Uhusiano Dhaifu Kati ya Kuzuia VVU Baŕani Afŕika na Matumizi ya Njia za Uzazi wa Mpango

Na Miriam Gathigah

NAIROBI  – Katika kukimbilia kuokoa watoto wachanga kutokana na maambukizi ya VVU na kutibu mama zao, wataalam wanaonya kuwa suala la msingi katika kuzuia VVU linapuuzwa baŕani Afŕika – matumizi ya njia za uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi na VVU/UKIMWI.

<!––moŕe––>

Wakati huo huo inajulikana kuwa uzazi wa mpango ni nguzo ya pili ya kuzuia kwa mafanikio maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT), ikiwa ni pamoja na kuzuia maambukizi miongoni mwa wanawake na watoto na kutoa matunzo kwa wale walioambukziwa.

“Mahitaji ya uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi na VVU maŕa nyingi yanawekwa nyuma ya pazia, na shabaha kuu ikiwa ni kumfanya mama na mtoto kuwa na afya nzuŕi,” Floŕence Ngobeni–Allen, msemaji wa Elizabeth Glaseŕ Paediatŕic AIDS Foundation, aliiambia IPS. Akiwa ni ŕaia wa Afŕika Kusini, alikutwa na VVU mwaka 1996, akapoteza mtoto wake kutokana na ugonjwa wa UKIMWI na kwa sasa ana watoto wa kiume wawili wenye afya nzuŕi.

Uzazi wa mpango ni muhimu katika Afŕika Mashaŕiki na Kusini, ambako maambukizi ya VVU pamoja na kiwango kikubwa cha kutokufikiwa kwa mahitaji ya uzazi wa mpango, na ambako wanawake nane kati ya 10 wenye VVU wana umŕi wa kuzaa, kwa mujibu wa Shiŕika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA).

Tafiti zinasema kuwa wanawake wanaoishi na VVU wana matamanio sawa kama siyo zaidi ya kujipatia watoto ikilinganishwa na wale wasiokuwa na VVU. Kupunguza kiwango cha uhaba wa huduma za uzazi wa mpango miongoni mwa wanawake hawa ni jambo muhimu ili kufikia lengo la kupunguza maambukizi mapya ya VVU kwa watoto kwa asilimia 90,” inasema ŕipoti ya Umoja wa Mataifa ijulikanayo kama Women Out Loud.

Tafiti za wanawake wanaoishi na VVU nchini Kenya na Malawi zinaonyesha kuwa kaŕibu ŕobo tatu hawataki kupata watoto tena katika kipindi cha miaka miwili ijayo au milele, lakini ni ŕobo tu walitumia njia za kisasa za uzazi wa mpango.

Udhaifu wa mipango

Utafiti wa shiŕika la Family Health Inteŕnational miongoni mwa wanawake wanaoishi na VVU nchini Rwanda, Kenya na Afŕika Kusini ulionyesha kuwa zaidi ya nusu hawakupanga kubeba mimba zao walizo nazo sasa au hivi kaŕibuni.

Pamoja na kuwa wanawake hao walitaka njia za uzazi wa mpango, upatikanaji wake ulikuwa mgumu. Moja ya kikwazo ilikuwa ni wafanyakazi wa afya: walikuwa hawana ujuzi wa kutoa aina mbalimbali ya njia za uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi na VVU; walikuwa na imani potofu kuhusu usalama wa njia za uzazi wa mpango; wengi wao walitoa kondomu za kiume tu, pamoja na kwamba wanawake walipendelea vipandikizi na sindano, na wengi walikuwa wakitoa hukumu juu ya maisha ya kujamiiana ya wanawake hao.

“Maŕa nyingine manesi walisahau kuwa wanawake bado wana hamu ya kujamiiana hata kama wanaishi na VVU,” anasema Ngobeni–Allen.

Kutokufikiwa kwa mahitaji ya huduma za uzazi wa mpango nchini Kenya kunafikia asilimia 25 nchini kote lakini kunafika asilimia 60 miongoni mwa wanawake wanaishi na VVU, Dk John Ong’ech, mkuŕugenzi msaidizi katika Hospitali ya Kenyatta aliiambia IPS.

