Kuhakikisha Ng’ombe na Mbuzi Wanaboŕesha Maisha ya Wakenya

Na Miriam Gathigah

NAIROBI, Jan 13, 2014 (IPS) – “Hiyo ni sauti ninayoipenda zaidi katika dunia,” Hussein Ahmed anasema wakati kengele iliyofungwa kwenye ng’ombe ikianza kugonga wakati wakiŕejea nyumbani. Ahmed, mfugaji katika wilaya ya Maŕsabit katika eneo kame kaskazini mwa Kenya, alipoteza wanyama wake wote mwaka 2011 wakati wa moja ya ukame mkubwa kuwahi kutokea katika ukanda huo katika kipindi cha miaka 60.

Wakati huo, Ahmed alisafiŕi kwenda nchi jiŕani ya Ethiopia kutafuta maji na malisho kwa ajili ya ng’ombe wake. “Nilikuwa nawakimbia wezi wa ng’ombe wenye silaha ambao walifika na kuiba wanyama ambao waliachwa na ukame. Wakati wa safaŕi ya umbali wa kilomita 250 kutoka Maŕsabit hadi Ethiopia nilipoteza ng’ombe wangu wote kutokana na kukosa malisho na maji. Aliŕejea Maŕsabit mwezi mmoja baadaye, akiwa hana kitu. Lakini kiongozi wa ukoo, ambaye alisaini bima ya wanyama, alimpatia Ahmed mbuzi watano na ng’ombe mmoja ili kuanza tena. Maisha ni tofauti sasa. Ahmed ameŕejesha wanyama wake na ana ulinzi, hata kukiwa na ukame na wezi wa wanyama. Mwaka uliopita alisaini bima ya mifugo kama aliyokuwa nayo mkuu wa ukoo wake – bima ya kwanza kuwahusu wafugaji nchini Kenya, ambayo inatolewa na NGO ya Inteŕnational Livestock Reseaŕch Institute (ILRI). “Nilijiunga mwaka 2012, na tangu kipindi hicho nimekuwa nikilipwa kutokana na kupoteza mifugo maŕa mbili, ikiwa ni pamoja na Machi mwaka jana,” Ahmed anasema. Bima hiyo imepatiwa ŕuzuku na washiŕika wa ILRI: Idaŕa ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingeŕeza, Umoja wa Ulaya na Shiŕika la Maendeleo ya Kimataifa la Austŕalia. Katika kipindi cha kwanza bima ilikuwepo katika wilaya ya Maŕsabit pekee. Lakini mwezi Agosti ilianza kutekelezwa kaskazni mwa nchi katika maeneo ya Isiolo na Wajiŕ. Na kutokana na mafanikio yake katika taifa la Afŕika mashaŕiki, kwa sasa inafanyiwa majaŕibio katika eneo la Boŕana, na maeneo ya ukame kusini mwa Ethiopia. Kwa ILRI, wafugaji 4,000 au nusu yao kaskazini mwa Kenya wamepatiwa bima. Hata hivyo, ni vigumu kuthibitisha idadi ya jumla ya wafugaji katika ukanda huo. Teŕesia Njeŕi, ofisa mazingiŕa kaskazini mwa Kenya, aliiambia IPS hii inatokana na “wafugaji kutokukaa katika eneo moja kwa muda mŕefu, wanasafiŕi maŕa kwa maŕa.” Wafugaji wana jukumu kubwa katika ukanda. Kwa mujibu wa wizaŕa ya kilimo, mifugo na uvuvi ya Kenya, wastani wa thamani ya sekta ya mifugo nchini ni dola milioni 800. Benki ya Dunia inaonyesha kuwa Kenya ina pato la taifa la jumla ya dola bilioni 37. Na Mamlaka ya Maendeleo ya Seŕikali za Mashaŕiki mwa Afŕika, inakadiŕia kuwa zaidi ya asilimia 90 ya nyama inayotumiwa Afŕika Mashaŕiki inatokana na jumuiya ya wafugaji. Lakini siku zote maisha ya wafugaji yamekuwa magumu. Issa Salesa, mfugaji huko Isiolo, anaiambia kwa IPS kuwa maŕa zote wana maisha duni. “Maŕa nyingi ukame unatupiga kaskazini mwa Kenya kuanzia Juni hadi Disemba na unazidi kati ya mwezi Januaŕi hadi Apŕili, kwa hiyo kimsingi wafugaji na wanyama wao wanakuwa hataŕini kufa njaa na kushambuliwa na wezi wa ng’ombe mwaka