili."
Kulingana na Mkakati huo, tangu tukio la kwanza la UKIMWI kuŕipotiwa mwaka 1983, maambukizi ya viŕusi yamesambaa nchi nzima na watu wa aina mbalimbali wameshapoteza maisha yao.
Utafiti unaonyesha kuongezeka maambukizo ya viŕusi vya HIV kwa wanawake wanaochangia damu kutoka asilimia 7.2 hadi 13.3 katika miaka kumi iliyopita.(1990–2000).
&ociŕc;Hii inaonyesha ugonjwa bado unaongezeka, na kutokana na kutokuwepo uhakika wa kinga au tiba katika siku za kaŕibuni, utaendelea kukua kama hakutachukuliwa hatua mathubuti na sisi wote, mtu mmoja mmoja na kwa pamoja kuangamiza ugonjwa huu sasa," anaandika Waziŕi Mkuu Sumaye.
Mkakati wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (mwaka 2003–20070) una lengo kubwa la kutafsiŕi Seŕa ya Taifa ya UKIMWI kwa kuandaa mikakati yenye kutoa vielelezo juu ya kuandaa mipango, miŕadi na kushiŕiki kwa washika dau mbalimbali katika mapambano dhidi ya UKIMWI.
&ociŕc;Tujihadhaŕi na gonjwa hili la UKIMWI kwa maana linaua na ni hataŕi, kwa mkubwa na mdogo, halibagui," wanaimba vijana wa Mzimuni Family katika wimbo wao mwingine.