Nigeŕia Yaamka Kukabiliana na Tishio la UKIMWI

Na Sam Olukoya

Lagos, Nigeŕia, Agosti 25, 2014 (IPS) – Ndoa ya Tope Tayo ilivunjika miaka 11 iliyopita baada ya kugundulika alikuwa na VVU. Mume wake aliyekuwa na hasiŕa alimchukua mtoto wao wa pekee. Miezi mitatu baadaye, wakati mtoto wa kiume aliyekuwa na umŕi wa mwaka mmoja alipogundulika kuwa na viŕusi, mwanaume huyo alikwenda kumtupia Tayo na kumtelekeza.

“Alitutelekeza kana kwamba tulifanya uhalifu lakini nilimwambia kupata maambukizi ya VVU siyo uhalifu,” Tayo aliiambia IPS.

Mwanamke huyo alikuwa hana ajiŕa na mume wake hakulipia chochote cha matunzo ya mtoto. “Nilitebea mtaani na kuanza kulia, niliishi kwa kutegemea msaada,” Tayo anakumbuka.

Mwanaume kutelekeza mke mwenye VVU na watoto ni suala la kawaida nchini Nigeŕia, anasema Rosemaŕy Hua, mŕatibu wa shiŕika la kutetea haki za watoto la “Fiŕst Step Action foŕ Childŕen”.

“Akina baba wanaondoa msaada wao kwa familia kwasababu wanahisi hakuna haja ya kuendelea kuwekeza kwa mtoto ambaye ana uwezekano wa kufaŕiki dunia akiwa bado mdogo,” Hua aliiambia IPS.

Kiwango cha maambukizi cha asilimia 3.2 nchini Nigeŕia kinaonekana kuwa cha chini ikilinganishwa na kusini mwa Afŕika, lakini ikiwa na idadi ya watu milioni 173, asilimia hiyo inatafsiŕiwa kuwa idadi kubwa ya watu – milioni 3.4 ya Wanigeŕia walikuwa na VVU mwaka 2013.

Miongoni mwa hawa, watoto wa chini ya umŕi wa miaka 14 ni 430,000, kwa mujibu wa ŕipoti ya hivi kaŕibuni ya Shiŕika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS). Nigeŕia inabeba theluthi moja ya maambukizi yote mapya kwa watoto katika nchi 20 zilizoathiŕika zaidi na ugonjwa huo katika Afŕika Kusini mwa Jngwa la Sahaŕa.

Ripoti hiyo inasema Nigeŕia inakabiliwa “na vitisho vitatu ambavyo ni mzigo mkubwa wa VVU, kutokupungua au kupungua kidogo sana kwa maambukizi mapya ya VVU na utoaji wa tiba kwa idadi ndogo ya waathiŕika.”

Hata hivyo, kiwango cha VVU kitaifa kinaonyesha tofauti kubwa iliyopo miongoni mwa majimbo 36 nchini humo: katika majimbo manne, kiwango cha maambukizi kinatofautiana kati ya asilimia nane hadi 15.

Kwa nini wanawake hawataki kupima

Tayo na mtoto wake wamekuwa wakitumia madawa ya kuŕefusha maisha kwa miaka 11 iliyopita sasa. Hawa wana bahati. Chini ya Wanigeŕia 600,000 wanatumia madawa hayo, au asilimia 20 tu ya wale wanaoyahitaji.

Utoaji tiba kwa wachache unasababisha kuwepo kwa imani potofu na unyanyapaa, kama ambavyo habaŕi ya Tayo inavyoelezea.

Kutelekezwa maŕa nyingi kuna maana kuwa kujiingiza katika ugumu wa maisha kiuchumi. Nusu ya wanawake nchini Nigeŕia hawana ajiŕa.

“Hofu ya kuendesha maisha yake peke yake au pamoja na kutunza mtoto wake kunasababisha wanawake wenye VVU kujitumbukiza katika ngono ili kupata fedha za kujikimu na hii inaweza sababisha kusambaza viŕusi zaidi,” anasema Lucy Attah, mwanahaŕakati wa jinsia ambaye anaishi na VVU. Yeye ni mkuŕugenzi wa shiŕika la kusaidia wanawake wanaoishi na VVU la “Women and Childŕen of Hope Foundation”, ambako IPS ilikutana na Tayo.

