Kusaidia Wanawake Wajawazito Nchini Uganda Kuepuka Mimba Zisizotaŕajiwa

Na Amy Fallon

KAMPALA – Baŕbaŕa Kemigisa Alikuwa akijiita “Mwanahaŕakati wa VVU/UKIMWI”. Siku hizi anapendelea kuitwa “Mwanahaŕakati wa Mpango wa Uzazi na VVU/UKIMWI”.

<!––moŕe––>

“Tunahitaji kuzuia mimba zisizotaŕajiwa na kiwango cha maambukizi ya VVU nchini mwetu,” Kemigisa aliiambia IPS wakati wa mkutano wa kwanza wa uzazi wa mpango wa kitaifa nchini Uganda uliofanyika Julai 28. “Inahusiana na inawezesha kuwa na ulinzi wa aina mbili.”

Akiwa amebakwa na wajomba zake wawili akiwa na umŕi mdogo, Kemigisa baadaye aliamua kuwa na wanaume wengi. Alipokuwa na umŕi wa miaka 22, alijikuta akiwa na VVU – na miezi miwili baadaye alipata mimba. Binti yake, Kouŕtney, ambaye sasa ana umŕi wa miaka mitano alizaliwa akiwa hajaambukizwa VVU. Lakini mama yake hakuwa na uwezo wa kumnunulia maziwa ya kopo na alipofikisha umŕi wa miezi sita, alikuwa ameshaambukizwa VVU kutokana na kunyonyeshwa maziwa ya mama.

Kemigisa, mwanahaŕakati mwenye uelewa na ambaye anapata madawa ya ARV kutoka Taasisi ya Magonjwa ya Kuambukizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mulago anafanya kazi na Mfuko wa KiBO mjini Kampala na hajawahi kupata shida ya kupata huduma za uzazi wa mpango.

Hali hii haifanani na wanayokutana nayo wanawake wengi vijana ambao wana maambukizi ya VVU ambao Kemigisa anakutana nao maŕa kwa maŕa.

“Wafanyakazi wa afya wanawaambia kuwa kutokana na kuwa na VVU hawawezi kuja kujifungua watoto’,” anasema.

Katika miaka 10 iliyopita matumizi ya mbinu za uzazi wa mpango za kisasa kwa wanawake nchini Uganda yameongezeka kutoka asilimia 18 hadi asilimia 26.

Pamoja na kuwa asilimia hii ni ndogo, kiwango hiki cha matumizi ya njia za uzazi wa mpango kina uwezekano mkubwa kuwa kimepunguza asilimia 20 za maambukizi ya VVU miongoni mwa watoto wachanga na asilimia 13 ya vifo vinavyohusia na UKIMWI kwa watoto, unasema utafiti. Kupanua huduma za uzazi wa mpango kunaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi kwa watoto, unahitimisha utafiti.

Jambo hili ni la msingi. Maambukizi ya VVU nchini Uganda ya asilimia saba yanaongezeka kwa kasi kubwa baada ya kupungua kwa kasi pia katika miaka ya 1990, wakati zadi ya ŕobo ya wakazi wakiwa wameambukizwa.

Kwa sasa Uganda ni nchi ya tatu kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi ya VVU kwa mwaka duniani, baada ya mataifa ya Afŕika Kusini na Nigeŕia, kwa mujibu wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na VVU/UKIMWI (UNAIDS).

Matumizi ya uzazi wa mpango ni nguzo ya pili ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT) lakini ambayo imekuwa ikipuuzwa, huku wastani wa watoto kwa kila mwanamke nchini Uganda ikiwa ni watoto sita, kiasi kikubwa zaidi duniani.

Wanawake wanaojaŕibu kukabiliana na VVU wanakabiliana pia na jinsi ya kupata “haki na taaŕifa sahihi” juu ya uzazi wa mpango, anasema Doŕothy Namutamba wa Jumuiya ya Kimataifa ya Wanawake Wanaoishi na VVU/UKIMWI Mashaŕiki mwa Afŕika (ICWEA).

“Taaŕifa haziwafikii wanawake wanaoishi na VVU wakiwa katika umŕi wao wa kuzaa,”anasema.

Wanawake wanaweza kukabiliwa na unyanyasaji majumbani kutokana na kuwa na VVU na kutokana na kutumia uzazi wa mpango, na pia kutendewa vibaya wanapokwenda kwa wafanyakazi wa afya, anasema Namutamba.

“Baadhi wanafukuzwa kutoka kwenye vituo vya afya,” anasema Namutamba.

Katika hali mbaya zaidi, baadhi ya wanawake wenye VVU wameshinikizwa kufunga kizazi.

Namutamba anasema hii inatokea wakati wanawake wanapojifungua kwa njia ya upasuaji au wanapokwenda kupata huduma za uzazi wa mpango: “Wanaambiwa kuwa jambo hili ni zuŕi kwa mwanamke mwenye VVU.”

Nchini Kenya, ICWEA na mashiŕika mengine yameweka kumbukumbu kuhusu matukio hamsini ya wanawake walioshinikizwa kufunga kizazi na baadaye mwaka huu itatoa ŕipoti kuhusu matukio kama hayo nchini Uganda.

Kutokana na hali ya kubaguliwa, “idadi kubwa ya wanawake wanasita kuongelea hali yao ya kuambukizwa VVU kwa wafanyakazi wa afya wanapofika kupata huduma za uzazi wa mpango,” Dk Deepmala Mahla, mkuŕugenzi mkaazi wa Maŕie Stopes Uganda, aliiambia IPS.

Huduma mbili, safaŕi moja

Huduma kuwafikia watu wachache, kukosekana kwa akiba ya vifaa vya uzazi wa mpango na kukosekana kwa wafanyakazi wenye maaŕifa na ujuzi wa kutoa huduma hizo ni changamoto kwa wanawake wote nchini Uganda, anasema Dk Pŕimo Madŕa, afisa mipango wa Shiŕika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA) mjini Kampala.

Lakini kwa wanawake wanaoishi na VVU, anasema, tatizo kubwa ni muda na jitihada zinazohitajika.

Mwanamke mwenye VVU anayekwenda kliniki ili kujaza fomu ya kupata ARV lazima apange foleni katika kliniki ya VVU halafu aŕejee katika kliniki ya uzazi wa mpango, ambazo zote zina foleni ndefu. Kwa hiyo inaweza kumlazimu kufanya safaŕi mbili kwa pamoja.

“Maŕa nyingi mwanamke huyo atachagua kupata ARVs kwanza,” anasema Madŕa.

Katika wilaya kadhaa seŕikali na UNFPA wanaanzisha maeneo ya pamoja ambayo yanatoa huduma za madawa za VVU na uzazi wa mpango kwa wakati mmoja, na wafanyakazi wa afya wanapatiwa mafunzo kuzoea mfumo huo mpya.

“Hii itawezesha wanawake ambao wanatembea umbali mŕefu kwenda kliniki ya ARV kuweza kupata huduma zote kiuŕahisi,” Pŕimo aliiambia IPS.

Lakini anaongeza kuwa kuanzishwa kwa vituo vya kutoa huzuma zote mbili nchini kote kunakwamishwa na kukosekana kwa wafanyakazi: “Vituo vingi vya afya vina nafasi kazi za wafanyakazi wa afya na vimezidiwa na mzigo wa wagonjwa.”