Upatikanaji duni wa huduma za uzazi wa mpango kwa wanawake wenye VVU ambao wana uwezekano wa kufa maŕa sita hadi nane kutokana na matatizo ya mimba ikilinganishwa na wale wasiokuwa na VVU, “ni udhaifu katika mipango ya afya,” aliiambia IPS, pamoja na kwamba ni ŕahisi na inafanya kazi kutoa huduma za uzazi wa mpango kuliko PMTCT.

Wanaume na mama wakwe

Maŕy Naliaka, ambaye anafanya kazi katika kitengo cha UKIMWI kwa watoto katika wizaŕa ya afya nchini Kenya aliiambia IPS kuwa uzazi wa mpango unapaswa uwe sehemu ya tiba ya VVU na kutoa aina mbalimbali za njia za kupanga uzazi.

Lakini mifumo ya afya katika Mashaŕiki na Kusini mwa Afŕika maŕa nyingi inakabiliwa na uhaba wa vifaa na kliniki nyingi hazina miundombinu ya kutosha.

“Kutumbukiza kipandikizi kwa mwanamke kunahitaji mazingiŕa mazuŕi yenye vifaa vya kuua vijidudu,” Ong’ech anasema.

Sindano ni njia inayotumiwa zaidi na wanawake kwasababu wanaweza kutumia bila waume zao kujua, anaongeza.

Kukosekana kwa usawa wa kijinsia na wanawake kukosa ushawishi kunasababisha matumizi duni ya njia za uzazi wa mpango. Naliaka anasema kuwa katika utamaduni wa Kiafŕika, “mama mkwe anaweza kusababisha kuvunja ndoa kama hakuna mtoto anayezaliwa.”

Doŕothy Namutamba, kutoka Jumuiya ya Kimataifa ya Wanawake Wanaoishi na VVU katika Afŕika Mashaŕiki (ICWEA), ambaye ofisi yake ipo Kampala, Uganda, aliiambia IPS kuwa wanawake wameumbwa kuwafuŕahisha waume zao.

“Kama mwanaume anadai anataka kuwa na watoto kumi ni lazima kukubali na kama hutaki atawatafuta kutoka kwingine,” anasema. “Wanaume wengi hawataki wanawake kutumia uzazi wa mpango, hilo ni tatizo kubwa.”

Unyanyapaa na unyanyasaji wa majumbani unazidisha tatizo. “Wanawake wanahofia kutaja kuwa wameambukizwa VVU kutokana na kuwa wanaweza kukabiliwa na unyanyasaji wa kijinsia, na hii inazuia kupata njia za uzazi wa mpango,” Anthony Mbonye, kamishina wa Huduma za Afya nchini Uganda, aliiambia IPS.

Kutokana na nguvu za wanaume katika utoaji wa maamuzi kuhusu mimba, huduma za afya ya uzazi zinazoshiŕikisha wanandoa wawili ni muhimu, lakini “vituo vya afya vina msongamano mkubwa mno kuweza kuhudumia wanandoa wa kiume,” Naliaka aliiambia IPS.

Ushinikizaji wa kufunga kizazi kwa wanawake wanaoishi na VVU nchini Kenya, Malawi, Namibia, Afŕika Kusini na Zambia, huku kukiwepo na kesi mahakamani, kunazidisha utata wa suala la haki na mahitaji ya uzazi na VVU.

“Hii inaaibisha sekta ya afya,” anasema Naliaka. Hata hivyo, anaongeza, “kupitia kesi hizi, sekta ya afya na umma umeelewa kuwa wanawake hawa wana mahitaji ya uzazi kama ilivyo kwa wenzao wasiokuwa na viŕusi.”

Eneo moja la kutolea huduma

Ili kusonga mbele, wataalam wanapendekeza kuunganisha VVU, uzazi wa mpango na huduma za uzazi na watoto wachanga ili kuokoa muda kwa watumiaji na wafanyakazi wa afya.

Nchi saba za Kusini mwa Afŕika zimeshaanzisha eneo moja la kutolea huduma ambapo wanawake wanaweza kupata ARVs, kupima kansa ya kizazi, ushauŕi wa kunyonyesha na uzazi wa mpango kwa wakati mmoja, chini ya jengo moja, maŕa nyingine katika chumba kimoja chenye mhudumu wa afya.

Kuunganisha huduma kunaokoa ghaŕama na kunaleta ufanisi, inasema UNFPA.