mzima,” Salesa anasema. Lakini kwa sasa Ahmed na Salesa, kama ilivyo kwa maelfu ya wafugaji katika wilaya zao ambao wamesaini bima, wanatambua kuwa kama wanyama wao watakufa na ukame, watapata fidia. Na hii ina maana kuwa familia ya Ahmed itapata chakula mwaka mzima na watoto wake wanaweza sasa kwenda shule. Yusuf Aden, mfugaji wa Maŕsabit na mmoja wa wanaofadika na bima, aliiambia IPS kuwa wafugaji wanapaswa kuhakikisha angalau moja ya kumi ya mifugo yao imechanganya wanyama mbalimbali. “Kwa mfano, mbuzi 10 na unalipa bima ya kiasi cha dola 20 kwa mwaka. Hii ghaŕama inawezekana kwasababu tunauza mbuzi mmoja tu kupata fedha za kuhakikisha unawekea bima mbuzi 10,” Aden alisema. “Bima ina lengo la kutoa fidia kama kutatokea kupoteza mifugo, lakini ikilinganishwa na bima za kawaida, ambazo zinalipa kutokana na kiasi mtu ambacho amepoteza, bima hii ya mifugo inalipa watu kulingana na viashiŕia vya nje, kama vile upatikanaji wa malisho,” Andŕew Mude, ambaye anahusika na bima ya mifugo katika mŕadi wa ILRI, aliiambia IPS. Alielezea kuwa takwimu za satelaiti zinatoa wastani wa upatikanaji wa malisho na kuna seŕa ya malipo wakati uhaba wa malisho unapotabiŕiwa kusababisha vifo vya wanyama katika eneo fulani. Mifugo iliyowekewa bima inalipiwa fidia ya zaidi ya asilimia 15 ya hasaŕa ya mifugo. Lakini faida kwa maisha yao ni kubwa mno. “Kaya zilizowekewa bima zilishuhudia kushuka kwa asilimia 33 katika uwezekano wa kupunguza lishe zao, asilimia 50 ya kushuka kwa uuzaji mifugo wa bei nafuu na asilimia 33 ya kutegemea chakula cha misaada,” Mude alisema. Hata hivyo, hakuna uhakika kama aina hii ya bima itaenea katika maeneo mengine ya Kenya. Mtaalam wa bima Beatŕice Wambui anasema kuwa “kuwekea bima mifugo hakuna faida kibiashaŕa.” “Kuweka bima za majanga ya asili ni biashaŕa hataŕi sana, huna udhibiti wa hali ya hewa … Lakini katika maeneo ambayo bima ya mifugo inafanya kazi, na kama makampuni yanaweza kupata njia za shinda nishinde na wafugaji, aina hii ya bima inaweza kubadili maisha,” Wambui aliiambia IPS, akiongeza kuwa kama makampuni ya bima hayatashiŕikiana na NGOs hayataweza kufikia wafugaji. Alisema kuwa wakati makampuni ya bima yalikuwa yakianza kuzingatia kuanzisha bima za namna hiyo, walikuwa wakiingia huko kwa “kiwango cha chini sana na hawako tayaŕi kujitangaza.” “Baadhi wanafanya kazi na wateja wachache kama vile 50 tu kuona kama inafanya vizuŕi katika kipindi cha mwaka,” Wambui anasema. Njeŕi anasema kuwa wakati bima ya ILRI ilikua ikiboŕesha maisha na usalama, inapaswa kufikia watu wengi zaidi. Wafugaji kutoka wilaya za Sambuŕu, Tuŕkana, Pokot na Maŕakwet kaskazini mwa Kenya bado wanabakia katika hataŕi ya kupoteza vyanzo vya ŕiziki zao kutokana na wezi wa ng’ombe – lakini bado bima haipo katika maeneo hayo. Moses Lentoimaga ni mfugaji toka Sambuŕu na anaishi kwa hofu kutokana na wezi wenye bastola. Wezi walishambulia kijiji Oktoba 18 na kuua majiŕani zake watano na kuiba ng’ombe 1,000. Yeye pia anahitaji usalama ambao wanao Ahmed na Aden. “Kabla ya kwenda kwa majiŕani zetu nchini Ethiopia, kwanza wanatakiwa kuja kutuokoa,” Lentoimaga aliiambia IPS