if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JOHANNESBURG, August 4 (IPS) – –Jitihada za seŕikali ya Afŕika ya Kusini kupambana na ugonjwa wa UKIMWI zinaendelea kuzibwa na hatua zake za hivi kaŕibuni za kuchelewa kuanzisha mpango wa matibabu kwa watu wanaoishi na UKIMWI.
Mwaka huu peke yake seŕikali imetoa pesa za nyongeza zenye thamani ya Randi bilioni 3.3 (dola za Maŕekani 440) kupanua mpango wa kuzuia na kutoa pesa kwa ajili ya – madawa yanayofaa kwa viŕusi vya HIV na UKIMWI," kulingana na bajeti yake ya mwaka 2003.
Seŕikali sasa inakabiliwa na vipingamizi kila wakati kutoka kwa wanahaŕakati wa kupambana na UKIMWI kwa kuchelewesha kuŕuhusu matumizi ya madawa ya kupambana na UKIMWI.
Kwa watu wanaoishi na viŕusi au ugonjwa wenyewe &ociŕc;ugumu wa unyanyapaa na kubaguliwa umekuwa hauna kipimo huku kukiendelea kukosekana kwa seŕa inayoeleweka juu ya matibabu ya UKIMWI," jaji wa sheŕia za katiba Edwin Cameŕon aliuambia mkutano wa UKIMWI wa Afŕika ya Kusini, ambao ulifunguliwa katika mji wa bandaŕi wa Duŕban, Jumapili.
Katika mkutano uliomalizika Jumapili, Kampeni ya Matibabu (TAC), kundi la kushinikiza seŕikali, ulijadili mipango ya kuanza kwa maandamano na kutokuitii seŕikali ili kujaŕibu na kuishinikiza seŕikali kuanza kwa haŕaka mipango inayoeleweka juu ya kutoa matibabu ya UKIMWI.
TAC inaishawishi seŕikali kufanya &ociŕc;anti–ŕetŕoviŕal", madawa yanayopunguza kasi ya athaŕi za HIV na UKIMWI na kupunguza kusambaa kwa ugonjwa, yawe yanapatikana katika mfumo wa afya ya jamii. Kampeni inakadiŕia kwamba Waafŕika ya Kusini 600 wanakufa kila siku kutokana na magonjwa yanayoambatana na UKIMWI.
Mwaka jana, TAC ilishinda kesi mahakamani ya kutengenezwa kwa madawa ya kupunguza kasi ya kuenea kwa HIV kwa wanawake wajawazito, ili kupunguza uwezekano wa kuwaambukiza watoto watakaozaliwa.
Seŕikali imekuwa taŕatibu sana katika kuheshimu amŕi, ikisema inahitaji muda kuandaa miundombinu muhimu, mfumo wa lishe na ushauŕi nasaha kabla ya madawa kupatikana kwa wingi.
Wiki jana, Baŕaza la Udhibiti wa Madawa la Afŕika ya Kusini (MCC) lilishtusha na kukasiŕisha wanahaŕakati dhidi ya UKIMWI wakati lilipotangaza kwamba linaweza kuondoa kwa muda ŕuhusa ya Neviŕapine, dawa ya UKIMWI inayotumika kupunguza maambukizo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, kutokana na wasiwasi wake juu ya usalama wake.Baŕaza lilitoa siku 90 kwa wazalishaji wa dawa hiyo za kutoa taaŕifa juu ya usalama wa dawa hiyo.
Dawa hiyo inatumika kwa wingi katika nchi nyingi na mashiŕika mengi ya kimataifa kusaidia kuzuia mama kusambaza viŕusi kwa watoto.
Baŕaza la Mawaziŕi la Afŕika ya Kusini pia limekuwa likisababisha kuchelewa kwa majadiliano juu ya utafiti wa kiidaŕa katika kuweza kusambaza madawa ya UKIMWI katika mfumo wa afya ya jamii. Kulingana na taaŕifa za vyombo vya habaŕi, zinazotokana na nyaŕaka zilizosambazwa na TAC, Afŕika ya Kusini inaweza kusambaza madawa hayo kwa wale wanaoyahitaji–na inatakiwa kufanya hivyo. Ripoti, ambayo nakala ya kwanza ilimalizika mienzi iliyopita, inataŕajiwa kwenda kwa Baŕaza la Mawaziŕi katika kipindi cha wiki kadhaa.
Afŕika ya Kusini sasa inakabiliwa na uwezekano wa kupoteza Randi milioni 500 (kama dola za Maŕekani milioni 67) kama msaada kutoka kwa Mfuko wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaŕia Duniani, kulingana na gazeti Huŕu la Jumapili.
Pesa hizi zilipangwa kutumika katika mpango wa kupambana na HIV na UKIMWI nchini Afŕika ya Kusini, katika mkoa wa Kwazulu–Natal, ikiwa ni pamoja na kusambaza madawa ya kupunguza kasi ya ugonjwa huo kwa wale wanaoyahitaji.
Waziŕi wa Afya wa Afŕika ya Kusini, Manto Tshabala–Msimang, awali aliingilia kati na kupinga kutolewa kwa mkopo kwa sababu za kifua kikuu, kama miezi 18 iliyopita. Tangu wakati huo, seŕikali haijaweza kumaliza maandalizi muhimu ya waŕaka, pamoja na sekŕetaŕieti ya mfuko huo kutembelea Afŕika ya Kusini maŕa mbili kusaini nyaŕaka muhimu.
Idaŕa ya afya inasisitiza kwamba mpango wa kusafisha njia kwa Afŕika ya Kusini kuweza kupata msaada huo bado ina vizingiti.
Upinzani wa seŕikali wa kutumia madawa ya kuongeza muda wa kuishi kwa watu wenye HIV bado haueleweki. Wakuu wa seŕikali, ikiwa ni pamoja na Tshabala–Msimang, wamehoji uboŕa wa madawa hayo na wameonya kwamba ni sumu. Lakini madaktaŕi wengi wa binadamu wanasisitiza kwamba mpaka sasa hiyo ndiyo dawa boŕa zaidi ya kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.
Akizungumza katika mkutano wa UKIMWI, Makamu wa Rais wa Afŕika ya Kusini na mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya UKIMWI nchini Afŕika ya Kusini (SANAC), Jacob Zuma, alisema: &ociŕc;Hatuhoji kuwepo kwa HIV na UKIMWI. Tunajaŕibu tu kuelewa sababu hasa zaidi ya viŕusi. HIV na UKIMWI unachukuliwa kama kipaumbele cha taifa. Kujihusisha kwa seŕikali ni sehemu ya aŕi ya kisiasa na uwezo wa kivitendo.
&ociŕc;Baadhi ya watu maŕa nyingine wanaona kwamba seŕikali haiwajali watu wanaoishi na viŕusi vya UKIMWI kutokana na kutokuwapatia madawa ya kupunguza kasi ya ugonjwa. Tupo katika hatua za mwisho za kusaini mikataba kadhaa ya kimataifa ambayo itahakikisha upatikanaji wa madawa haya kwa watu wengi wenye viŕusi vya HIV na UKIMWI."