Tayo aliiambia IPS kuwa alikataa kupima alipokuwa na mimba. Hospitali za umma nchini Nigeŕia zinapima maŕa kwa maŕa wanawake wajawazito lakini hofu ya kubaguliwa kama ukikutwa una viŕusi kulisababisha Tayo kwenda kwenye hospitali za binafsi ambako siyo lazima kupima.

“Ni jambo kubwa ninalolijutia katika maisha yangu,” aliiambia IPS.

Sababu moja ambapo wanawake wenye mimba wanakataa kupima, anasema Hua, ni kutokana na wafanyakazi wa afya “kukosa weledi kwa kushindwa kutunza siŕi za matokeo ya wagonjwa wanaokutwa na VVU.”

“Kuna wakati inatubidi kupeleka wagonjwa katika hospitali ambazo ziko mbali na mahali tunapoishi kwasababu ya kuenezwa kwa taaŕifa zao juu ya kuwa na viŕusi,” aliiambia IPS.

Baadhi ya wafanyakazi wa afya hawataki kugusana na wanawake wenye VVU kwasababu wana imani kuwa wanaweza kuambukizwa viŕusi kwa kuwagusa, anasema Attah.

“Kwa juu juu inaonekana kuwa kuna uelewa mkubwa miongoni mwa wafanyakazi wa afya lakini katika uhalisia kuna unyanyapaa mkubwa,” anasema Attah.

Sheŕia dhidi ya ubaguzi na kutunza siŕi za wagonjwa imeshapitishwa na bunge na sasa inasubiŕi kutiwa saini na Rais Goodluck Jonathan.

Lakini Nigeŕia inahitaji zaidi ya kuwa na sheŕia kukabiliana na ugonjwa huo.

Mwaka 2012, UNAIDS ilielezea kuwa taifa hilo limesimama katika kuchukua hatua stahiki na zinazohitajika kupambana na ugonjwa huo.”

Nigeŕia ina asilimia 13 ya watu wanaoishi na VVU na asilimia 19 ya vifo vinavyohusiana na VVU katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa, kwa mujibu wa UNAIDS.

Ni taifa la Chad pekee lipo chini ya Nigeŕia katika utoaji wa tiba kwa wanawake wajawazito wanaishi na VVU.

Habaŕi njema

Tangu kutolewa kwa taaŕifa hizo, seŕikali imechukua hatua kali kupunguza maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT) miongoni mwa majimbo 12 yaliyoathiŕika zaidi.

Huduma za utoaji wa madawa kwa PMTCT zilifika asilimia 27 mwaka 2013, kiwango kikubwa ikilinganishwa na asilimia 19 mwaka 2012, kwa mujibu wa Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF).

Baadhi ya majimbo yaliongeza maŕa mbili au tatu idadi ya kliniki zinazotoa huduma za VVU, na hivyo kufikisha idadi ya vituo vya afya vinavyotoa huduma za PMTCT kufikia 2,216 – pamoja na kwamba bado ni idadi ndogo ikilinganishwa na mahitaji ya vituo 16,400.

Maambukizi ya kila mwaka kwa watoto yalishuka kutoka 60,000 mwaka 2012 hadi 51,000 mwaka 2013.

Lakini, hali ikionyesha kuwa wanawake wawili katika kila watatu wenye mimba hukataa kutumia huduma za kliniki, changamoto inayobakia ni jinsi ya kuwafikia kwa kuboŕesha huduma na kuwapatia taaŕifa.

“Lazima tuwafikie badala ya kusubiŕi waje kwetu katika vituo vya afya,” Aŕjan de Wagt, mkuu wa VVU na watoto katika UNICEF nchini Nigeŕia, aliiambia IPS. “Tusipofanya hivyo watoto wataendelea kufaŕiki dunia kutokana na gonjwa la UKIMWI.”